Simulizi

Siku zote jifunze kutokana na makosa ya wengine

Mimi ni binti wa miaka 24, ndiyo nimemaliza chuo mwaka huu hata nyumbani bado sijaenda, kuna mwanaume nilikua naye kipindi niko chuo, alikua ananihudumia kwa kila kitu hata ada alikua ananisaidia kulipa. Nilikua namuona kama mume wangu, alinitambulisha kwa baadhai ya ndugu zake na mimi nilimtambulisha mpaka kwa Mama yangu.

Wakati nakaribia kumaliza chuo aliniambia kuwa nibebe mimba yake ili iwe rahisi kujitambulisha kwetu. Kaka mimi nakusoma lakini sikusita kubeba mimba kwani nilijua kabisa ni kama mume wangu kutokana na vitu alivyokua ananifanyia. Nilibeba mimba kweli na sasa hivi ujauzito una miezi 7.

Nilipomuambia kuwa aje kwetu kujitambulisha ili niweze kwenda kujifungua vizuri aliakataa,a kaniambia kimila zao ni mpaka nijifungue ndiyo anawez akuja kwetu. Mimi nilikubali nikampigia simu mama yake kumuambia kuwa nitaenda kwao kujitambulisha, kwanza alianza kucheka, ni Mama ambaye alishanipeleka mpaka wkake na kunitambulisha kua ni Mama yake mzazi.

Siku hiyo ndiyo akaniambia kuwa yeye si Mama yake mzazi bali huyo kijana ni mteja wake wamezoeana,huyo Mama anauza chakula mbona wanawake zake wengi anakuja nao tuhapa kunitambulisha, halafua na mke na familia yake iko Mwanza. Huyo Mama aliniambia, nilimuuliza mwanaume mwanzo alikataa lakini baadaye alikubali kuwa yeye kaoa na aliniambia nibebe mimba ili iwe rahisi nisijekumuacha.

Nikimuambia kuhusu mimi mipango yake ananiambia atahudumia mtoto, Kaka mwanaume baada ya hapo aliondoka, nilikua nikimpigia simu hapokei na meseji hajibu, kufuatilia kumbe mradi wao umeisha, yeye ni injinia hivyo mradi ukiisha anaondoka, hata tulipokua tukiishi naye kapangishiwa na kampuni hivyo natakiw akuondoka.

Kaka siwezi kurudi kwetu nah ii mimba, nimehangaika mpaka nimejua anapoishi na mke wake, nawaza niende hukohuko ili mke wake ajue kuwa kuna mtoto mwingine anakuja au nifanye nini? Naomba ushauri wako Kaka ninajua ulishaongelea hili swala lakini nimekwama na sijui nifanye nini? Naomba unipostie nipate na mawazo ya watu wengine!

Said Abdullah

^ SENIOR C E O & PUBLISHER ^ Software engineering ^ Fan of programming ^ Technology Enthusiast.. ^ System developed|C,C++&java 👇Get more news and updates

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button