Habari

Kila goli Simba, Yanga CAF Sh mil.10

RAIS Samia Suluhu Hassan ameongeza fedha za motisha kwa timu za Simba na Yanga kutoka Sh milioni 5 hadi Sh milioni 10.

Rais atatoa fedha hizo  endapo timu hizo zitafuzu kucheza nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika na Kombe la Shirikisho.

Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa leo Aprili 28, 2023 amesema magoli yatakayolipiwa shilingi milioni 10 ni yale yatakayofungwa katika dakika 90 za mchezo au dakika 120 na sio magoli ya penalti.

Amesema, Rais Samia anazitakia kila la heri Simba na Yanga na amewataka wachezaji kujituma uwanjani na kutumia maarifa yao yote kuhakikisha wanashinda michezo ya kukamilisha hatua ya  robo fainali ili wafanikiwe kuingia nusu fainali, ambapo kila goli litakuwa shilingi milioni 10.

Simba inacheza mchezo wa marudiano leo Aprili 28, 2023 saa nne usiku kwa saa za Afrika Mashariki dhidi ya Wydad Casablanca nchini Morocco,  wakati Yanga watawakaribisha Rivers United ya Nigeria katika mchezo wa marudiano utakaofanyika kwenye Uwanja wa Benjamini Mkapa  jijini Dar es Salaam.

Simba inacheza mchezo wa marudiano ikiwa na mtaji wa ushindi wa 1-0 ilioupata katika mchezo wa kwanza wa robo fainali uliofanyika katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam wakati Yanga itacheza mchezo wa marudiano ikiwa na mtaji wa ushindi wa 2-0 ilioupata ugenini huko nchini Nigeria.

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button