Habari

Ajali ya treni yaua 12 Uturuki

WATU 12 wamepoteza maisha na wengine kujeruhiwa baada ya treni mbili kugongana nchini Uturuki.

Tukio hilo lilitokea jana jioni nje ya Jiji la Larissa wakati treni hilo likitokea mji wa Athens kwenda Kaskazini mwa jiji la Thessaloniki na kugongana na treni nyingine ya mizigo.

“Tulisikia kishindo kikubwa kwa takribani sekunde kumi,” alisema Stergios Minenis, abiria ambaye aliruka baada ya ajali kutokea.”

Gavana wa eneo la Thessaly Konstantinos Agorastos aliiambia SKAI TV kwamba mabehewa manne ya kwanza ya treni ya abiria yalikatika katika ajali hiyo, na mabehewa mawili ya kwanza yalishika moto.

 Imeelezwa abiria wapatao 250 walio na majeraha madogo wamehamishwa salama kwa basi kwenda Thesaloniki.

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button