Teknolojia

Apple kuboresha iPhone 12 Ufaransa

KAMPUNI ya Kielektroniki ya Apple inakusudia kuboresha simu aina ya iPhone 12 nchini Ufaransa, baada ya hofu kuhusu mionzi, Waziri wa masuala ya kidijitali wa nchi hiyo anasema.

Jean-Noel Barrot alisema Apple itafanya hivyo katika siku zijazo.

Uuzaji wa iPhone 12 ulisitishwa nchini Ufaransa baada ya mdhibiti kugundua mionzi mingi ya sumaku umeme.

Apple iliambiwa kurekebisha suala hilo. Kampuni hiyo ilisema sasisho jipya litatumika tu kwa watumiaji nchini Ufaransa, ambapo ilisema itifaki maalum ya majaribio ipo.

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button