Habari

Ajali kitonga hakuna kifo, majeruhi

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Allan Bukumbi amethibitisha kutokea kwa ajali ya Basi la Kampuni ya New Force katika eneo la Mlima Kitonga mkoani Iringa leo.

Akitolea ufafanuzi, RPC Bukumbi amesema basi hilo lenye namba za usajili T 448 DDT lilokuwa likitokea mkoani hapo kuelekea Dar es Salaam, lilibeba abiria 57, hakuna kifo wala majeruhi.

Ametaja chanzo cha ajali hiyo kuwa ni baada ya dereva wa basi hilo kuyapita mabasi ya mbele na kushindwa kurudi upande wake wakati akishusha mlima huo.

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button