

RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesema serikali imeamua kukuza sekta ya kilimo na kuifanya sekta hiyo kuingiza asilimia 10 ya ukuaji wa uchimi nchini ifikapo mwaka 2030.
Akizungumza leo Machi 19, 2023 katika maadhimisho ya miaka miwili ya urais wake katika Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam, Rais Samia amesema wakulima wengi kwa sasa ni vijana wa kiume, hivyo kesho watazindua shamba la kwanza la vijana Dodoma.
Rais Samia amesema kwa umoja wao watafanya kilimo cha kisasa, chenye tija na biashara pia na kwamba mashamba ya aina hiyo yataanzishwa nchi nzima.
Amesema wameamua kuja mpango wa unaosema ‘Jenga Kesho Nzuri’ kwa ajili ya vijana kupitia kilimo wenye nia ya kujenga maisha mazuri kwa vijana.
“Badala ya kupita na kuzurura na kusikitika hakuna pesa mfukoni waende wakazalishe ili mifuko ijae fedha mfukoni”.amesema Rais Samia.