Habari

1,949 watunukiwa vyeti, leseni za uuguzi, ukunga

WAHITIMU 1,949, wametunukiwa vyeti vya usajili na leseni za Uuguzi na Ukunga huku serikali ikisema, itaendelea kuchukua hatua kwa wauguzi na wakunga wanavunja sheria na miiko ya taaluma bila kuwaonea, ili wasiwachafue wauguzi wengi wanaofanya kazi nzuri za kuwahudumia wananchi kwa kufuata maadili ya taaluma.

Alikabidhi vyeti hivyo, Mwenyekiti wa Baraza la Uuguzi na Ukunga, Profesa Lilian Msele, alisema kuwa idadi ya wauguzi imekuwa ikiongezeka kadri siku zinavyoendelea.

Álisema kuwa Serikali ya Awamu ya Sita imekuwa ikitoa kipaumbele katika masuala ya afya, ili wananchi wapate huduma bora na kuweza kushiriki shughuli za maendeleo.

Aliwataka kwenda kusimamia maadili na weledi na baraza litaendekea kusimamia viwango vya taaluma.

Msajili wa Baraza la Uuguzi na Ukunga, Agnes Mtawa Álisema kuanzia mwaka 2016 mpaka sasa jumla ya wakunga 50 waligundulika na vitendo vya uvunjifu wa maadili, ambapo wanne kati yao walifutwa kabisa kwennye daftari la usajili na 46 walipewa onyo kali.

Muuguzi Mkuu wa Serikali Ziada Sella aliwataka kwenda kufanya kazi kwa kuzingatia maadili huku wakiheshimu mila na desturi .

” Kujiheshimu na kutunza heshima ya taaluma, usipokee rushwa au kuombaomba hela kwa wagonjwa ,” alisema

Kati ya watunukiwa hao 112 ni ngazi ya cheti, ngazi ya diploma ni 1,450 na shahada ni 387

 

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button