Biashara

Kihenzile ataka kasi zaidi TRC

NAIBU Waziri wa Uchukuzi, David Kihenzile na Wakuu wa Wizara hiyo leo Septemba 18,2023 wametembelea Shirika la Reli Tanzania (TRC).

Pamoja na kujitambulisha pia ilikuwa fursa muhimu ya kufahamu kwa kina majukukumu ya Shirika, kazi wanazofanya ikiwemo utekelezaji wa miradi ya kimkakati na mipango ya shirika.

Akizungumza katika ziara hiyo, Kihenzile ameitaka TRC kuongeza kasi ya usimamizi wa miradi na kuzingatia thamani ya fedha.

” Maono ya Rais Dk Samia Suluhu Hassan ni kuona taifa letu linakuwa kitovu cha usafirishaji kwenye Ukanda wetu wa Afrika Mashariki, Kusini na Kati kwa kutumia fursa ya kimkakati tuliyopewa na Mungu.” Amesema Kihenzile na kuongeza

“Hivyo ni lazima kuongeza kasi zaidi katika kuhudumia mizigo mingi na abiria wengi kutoka bandarini na kuleta mizigo bandarini.” Amesema

Amesema, Wizara ya Uchukuzi chini ya Waziri wake Prof Makame Mbarawa na wataendelea kuweka mkazo mkubwa kwenye kuboresha usafiri wa reli , viwanja vya ndege, Meli na kufanya mageuzi makubwa kwenye bandari ili kuongeza tija.

 

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button