Habari

  • Bunge la ridhia mkataba wa bandari

    BUNGE limeridhia Azimio la serikali kuhusu Mkataba baina ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Dubai juu ya Ushirikiano wa Kiuchumi na Kijamii wa Uendelezaji na Uboreshaji wa Utendaji Kazi wa Bandari Tanzania. Azimio hilo liliwasilishwa na Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa akisisitza kuwa pamoja na Serikali kuchukua hatua mbalimbali za maboresho ya…

    Read More »
  • Ulinzi, usalama bandarini kusimamiwa na serikali

    Tofauti na inavyosemwa na baadhi ya watu katika mitandao ya kijamii, Waziri wa Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa amesema pamoja na uwekezaji utakaofanyika bandarini, suala la ulinzi litabaki mikononi mwa Serikali. Amesema “jukumu la Ulinzi na Usalama katika Bandari ya Dar es Salaam litaendela kusimamiwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia vyombo vyake vya Ulinzi na Usalama”

    Read More »
  • Bandari Tanga, Mtwara hazihusiki

    Kuhusu tetesi kwamba DP World watawekeza katika bandari zote nchini, Waziri wa Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa amesisitiza kwamba uwekezaji huo hautahusisha bandari zote nchini. Amesema kwamba katika Awamu ya Pili ya Mkataba huo, chombo kitakachokuwa na mamlaka ya kuchagua bandari zinazoweza kuhusika katika uwezekezaji huo katika bandari za Bahari na Maziwa, ni TPA (Mamlaka ya Bandari Tanzania). Aidha amesema uwekezaji…

    Read More »
  • Ajira za watanzania kipaumbele uwekezaji bandarini

    “Uwepo wa ajira za Watanzania hususan watumishi wa bandari ya Dar es Salaam ni kipaumbele kikubwa cha Serikali sio tu katika Azimio hili bali katika kila aina ya uwekezaji ambao nchi itaufanya. Ibara ya 13 ya Mkataba huu inaitaka DP World kuendeleza ajira za watumishi wote waliopo, kuwaajiri Watanzania pamoja kuwaendeleza kitaaluma. Vile vile Mkataba huu umeweka bayana sharti kwa…

    Read More »
  • Meli Bandari ya Dar kuweka nanga saa 24

    SERIKALI imesema mashirikiano ya kiuchumi na kijamii ya uendelezaji na uboreshaji utendaji kazi katika bandari nchini kati ya Tanzania na Dubai utapunguza muda wa meli kukaa nangani kutoka siku 5 kwa sasa mpaka masaa 24. Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa ameliambia Bunge kuwa azimio lililowasilishwa na Serikali bungeni lina manufaa na kwamba mpango huo utapunguza gharama za…

    Read More »
  • Shehena Bandari ya Dar es Salaam kufikia tani milioni 47.57

    MAKUBALIANO yanayopendekezwa katika Azimio la serikali kuomba Bunge kuridhia mashirikiano kati ya Tanzania na Dubai yanalenga kuongeza shehena inayohudumiwa kutoka tani milioni 18.41 za mwaka 2021/22 hadi kufikia tani milioni 47.57 mwaka 2032/33, sawa na ongezeko la asilimia 158. Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa ameliambia Bunge kuwa mbali na shehena, gharama ya usafirishaji wa mizigo kutoka nchi…

    Read More »
  • Mapato ya bandari kufikia Sh Tril 27- Mbarawa

    WAZIRI wa Ujenzi na Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa amesema mapato ya serikali yatokanayo na kodi ya forodha inayokusanywa katika shehena inayopitishwa bandarini yanategemewa kuongezeka kutoka Sh trilioni 7.76 za mwaka 2021/22 hadi Sh trilioni 26.7 mwaka 2032/33. Vilevile ajira zinazotokana na shughuli za bandari zitaongezeka kutoka 28,990 mwaka 2021/22 hadi ajira 71,907 ifikapo mwaka 2032/33. ⤵️

    Read More »
  • Mkataba huu una ukomo ila..

    “Kuhusu muda, Mkataba huu utakuwa hai mpaka pale ambapo shughuli za miradi zitasitishwa au kuisha kwa muda wa mikataba ya nchi mwenyeji na mikataba ya miradi. Msingi wa Mkataba huu kuendana na mikataba ya miradi ni kutokana na kwamba unaweka msingi unaowezesha kuingia na kutekelezwa kwa mikataba hiyo nchini. “Iwapo Mkataba huu utakuwa na ukomo kabla ya kuisha mikataba ya…

    Read More »
  • TPA inaweza kutafuta wawekezaji wengine

    “Mkataba huu unatoa haki ya upekee ya kufanya majadiliano kwa Awamu ya Miradi iliyoanishwa kwenye Mkataba huo kwa kipindi kisichozidi miezi kumi na mbili (12). Msingi wa kutoa haki hii ya kipekee ni kuwezesha pande mbili kufanya majadiliano na kumpa uhakika Mwekezaji kujadiliana katika maeneo pasipo kuwepo kwa majadiliano na Mwekezaji mwingine katika maeneo hayo hayo. Hivyo, iwapo kipindi hicho…

    Read More »
  • Profesa Mkumbo: Bandari haijauzwa

    MBUNGE wa Ubungo Profesa Kitila Mkumbo (CCM) amesema Azimio lililowasilishwa na Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi halihusu kuuzwa kwa bandari za Tanzania na kwamba linahusu uendelezaji na uboreshaji wa utendaji wa bandari. Amesema Chama cha Mapinduzi (CCM) kisinge ruhusu serikali yake kuuza bandari kwa sababu sio sera ya CCM. “Rais Samia Suluhu Hassan ambaye ndiye Mwenyekiti wa CCM kamwe asingeruhusu…

    Read More »
Back to top button