Habari

Nusu fainali Angeline Jimbo Cup kupigwa Septemba 20

MASHINDANO ya Angeline Jimbo cup yanatarajia kuendelea Septemba 20 mwaka huu kwa mchezo mmoja wa nusu fainali katika uwanja wa shule ya msingi Sabasaba wilayani Ilemela utakaokutanisha kata ya Kirumba dhidi ya Nyakato.

Mchezo wa pili wa nusu fainali utachezwa Septemba 21 kata ya Ibungilo itacheza dhidi ya kata ya Shibula.

Mchezo huo pia utachezwa katika uwanja wa Sabasaba wilayani Ilemela.

Naye Katibu Mkuu wa Chama cha soka Wilaya ya Ilemela(IDFA), Almas Moshi ameziomba timu zote nne zilizoingia hatua ya nusu fainali kuhakikisha zinajiandaa vyema na kuzingatia muda wa kufika uwanjani wakati wa mashindano hayo.

Naye katibu wa mbunge wa jimbo la Ilemela Charles David amewaomba makocha na viongozi wa vilabu vya ligi kuu na ligi ya championship kujitokeza katika mashindano hayo na kuweza kuchagua wachezaji watakaoweza kusaidia katika timu zao.

Amesema mshindi wa mashindano hayo atapokea fedha taslimu Sh milioni 2.5 pamoja na kikombe huku nafasi ya pili atapokea Sh milioni 2.

Amesema nafasi ya tatu atapokea Sh milioni 1.5 huku nafasi ya nne atapokea Sh milioni

Amesema kwa upande wa timu timu yenye nidhamu na timu ya mashabiki bora zote zitapokea shilingi 500,000/- kwa kila timu.

Amesema mwamuzi bora na mwandishi bora watapokea Sh 300,000 huku mchezaji bora atapokea shilingi 200,000/-.

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button