Habari

Julio aanza mikakati msimu mpya

BAADA ya kuinusuru KMC kushuka daraja, Kocha Mkuu wa timu hiyo Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ amesema tayari ameanza mikakati ya kukisuka upya kikosi chake kwa ajili ya msimu ujao.

Akizungumza na HabariLEO, kocha huyo ameeleza kuwa anachotaka ni kuona msimu ujao timu hiyo inakuwa tishia na kuwa miongoni mwa timu zinazowania ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

“Kazi yangu kubwa ilikuwa ni kuinusuri timu isishuke daraja nashukuru tumefanikiwa kwani tumeondoka katika janga hilo kwa sasa tunapambana tushinde mechi zetu mbili zilizobaki ili tusicheze Play- Offs, kitu kama mkuu wa benchi la ufundi nimeshaanza kujenga KMC ya msimu ujao kwa kusajili wachezaji wenye viwango bora hilo linawekana sababu hii ni timu inayojiweza,” amesema Julio.

Mwishoni mwa wiki iliyopita KMC, iliifunga Singida Big Stars mabao 2-0, katika mchezo uliopigwa uwanja wa Uhuru Dar es Salaam, matokeo ambayo yaliiweka sehemu salama timu hiyo huku ikisaliwa na michezo miwili kabla msimu huu kumalizika.

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button