Teknolojia

Nape mgeni rasmi Lugalo Openi 2023

WAZIRI wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nauye anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika ufungaji wa shindano la “Lugalo Open 2023” litakalo fanyika Machi 25 na 26 Lugalo Gofu jijini Dar es salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Klabu ya Gofu ya Lugalo Brigedia Jenerali Michael Luwongo, amesema muitikio wa wachezaji ni mkubwa ambapo wachezaji kutoka vilabu mbalimbali ndani na nje ya nchi watashiriki shindano hilo.

“Witikio ni tofauti na tulivyotegemea wachezaji wamejitokeza kwa wingi kushiriki mchezo huo, wajiandae vixuri kwa kuwa hata wakimataifa wanajiandaa zaidi.” amesema Brigedia Jenerali Mstaaafu Michael Luwongo Mwenyekiti wa Lugalo Gofu.

Naye Katibu wa Hendcape wa Chama Cha Mchezo wa Gofu nchini TGU Mhandisi Enok Magile amesema, Lugalo Gofu imekuwa bora katika kuandaa mashindano mbalimbali ya mchezo wa gofu, hivyo anatarajia shindano hilo litakuwa bora Zaidi.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Wateja Binafsi wa Beki ya NBC ambao ndio Wadhamini wakuuu wa shindano hilo Elibariki Masuke amesema, anaushukuru uongozi wa Lugalo Gofu kwa kuwashirikisha mara kwa mara katika mashindano yao na wataendelea kudhamini mashindano mbalimbali ili kukuza zaidi mchezo huo.

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button