Biashara

Dk Ashatu Kijaji asisitiza uwajibikaji TBS

DAR ES SALAAM: Waziri wa viwanda na biashara Dk Ashatu Kijaji leo Septemba 18, 2023 ametembelea shirika la viwango Tanzania (TBS) ikiwa ni muendelezo wa dhamira yake ya kutembelea taasisi zote zilizopo chini ya wizara hiyo.

Katika ziara hiyo waziri huyo amekagua utendaji kazi wa shirika hilo huku pia akiafuatilia utekelezaji wa bajeti kwa mwaka wa fedha ya 2023-2024 ilioanza kutekelezwa Julai 2023.

Ziara hiyo iliambatana na kutembelea maabara 4 kati ya 9, ikiwemo maabara ya chakula, ngozi, nguo na kemia.

Dk Ashatu Kijaji ameridhishwa na utendaji kazi Katika shirika hilo na kujionea changamoto mbalimbali na kuwashauri kufanya ushirikiano na Taasisi zingine ili kurahisisha kazi zao na kuhakikisha ubora,ufanisi na usalama kwa mtumiaji.


Hata hivyo ametoa wito kwa waagizaji wa bidhaa kutoka nje ya nchi wakikishe zinakaguliwa Ili kulinda afya za watanzania, na wenye Viwanda vya ndani kuhakikisha bidhaa zinakaguliwa na TBS kabla ya matumizi.

Kaimu mkurugenzi Mkuu wa TBS Lazaro Msasalanga amesema ziara imekua ya manufaa kwao Kwakua changamoto alizoziona Waziri itakua rahisi kuzitatua

 

 

 

 

 

 

 

 

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button