Teknolojia

Laini zisizohakikiwa kufungiwa Feb.13

SERIKALI imetangaza kuzifungia laini za simu ambazo hazijahakikiwa ifikapo Februari 13, 2023.

Akizungumza leo Januari 24, 2023 Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye amesema mpaka Januari 19, 2023 kuna watumiaji wa simu 60,739, 790 kati ya Watanzania milioni 61.

Amesema :“Utapeli mwingi unaendelea na jambo hili linaongezeka, kupitia Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA) tulichukua hatua za kufanya usajili kwa kutumia alama za vidole na vitambulisho, zoezi hili lilianza Januari 5, 2019 na kufungwa Desemba 2021,”amesema Nape na kuongeza:

“Kila laini iliyokuwa imelengwa kwa wakati ule ilisajiliwa.”

Amesema Februari 13, 2023 kama namba haijahakikiwa basi namba hiyo itazimwa, na kama kuna mtu alisajili namba kwa jina la mtu mwingine basi ajisalimishe kimaandishi iwapo namba hiyo itafanya uhalifu basi atachukuliwa hatua.

“Kama namba haijahakikiwa hiyo namba itazimwa, laini nyingi mtaani watu wametumia vitambulisho vya watu wengine kusajili na zinatumika kufanya utapeli. Laini tunazoenda kuzifungia ni zile zilizosajiliwa kwa uongo, tumelenga kuwaondoa matapeli kwenye mfumo.

“Tumeongeza siku nyingine 14 hivyo ikifika Januari 13, 2023 siku moja kabla ya siku yawapendao, anga la mawasiliano liwe salama, hatutaki zile meseji ‘ile nauli tuma kwenye namba hii’, saa 10 jioni kama kuna laini itakuwa haijahakikiwa itakuwa mwisho wa kutumika kwake,”amesisitiza.

Nape amewataka wananchi ambao hawajahakiki namba zao kufanya hivyo kabla ya Januari 13 kwa kupiga *106# ili kuhakiki namba yako kama imesajiliwa au la!

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button