Biashara

Bandari Mtwara yavuka lengo usafirishaji makaa ya mawe

BANDARI ya Mtwara imevuka lengo la usafirishaji wa makaa ya mawe kutoka tani 402, 000 kwa mwaka mpaka kufikia tani milioni 1.003 ndani ya miezi saba.

Kaimu Meneja wa Bandari hiyo Mhandisi Norbert Kalembwe, amesema hayo wakati wa ziara ya Naibu Katibu Mkuu (Uchukuzi) wizara ya Ujenzi na Uchukuzi, Dk Ally Possi katika bandari hiyo kujionea maendeleo na kuweka mikakati zaidi ya kuiwezesha bandari hiyo kukuwa zaidi kibiashara.

“Mpaka sasa performance yetu tuko kwenye tani milioni moja na kama elfu tatu hivi, kiasi ambacho tumesafirisha kwa kipindi cha miezi saba kufikia mwezi Januari,” amesema.

Kalembwe amesema bandari hiyo iliwekewa lengo la kusafirisha makaa ya mawe tani 402,000 Kwa mwaka, lakini ulinganisho unaonesha wamevuka lengo mpaka kufikia asilimia 150.

Makaa hayo ya mawe yanasafirishwa na Kampuni ya Ruvuma Coal na Jitegemee huku Kalembwe akisema kampuni nyingine zaidi zimeanza kutumia bandari kwenye usafirishaji wa makaa ya mawe.

“Tumekuwa na maendeleo mazuri, kiasi kikubwa cha makaa ya mawe sasa hivi kinasafirishwa, tumekuwa na meli nyingi, bandika bandua , inatoka meli inaingia meli,” amesema.

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button