HABARI

Mbeya : Wahudumu wa Bar kuanza kuvaa Mask

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila, ametengua kauli yake ya kuzifunga baa zote ifikapo saa tatu usiku aliyoitoa jana wakati wa kikao na waandishi wa habari, badala yake ziendelee na shughuli kama kawaida huku tahadhari zaidi zikichukuliwa ili kukabiliana na maambukizi ya Virusi vya Corona.

Chalamila ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na wamiliki wa Bar mkoani Mbeya ambapo wamiliki hao wamemuahidi kwamba watahakikisha wanachukua tahadhari ya ugonjwa huo, kwa kuwapatia wahudumu Barakoa pindi wanapohudumia wateja wao, pamoja na kufunga kumbi za starehe (Disko).

Kwa mujibu Mwandishi wa EATV Mbeya Grace Mwakalinga, amesema kufuatia mapendekezo hayo, ikapelekea Mkuu wa Mkoa kubadilisha agizo lake la kuzuia Bar kufanya kazi.

Publisher

Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button