Habari

Messi kugawa Iphone za kibabe Argentina

Nahodha wa timu ya Argentina na klabu ya PSG ya Ufaransa, Lionel Messi ameagiza iPhones za Dhahabu 35 zenye thamani ya £175,000 ( Sh milioni 490) kwa ajili ya wachezaji na wafanyakazi wote wa Argentina walioshinda Kombe la Dunia 2022.

Ben Lyons, Mkurugenzi Mtendaji wa iDesign Gold, ameliambia gazeti la The Sun kuwa “Lionel Messi ni mmoja wa wateja waaminifu zaidi wa IDESIGN GOLD na aliwasiliana nao miezi michache baada ya fainali ya Kombe la Dunia.

Alisema Messi alitaka zawadi maalum kwa wachezaji na wafanyikazi wote kusherehekea ushindi huo lakini hakutaka zawadi ya saa.

Kila simu ina jina la mchezaji na namba ya jezi ya timu ya taifa na nembo ya Argentina iliyochongwa juu yake nyuma ya simu hizo.

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button