Habari

  • Man United kumkosa Lisandro Martinez

    BEKI  wa Manchester United, Lisandro Martinez atakuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu kutokana na majeraha ya mguu aliyopata mwezi Aprili. Taarifa zinaeleza beki huyo wa Argentina alipata mshtuko katika mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Arsenal mapema mwezi huu, Man United imeripoti. Martinez sasa anaunga na Luke Shaw, na Aaron Wan Bissaka ambao wote wameumia.

    Read More »
  • Wafanyabiashara wachangiana ukarabati wa madarasa

    BAADHI ya wafanyabiashara na wawekezaji katika maeneo mbalimbali wilayani Rorya mkoani Mara wameanzisha mkakati wa kukarabati wa madarasa na upanuzi wa shule za msingi walizosoma kwa lengo la kuunga mkono juhudi za Rais Samia Suluhu Hassan aliyelenga kuboresha sekta ya elimu. Wawekezaji watano waliowekeza katika mikoa ya Mwanza, Kigoma na Mara wakiongozwa na mfanyabiashara wa mazao mkoani Kigoma Hunga Marwa…

    Read More »
  • Wema: Nimetimiza miezi 9 sijagusa pombe

    DAR ES SALAAM: Msanii wa filamu nchini Wema Sepetu amesema miongoni mwa vitu alivyofanikiwa mwaka huu ni kuacha pombe, kwani tangu Januari hajaigusa. Akizungumza kwenye sherehe ya siku yake ya kuzaliwa, Wema amesema mwaka huu ameona afanye sherehe kwani ni miaka mingi hajafurahia siku yake ya kuzaliwa. “Sijasherekea siku yangu ya kuzaliwa siku nyingi, miaka kama 5, nafanyaga kawaida lakini…

    Read More »
  • Waziri Kairuki akutana na Rais wa Utalii Duniani

    SAUDIA ARABIA; Riyadh. Waziri wa Maliasili na Utalii, Angellah Kairuki amekutana na kufanya mazungumzo na Rais ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Utalii Duniani (World Travel Tourism Council (WTTC) , Bi. Julia Simpson kwa lengo la kujadili namna bora ya kushirikiana katika kutangaza na kukuza utalii endelevu nchini Tanzania. Kikao hicho kilifanyika kwenye ukumbi wa hoteli ya Four…

    Read More »
  • Mwakinyo: Nina asilimia 5 kupanda ulingoni

    DAR ES SALAAM: BONDIA Hassan Mwakinyo amesema ana asilimia 5 tu za kupanda ulingoni kwenye pambano lililopangwa kupigwa leo Septemba 29, 2023 kuwania mkanda wa IBA na mpinzani wake Julius Indongo Kupitia mitandao yake ya kijamii Mwakinyo ameandika: “Maswali na simu zimekuwa nyingi, kiukweli mpaka sasa nina asilimia 5 tu za kupanda ulingoni ikiwa zitaongezeka ni mimi mwenyewe nitasema. “Naomba…

    Read More »
  • Mwakinyo msimamo ni uleule,

    DAR ES SALAAM: BONDIA Hassan Mwakinyo amesema ana asilimia 5% tu za kupanda ulingoni kwenye pambano lililopangwa kupigwa leo septemba 29, 2023 la kuwania mkanda wa IBA na mpinzani wake Julius Indongo Kupitia mitandao yake ya kijamii Mwakinyo ameandika… “Maswali na simu zimekuwa nyingi, kiukweli mpaka sasa nina asilimia 5 tu za kupanda ulingoni ikiwa zitaongezeka ni mimi mwenyewe nitasema,…

    Read More »
  • Napoli yakanusha kumdhihaki Osimhem

    KLABU ya Napoli imesema video iliyopostiwa Septemba 26,2023 kupitia ukurasa wa Tiktok wa klabu hiyo ikionesha kumkejeli, mshambuliaji, Victor Osimhen haikuwa na lengo la kumdhihaki. Jana Septemba 27, 2023, Mnaigeria huyo akiwakilishwa na wakala wake walitishia kuishtaki klabu hiyo kwa kitendo hicho ambacho kimetafsiriwa kama dhihaki na kumkosea heshima nyota huyo. Napoli wamesema: “Kwa vyovyote vile, ikiwa Victor angeona kosa…

    Read More »
  • Mwakinyo agomea pambano la kesho

    BONDIA Hassan Mwakinyo amesema hatopanda ulingoni kupigana dhidi ya Bondia Julius Indonga kwenye pambano la kuwania mkanda wa IBA International kesho. –Mwakinyo amesema uamuzi huo umetokana na uwongo na udanganyifu wa Mapromota.–Kupitia ukurasa wake wa Instagram Mwakinyo ameandika kuwa “Kwetu kama wachezaji wa ndani naomba niweke hisia zangu wazi kwa mashabiki ya kuwa kesho sitaweza kupanda ulingoni kutokana na uwongo…

    Read More »
  • Watoto wajitokeza utalii Karibu Kusini

    IDADI kubwa ya watoto imejitokeza kushuhudia Maonesho ya Utalii ya Karibu Kusini yanayoshirikisha mikoa 10 ya Kusini hatua iliyopongezwa na wadau wa utalii waliosema wamepata fursa ya kujifunza. Diwani wa kata ya Mkimbizi, Elliud Mvella ni mmoja wa wadau aliyeonesha kufurahishwa kuona kuna idadi kubwa ya watoto katika maonesho hayo yanayofanyika kila mwaka mjini Iringa akisema: “Sio jambo la kubeza…

    Read More »
  • Viongozi wananufaika migogoro ya ardhi

    MOROGORO; Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Adam Malima amesema migogoro mingi ya ardhi ndani ya mkoa huo ina sura mbaya,ni ya kutengenezwa na wapo watu wakiwemo viongozi  wananufaika na migogoro hiyo kimyakimya. Hivyo amewaagiza wakuu wa wilaya kufanya tathimini ya migogoro ya ardhi katika maeneo yao ambayo wataisimamia na itaratibiwa na wakurugenzi  wa kila halmashauri, ili hatua za kisheria ziweze…

    Read More »
Back to top button