Habari

Rostam Aziz aomba radhi

MFANYABIASHARA Rostam Aziz ameomba radhi kufuatia taarifa iliyotolewa na Chama cha Majaji na Mahakimu Tanzania ya kumtaka kuthibitisha shutuma alizozitoa dhidi ya Mahakama ya Tanzania.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Julai 4, 2023 jijini Dar es Salaam mfanyabiashara huyo amekubali kuwa aliteleza wakati akitoka kauli yake ambayo ilioneknaa kuishushia hadhi Mahakama ya Tanzania.

“Nakiri kwamba niliteleza, na uungwana ni kuomba msamaha ninaomba radhi kwa kauli yangu iliyowakwaza watu” amesema Rostam.

Rostam amesema uwekezaji wa sekta binafsi katika bandari una faida kubwa katika ustawi wake.

Ikumbukwe June 26 Rostam Aziz aliishutumu mahakama  hiyo akitilia shaka maamuzi yanayoweza kutolewa na mahakama akisema haina uhuru kwenye maamuzi yake na leo ametoka hadharani na kuomba radhi kwa kauli yake hiyo.

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button