Habari

Achraf Hakimi atuhumiwa ubakaji

WAENDESHA mashtaka nchini Ufaransa wameanza uchunguzi wa awali kuhusu tuhuma ya ubakaji inayomkabili beki klabu ya PSG na Taifa la Morocco Achraf Hakimi.

Mwanamke mwenye umri wa miaka 24 ambaye hakutajwa jina amemshutumu mchezaji huyo kuwa alimbaka akiwa nyumbani kwake Februari 25, 2023 katika Jiji la Paris.

Kwa mujibu wa BBC Sport mwanamke huyo aliripoti tukio hilo katika kituo cha polisi siku ya Jumapili lakini hakufungua mashtaka. Ofisi ya mwendesha mashtaka wa umma inayoshughulikia kesi hiyo huko Nanterre, ilikataa kutoa maoni lakini ilithibitisha kuwa uchunguzi umeanza.

Hakimi alizaliwa Hispania, alikuwa mchezaji muhimu wakati Morocco ilipoweka historia kwa kufika nusu fainali ya Kombe la Dunia nchini Qatar, timu ya kwanza ya Kiafrika kufanya hivyo.

Ubora wake ulimwezesha kutunukiwa tuzo za Fifa zilizofanyika jijini Paris Jumatatu jioni, ambapo aliteuliwa katika timu ya mwaka ya dunia  ya FIFPro ya wanaume.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 alisimama jukwaani kuchukua tuzo hiyo pamoja na washindi wengine wakiwemo wachezaji wenzake wa PSG Kylian Mbappe na Lionel Messi.

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button