Simulizi

SIMULIZI |NILIPOFUNGWA GEREZA LA WANAWAKE KIMAKOSA SEHEMU YA – 01 HADI 05

SEHEMU YA (01 —-05)

“Na kesi imehairishwa mpaka tarehe ishirini na moja ya mwezi ujao, mtuhumiwa aende gerezani kwa sababu ya shtaka lake hili zito hatoweza kuwekewa dhamana, mpaka upelelezi utakapokamilika!” Hakimu aliongea akiinuka na mavazi yake ya kijaji na kofia yake maalumu kichwani

“wote simama!” yule askari maalumu aliamrisha watu wakasimama wote mahakamani kwa ajili ya Hakimu ambae alitoka, na mimi nikiwa na mavazi yangu ya kawaida ya uraiani nikashikwa na askari wawili wa kike nikiwa nimefungwa pingu mikononi kwa nyuma tayari kupelekwa kwenye karandinga la askari magereza ili wanipeleke gerezani kama mfungwa mahabusu nikisubiri kesi yangu kusikilizwa kwa mara ya pili

Kwakweli leo niliona kama dunia imenigeukia mimi, mbingu zimehamia chini na ardhi imehamia juu, nikiwa siamini kwa mara ya kwanza ndiyo ninaenda kuingia gerezani hata kama sijahukumiwa bado lakini ndiyo nitakaa wiki mbili mpaka tarehe ya kesi yangu itakapofika na kama ikihairishwa tena huenda nikakaa siku nyingine zaidi kama ujuavyo mambo ya kimahakama

Nilishushwa tukiwa tunatoka nje ya mahakama, nikiwa sipo peke yangu kama mtuhumiwa, nikiwa na wanawake wengine takribani saba wote tukiwa na kesi tofauti tofauti lakini zikishahabiana, mimi nikiwa na kesi ya kukutwa na madawa ya kulevya, wakati huo wakili na mwanasheria wangu alikuwa akinikimbilia nyuma nyuma akitaka kuongea kitu na mimi akawasimamisha askari

“una shida gani?” askari magereza mmoja wa kike alimwuliza
“nataka kuongea na mteja wangu sekunde chache!”
“haturuhusu!”
“kwa sheria gani?” wakili alimwuliza askari huyo aliyemtazama askari mwenzake ambae alitikisa kichwa kumruhusu wakili wangu azungumze na mimi akiogopa kufunguliwa vifungu vya sheria na wakili huyo msomi ambae sheria ipo kichwani

“naam kaka!” nilimwitikia nikibana sauti yangu kama mtoto wa kike kama kawaida yangu

“nitakuja kesho kutwa tuzungumze Reshma sawa?”
“sawa kaka wakili jitahidi ushughulikie mimi sijawahi kufungwa jamani?” niliongea kwa sauti ya kike huku nikijiliza
“sawa na kuna mzigo wako nitakueletea usijali hautokaa mda mrefu utatoka!”
“sawa nakuamini!”

Nilimjibu nikashikwa na askari safari kuelekea nje ya mahakama kwenye gari (karandinga) la askari magereza

Kiukweli kwa jinsi nilivyovaa hakuna ambae angejua kama mimi ni mwanaume, kwa kuwa nilikamatwa kwenye mazingira hayo, ilibidi tu nivumilie na kuendelea kujifanya mwanamke hivyo hivyo ilimradi nisikumbane na dhahama au kashkash wanazokutana nazo watuhumiwa wa kiume na kama ningegundulika kuwa mwanaume na nimejifanya kuwa mwanamke basi huenda ningeongeza kesi na kuonekana ni kweli mimi ni muhalifu kwa kitendo tu cha kujifanya mwanamke wakati wala siyo muhalifu lakini nilikuwa kwenye harakati tu za kukwepa kufanya tukio la uhalifu ambalo nililazimishwa kulifanya bila mimi kutaka

Mpaka nasomewa kesi kwa mara ya kwanza na kutolewa sasa kupelekwa kwenye karandinga la magereza nilikuwa na mavazi yangu, baibui jeusi na refu ambalo hapo awali wakati nakamatwa lilinifunika mpaka uso nikawa naonekana macho tu lakini mahakamani nilifunuliwa nikitakiwa uso uonekane lakini kutokana na make up nilizopakwa na urembo usoni niliopakwa na wabobezi wa mambo ya urembo ukichanganya na sura yangu nzuri niliyoirithi kutoka kwa mama yangu mzazi, hakuna ambae angedhani kuwa mimi ni mwanaume, maana ndefu zote zilikwanguliwa (nitawaeleza huko mbeleni kwanini nimekuwa hivi)

Na urijali wangu nikiwa mwanaume niliyekamilika kila kitu, nilikuwa ndani ya baibui langu refu nikipakizwa ndani ya karandinga la magereza, pamoja na watuhumiwa wa kike halisi, safari kuelekea gerezani kwa mara ya kwanza kwenye maisha yangu, nikiwa nimewahi kulala mahabusu tu kituo cha polisi lakini siyo gerezani kabisa, hii ndiyo ikiwa mara ya kwanza kwenye maisha yangu

Nilikaa ndani ya basi nikitazama tu nje dirishani nikiwaza na kuwazua yatakuwaje maisha hayo ya gerezani ambayo ninasikia watu wakisema ni magumu sana sana na ya mateso, nikashusha pumzi ndefu nikijikaza kiume nikiwa nimekaa na mfungwa mwenzangu mwanamke ambae alikuwa yupo siriasi hacheki na mtu, akionekana ni mtu mkorofi sana aliyefanya matukio ya kutosha mtaani maana amekaa kiume kiume tu

“samahani hivi wewe nawe ni mara yako ya kwanza kuingia gerezani au!?” nilimwuliza nikijaribu kumsemesha akageuka na kunitazama kwa sekunde kadhaa na sura yake ya ukauzu

“mimi gerezani ni kama nyumbani!” alinijibu jibu lililonimaliza nguvu nikatikisa kichwa tu, na muda huo huo askari alipiga mayowe ya kuamrisha tushuke wote tukashuka kwenye karandinga hilo la magereza kumbe tulikuwa tumeshafika kwenye gereza na ndipo niliposhuhudia lango la gereza mbele yangu kwa mara ya kwanza nikiingia ndani ya gereza, tena gereza la wanawake na mimi ni mwanaume…….

Inaendelea

NILIPOFUNGWA KWENYE GEREZA LA WANAWAKE KIMAKOSA

SEHEMU YA 02
na @King Author
WhatsApp 0629980412
utapata story 3 kwa 2000 tu

Nilibaki nikipepesa pepesa macho nikiwa siamini amini kama ndiyo kweli naingia gerezani kwa mara ya kwanza

“tembea wewe!” askari mmoja wa kike aliyekuwa nyuma yangu alinisukuma kumbe nilikuwa nimejisahau nikasimama bila kujua nikawa nimeduwaa baada ya kusukumwa ndipo nikashtuka kutoka kwenye bumbuwazi,

Tulifika mpaka sehemu ya mapokezi kwa askari mmoja ambae alipewa karatasi ya majina yetu, akatutazama na kutukagua kagua kisha tukapelekwa mpaka chumba maalumu cha kubadilisha mavazi, tuyatoe yale tuliyokuja nayo ya kiraia ili tuvae sare za kimahabusu tufanane na wengine, mtihani ukawa upo hapo, tuliingizwa wote saba kama tulivyo, tukaanza kubadilisha nguo, askari huyo wa kike akiwa nje anatusubiria

Wanawake hao wafungwa mahabusu wenzangu walianza kuvua nguo zao mbele yangu wakijua mimi ni mwanamke mwenzao nikabaki nimeganda nimesimama natazama pembeni nikikwepa kuwatazama maana mambo lazima yabadilike kama mwanaume unapomwona mwanamke akiwa mtupu (uchi) na nikagundulika bure kama siyo mwanamke, ni mwanaume kamili tena rijali

Wakati nikiwa nimegeukia pembeni nisiwatazame wanawake hao mmoja alikuja huku huku mbele yangu akisimama akiwa uchi hana nguo

“ohooo huyu nae vipi?” nilijisemea kimoyomoyo nikageuza kutazama upande wa pili kumkwepa nikakutana na wale wengine bado baadhi nao wakiwa uchi wengine wakiwa wamevaa tayari sasa nikawa nimefanya ‘ushubwada’ kama vijana wa sasa waitavyo, nakwepa kumtazama mmoja najikuta nawatazama wengine wanne, ikabidi nigeukie kwa huyu huyu aliyekuwa peke yake huku ndo dah! nilijikuta kwenye wakati mgumu maana alikuwa ameinama yaani amebong’oa akihangaika kuvaa suruali ya sare ya mahabusu makalio yake ameyaelekezea kwangu akiwa amevaa chupi tu, Jogoo wangu akasimama dede ndani ya baibui nililovaa lakini kwa sababu lilikuwa pana pana nikanusurika kujulikana

“mbona huvai shosti umeganda tu hapo?” aliniuliza
“ndo navua hapa namimi ngoja nije nikusaidie naona unapata tabu” nilijibu huku nikizuga kulishusha baibui langu lakini nikivua kwa mahesabu nisije kujulikana kama siyo mwanamke mwenzao

“njoo unisaidie tu utakuwa umefanya la maana shosti maana hii nguo mh changamoto”
“sawa!” nilimwitikia nikibana sauti yangu kama ya kike na uzuri kipaji hicho nilikuwa nacho tangu shuleni cha kuiga sauti za watu maarufu na mpaka wanawake, mpaka nilipata kesi siku moja nilipokuwa sekondari kidato cha tatu, nilipowatangazia wanafunzi wenzangu darasani kwetu kuwa kuna kikao cha wazazi nikiiga sauti ya mwalimu mkuu wa kike huku nikiwa nimejibanza wasinione na nikawaruhusu waondoke shuleni kama utani lakini kwakuwa hawakuniona nilijibanza na sauti ya mwalimu mkuu naipatia haswa wakaniamini na kuondoka shuleni kabla ya kengele ya mwisho ya kutoka madarasani kupigwa

Jambo hilo lilinifanya nipewe adhabu ambayo sikuwahi kuipata, nitandikwe bakora zisizo na idadi, tena siyo kwa mwalimu mmoja ila wote shule nzima, adhabu ambayo sitokaa niisahau kamwe, yaani maisha yangu yote

Nilimsogelea yule mfungwa wa kike mahabusu mwenzangu aliyekuwa akihangaika kuvaa suruali yake ya sare bila mafanikio nikachuchumaa akiwa na chupi tu tena kifuani akiwa wazi matiti yake yananing’inia nikaanza kumsaidia kumvalisha, mimi nikiwa hata bado sijaanza kuvaa zangu

“uuuwiii!” alishtuka nilipomshika mguu akihisi kama ameguswa na kitu cha tofauti, nadhani alihisi kama kutekenywa hivi sababu ya jinsia yangu kwa hiyo ile kanuni ya ‘hasi na chanya ilifanya kazi yake, au ile ya sumaku na chuma’ kuvutana

“kulikoni mbona tunashtuana?” mmoja aliuliza, wote waliokuwa pembeni wakitushangaa

“hamna kanigusa tu kwenye kidonda mguuni niliumia!” yule mwanadada alizuga
“pole na samahani kama nimekuumiza!” nilimwambia kama kawaida kwa sauti yangu ya kike
“asante usijali!” aliniambia huku akitabasamu na kunitazama usoni, machoni kwa sekunde kadhaa akinikazia macho yake

“hey hey hamjamaliza tu mnadhani mpo majumbani mwenu mnajipodoa?” yule askari aliyetuleta aliongea kwa ukali akiupiga mlango kwa nguvu na kutushtua mle ndani kila mtu akaanza kuhangaika haraka haraka kumalizia kuvaa, kazi ikiwa kwangu kulivua juba langu, haraka haraka nikaanza kulivua wote wslipokuwa wakihangaika kuvaa nami nikiwa nimegeukia ukutani lakini yule niliyemsaidia kuvaa suruali yake ya sare alikuwa bado akinitazama, nadhani hakuwa na uhakika namimi,

Wote walikuwa wameshamaliza kuvaa wakitoka ndani ya chumba hicho haraka haraka nikabaki mimi tu peke yangu nikihangaika kuvaa na ndipo yule askari akaingia na mwenzake wakiwa na virungu vyao mikononi, wote wakiwa askari magereza wa kike kutokana na kuwa ni gereza la wanawake, wakiwa na kofia zao vichwani

“halow kwahiyo wewe ndo husikii amri?” askari yule mwingine aliniuliza huku akigonga gonga kirungu chake kwenye mkono wake akimaanisha hakuna usalama kwangu, wote wawili wakinifuata

“hapana afande nguo tu ilikuwa inanisumbua halafu nilikuwa namsaidia yule paa…. le mwenza……ngu!” nilijitetea kwa sauti ya kike kama kawaida yangu huku nikirudi kinyume nyume kwa wasiwasi

“hapana afande nini nini na nini, unaongea kama upo chumbani na mumeo… tumfanyaje huyu afande?” askari mwenzake alinijibu kwa kubana sauti akiiiga sauti yangu iliyoonekana kama ya mapozi sana huku akimwuliza afande yule mwingine

“huyu ni wa kutandikwa mpaka ajinyee, aelewe hapa siyo kwa mumewe, ni gerezani”……

Inaendelea………

NILIPOFUNGWA KWENYE GEREZA LA WANAWAKE KIMAKOSA

SEHEMU YA 03

naa @King Author
WhatsApp 0629980412
utapata story 3 kwa 2000 tu

“sogea hapa!” askari mmoja wapo aliniita kwa amri nikamsogelea kiuwoga uwoga, woga wangu ukiwa siyo kwa ajili yao maana walikuwa ni warembo tu mmoja akiwa mwanamama wa makamo mwenye shepu siyo ya kitoto, akiwa amevalia sare zake za askari, nguo zimemshika ipasavyo na kumchonga hipsi zake na nyuma sasa ndo dah, alijaaliwa msambwanda mwanamama huyu uliojichora kwenye suruali yake ya sare aliyochomekea, na mwingine akiwa ni mwanadada tu mdogo mdogo

Kilichonitisha kwao ni virungu vyao vya chuma walivyoshika mikononi ambavyo kama wangenitandika navyo basi nisingebaki salama ningebaki na maumivu makali pamoja na ‘manundu’ ya kutosha mwilini

“naam… abee afande!” nilijikuta nikichanganya namna ya kuitikia kwa vile ni mwanaume niliyejifanya mwanamke kuna baadhi ya mambo yakinishinda kwa sababu kila jambo nililotakiwa kulitenda ilikuwa lazima nilipange kichwani kabla ya kulitenda, askari wale wawili wakatazamana

“unaitikia naam umekuwa mwanaume wewe dada kwani?” mmoja aliniuliza
“hapana samahani afande!” nilijibu nikitikisa kichwa kwa msisitizo

“afande Jane afande Rukia!” mara wakaitwa nje

“ndiyo afande!”
“ndiyo afande!” wote wakaitikia kwa pamoja muito huo kutoka kwa askari aliyewazidi cheo huku wakipiga saluti ingawa hawakumwona bado

“njooni!” aliwaita
“wewe nenda kaungane na wenzako kule!” mmoja aliniamrisha huku wakitoka

“sawa afande!” nilijibu namimi nikitoka haraka haraka huku nikiyaweka weka maziwa yangu (ya bandia) vizuri kifuani, yaliyokuwa yakiteremka teremka kila mara, lakini kichwani nikiwa na mtandio wangu ule kama mwanadada wa kiislamu huku sababu sheria zikiruhusiwa, ila nguo zikiwa ni sare za kifungwa na namba ya mfungwa (mahabusu)

“wewe njoo hapa!” mara nikasikia nikiitwa na sauti nzito ya kiume kugeuka hivi nikamwona askari mmoja baba mtu mzima aliyekuwa mwanaume peke yake amekaa kwenye kiti akinitazama, nikamsogelea

“naam… abee afande!” nilijikuta nachanganya tena habari kwenye uitikiaji
“unaitwa nani?” aliniuliza askari huyu ambae mdomo wake ulitoa harufu ya sigara aliyokuwa ametoka kuvuta muda si mrefu

“naitwa Reshma!”
“ohoo jina zuri, vipi hapo kifuani nini kinasumbua sumbua mrembo?” afande huyu aliyeonekana mkware (mpenda wanawake sana) aliniuliza akiinuka taratibu na kutazama kulia na kushoto kama kuna mtu anatuona, nikagundua kuwa aliniona wakati nikiyapandisha na kuyaweka weka matiti yangu kifuani vizuri (ya bandia)

“hamna afande nilikuwa najiweka vizuri tu!”
“ahii jamani Reshma ngoja basi nikusaidie eti” aliniambia akicheka cheka huku akinyoosha mikono yake kutaka kunishika kifuani kwenye matiti

“usinishike afande!” nikawa mkali nikimkwepa lakini akazidi kunisogelea
“aaah Reshma kwani hutaki kuishi kama malkia humu ndani ya gereza jamani hautapata shida kabisa ukinikubalia na hakuna atakayejua ni sisi tu!” alinijibu akinivuta mkono tukiwa kwenye korido moja

“sitaki afande sitakiiiii!” nilimjibu kwa sauti ya kike, askari huyu baba mwenye kitambi akanishika mkono kwa nguvu akinivuta sijui alitaka kunipeleka wapi

“njoo huku wewe acha ubishi usio na maana!”

“afande Songa!” mara akaitwa na askari mwenzake akashtuka na kuniachia haraka haraka
“naam afande Jane!” aliitika baada ya kuitwa na yuleyule afande aliyetusimamia sisi
“kuna nini kinachoendelea hapo mbona unamvuta huyo dada?”
“anasumbua sumbua sana huyu dada inaonekana hajazoea mazingira ya gerezani!”
“hapana huyu afande ana…..!”
“shiiiiiiii!” baba huyo alininyamazisha kabla sijajitetea
“wewe unasumbua nini haya harakisha uende ukaungane na wenzako kule ala!” askari huyo wa kike alinikemea na kuendelea na safari yake

“usifikiri ndo umenusurika kwenye mikono yangu, nitakusaka na kukupata tu, mimi ndiye afande Songa, nina miaka ishirini kwenye kazi hii!” mzee huyo aliongea kwa kunitisha huku akininusa nusa kama mbwa, na kunipiga kofi la mgongoni akinisukuma niendelee na safari yangu nikaenda kama mzigo wa kuni mpaka kwenye uwanja wa ndani ya gereza hilo

Hatimae niliingia kwenye uwanja wa ndani kabisa wa gereza hilo nikakutana na wafungwa wengi hasa mahabusu wenzangu wakiwa na sare moja kama yangu, suruali ya rangi ya bluu iliyounganika na shati moja kwa moja, kama ma ‘overoll’ wanayovaaga mafundi magari na mashine mbali mbali za kielektroniki, wanawake wengi walikuwa wakinitazama tazama na kunishangaa shangaa kwa jinsi nilivyokuwa nashangaa shangaa wakinigundua kuwa ni mgeni

“karibu mgeni hapa ndo umefika dada naona huamini amini, ndiyo hapa gereza la wanawake la (…. )” aliongea akilitaja jina la gereza hilo huku akigonga mikono na wenzake wakinicheka

“hebu acheni kumsumbua mwenzenu kwani mnafikiri kapenda kuwa hapa kama ninyi njoo rafiki yangu!” mwanamke mmoja alinishika mkono, alikuwa ni yuleyule niliyemsaidia kuvaa nguo yake wakati akihangaika, tukawa tunaongozana kuelekea upande mwingine wa vyumba vya kulala

“kumbe wewe una muda mrefu humu ndani?” nilimwuliza
“nipo takribani mwaka sasa ila karibia nitatoka maana kesi yangu ina muelekeo siku hizi za karibuni unaitwa nani vile?”

“Sherma, na wewe je?”
“naitwa Anitha!”
“upo hapa kwa sababu gani?”
“mambo ya ndoa yangu tu na migogoro ya kifamilia!”
“pole sana!”
“ndo maisha, na wewe nini kimekuleta humu?”
“kesi za madawa ya kulevya”
“madawa ya kulevya mh?” Anitha alishtuka
“eeh nilisakiziwa kesi baada ya kukataa kuyasafirisha!”
“pole Sherma ndo dunia yetu ilivyo ina…. ” kabla Anitha hajamalizia sentensi yake

“ni muda wa kuoga haraka wote muende kwenye mabafu yenu kuoga ni dakika tano tu!” askari mmoja wa kike alitangaza kwenye kipaza sauti kilichofungwa kwenye mti mmoja uliokuwa umepandwa katikati

“tuwahi Sherma!” Anitha aliniambia akikimbia nami nikimfuata nyuma, kila mfungwa alikuwa amebeba ndoo yake ya maji tukiingia kwenye mabafu ya pamoja ambayo wanaingia watu kumi kumi, mimi nikiwa nimeongozana na Anitha tukishea ndoo yake moja, tukaenda mpaka bafuni,

“ohoo kazi ninayo!” nilijisemea kimoyomoyo baada ya kuona wanawake wakivua nguo zao na kuanza kuoga kwa kujiachia maana mimi sikuwa mwanamke mwenzao nikabaki napata tabu tu huku dudu langu likisimama ndani ya nguo,

Wengine waliinama mbele yangu nikigusana gusana na matako yao, wengine vifuani ndo mashallaah, matiti yalikuwa saa sita, na wengine walipochuchumaa kukojoa ndo nilizidi kuvurugwa nikabaki natazama tazama tu pembeni maana hali yangu ilikuwa mbaya

“mbona huvui nguo zako Sherma hasa mtandio wako huo upo kichwani tu muda wote huoni joto?”
“hamna nitaoga tu usijali wewe anza tu!”
“tuna dakika tano wewe zembea tu, halafu nitazame hapa matakoni kuna nini naona kama kunauma!” Mwanadada Anitha, dada wa kichaga aliniambia akinisogezea matako yake nimtazame akiwa hana nguo hata moja yupo uchi

“ohooo!” nilijisemea kimoyomoyo maana alinipa wakati mgumu kwelikweli…..

Inaendelea……

NILIPOFUNGWA KWENYE GEREZA LA WANAWAKE KIMAKOSA

SEHEMU YA 04

a @King Author
WhatsApp 0629980412
utapata story 3 kwa 2000 tu

“wapi??!! Nilimwuliza Anitha huku nikijikuna kichwani maana mambo yalikuwa mabaya kweli kweli

“si hapa jamani Sherma hupaoni au??” Alinijibu akiukamata mkono wake na kunigusisha kwenye tako lake la kulia huku nikiwa natazama pembeni na kuangalia matako yake kwa machale machale, mambo yote yakiwa wazi

“kuna kipele kidogo!” nilimjibu akiwa uchi hana nguo kama wengine ambao walikuwa wakiendelea kuoga huku mimi peke yangu nikiwa bado nina nguo zangu mwilini sijazivua

“nikune basi Sherma!”
“umesema?”
“nikune haraka!”
“sawa!” nilimjibu, sikuwa na namna nikanyoosha mkono wangu na kuanza kumkuna kipele hicho kidogo kilichomuota kwenye tako lake la kulia, lakini nilipokuwa nikimkuna Anitha aligeuka na kunitazama huku akivibrate vibrate na kushtuka shtuka kama mtu apigwae na shoti ndogo ya umeme ya kimya kimya

“Sherma?” aliniita kana kwamba anataka aniulize kitu
“abee, vipi tayari?”
“bado nikune na kwa juu hapo shoga yangu maana mh!” aliguna huku akinipanulia matako yake zaidi nami nikizidi kuchanganyikiwa, hali ikiwa mbaya ndani ya overoll la kifungwa nililolivaa, dudu langu likiwa limesimama dede linahemea hemea tu juu juu lakini bahati yangu ni kwa sababu tu linguo lenyewe nililobahatika kulipata ni likubwa chini kama bwanga lakini juu ndo likinibana, hivyo haikuwa rahisi mtu kuliona dudu langu lililosimama likilalia pembeni na kunigundua kama mimi ni mwanaume na siyo mwanamke

“vipi tayari?”
“ndiyo tayari uuwiii! Sherma wewe mh?? ” Anitha alijibu huku akinitazama na kutikisa kichwa chake, nami sikutaka kuongeza neno maana nilishajua kuwa wakati namkuna kwenye tako lake alikuwa akihisi msisimko na hisia tofauti na ambayo angeisikia kama angekuwa anakunwa na mtu wa jinsia yake yaani mwanamke mwenzake

“hey leo ni sikukuu kwahiyo mpo huru kufanya usafi wenu na mambo yenu ya kawaida hiyo ni amri kutoka kwa mkuu wa gereza, lakini kesho litakuwa balaa mtafanya kazi double yaani maradufu kwahiyo leo sherehekeeni lakini kesho mjipange sanaaaa???!!” afande Rukia alitutangazia alipokuja bafuni

“ndiyo afandeeeeee!!!” wote walishangilia wakiruka ruka na kuanza kurushiana maji bafuni huku wengine waliokuwa wameshavaa nguo zao wakizivua tena na kuanza kuoga tena ikiwa ni shamra shamra za siku hiyo ya mapumziko na wengine wakipiga ngoma kwa kutumia ndoo za kuogea na makopo, wengine wakiingia kati na kuanza kushindana kukata mauno na kutingisha matako yao wakiwa uchi huku wakimwagiana maji kama sehemu ya shamra shamra, uvumilivu ukanishinda nikajikuta nikitoka mwenyewe ndani ya bafu hilo taratibu maana mambo yalizidi kuwa mabaya kwangu kutokana na urijali nilionao, kwakuwa nilishapajua pa kulala nikaelekea moja kwa moja mpaka kwenye chemba yetu ya kulala iliyokuwa na vitanda viwili vya ghorofa, kila kitanda tulilala wawili wawili, juu wawili chini wawili, kwahiyo ni wanne kila kitanda kizima na jumla nane ndani ya chumba hicho,

Nilipoingia nikashtuka nilipokuta wadada wawili wakiwa wanabusiana busiana na kushikana shikana wakipapasana papasana wenyewe kwa wenyewe ambao inaonekana hawakuenda kuoga wakitumia nafasi hiyo kuburudishana tena hawakuwa na nguo, nilipowakuta nikajua akina dada hao watashtuka lakini wala hawakushtuka wakaendelea na mambo yao ndani ya shuka, nikajikuta nikipiga ishara ya msalaba baada ya kuona kituko hicho ambacho nimezoea sana kuona kwa upande wetu wanaume, mwanaume akiwa na mahusiano ya kimapenzi na mwanaume mwenzake (ushoga) lakini leo ndiyo nimeshuhudia mahusiano baina ya mwanamke na mwanamke mwenzake wakifanya yao kitandani huku mmoja aliyeonekana ni mwanamke halisi akiguna guna na mwingine aliyejifanya kama ndo mwanaume akijitahidi kukoroma kwa sauti nzito lakini uhalisia ulibaki palepale wote ni wanawake tu

“Sherma!” Anitha aliniita na kunitoa kwenye mshangao niliokuwa nikiwashangaa wanawake hao walichokuwa wakikifanya ndani ya shuka ambalo walijifunika nusu kuanzia miguuni mpaka kiunoni tu, kuanzia kiunoni mpaka kichwani wakiwa wazi matiti nje nje

“abee!”
“usiwatazame sana watakukasirikia!” alininong’oneza taratibu
“kwahiyo ni wapenzi hawa au?” nilimwuliza tukinong’ona chini chini wakati wanawake hao wakiwa bize kitandani wakiendelea na shughuli yao
“ndiyo hali ya huku ilivyo, wanaume hakuna kwahiyo watu wanaamua kumalizana kiu zao za mapenzi wenyewe kwa wenyewe wale wenye mioyo midhaifu, ila sisi wenye uvumilivu ndo tunajizuia hivyo hivyo tusije kutumbukia kwenye michezo hiyo!”

“mh?” niliguna tu

“kwahiyo ndo hujaoga Sherma?”
“aah nitaoga baadae Anitha”

Nilimjibu, wakati huo huo kengele ikagongwa kama tupo shuleni
“kengele ya chai hiyo tuwahi!” Anitha aliniambia akiinuka nami nikamfuata tukiwaacha hawa wengine wakiendelea na mapenzi yao kama kawaida

“vipi wale hawanywi chai askari akiwafuata je si tungewashtua na wao?” nilimwuliza wakati tukiwa tumefika kwenye foleni ya chai tayari
“mh Sherma humu askari kwenye muda wa kula hana muda na wewe na wala hakuamrishi, yaani humu ni wewe tu, ila wakati wa kazi ndo thubutu zubae zubae utakula kirungu au mkanda wa mgongo wale kengele wamesikia sana sasa wakikaa njaa kisa nyege zao ni wao wenyewe tu” Anitha aliniambia nikatikisa kichwa tukaingia kwenye foleni hiyo ndefu ya chai mpaka tukapata chai kwa vipande viwili vya mihogo ya kuchemsha tukakaa kwenye meza na kuanza kunywa pamoja na wengine na ndipo tukawaona wale waliokuwa tumewaacha wakisagana chumbani nao wakija kupanga foleni wakiwa wa mwisho mwisho huku yule aliyekuwa chini kama ‘mwanamke halisi’ akiwa amekasirika sana na yule aliyekuwa kama ndo ‘mwanaume wake’ akiwa hana habari tena kwenye foleni yeye ndo kakaa mbele ya ‘mwanamke wake’ wakati ilibidi yeye kama ‘mwanaume’ amtangulize ‘mkewe’

Yule ‘mwanaume’ alipata chai kwa bahati mbaya ‘mwanamke’ akakosa chai maana iliisha na ‘mwanaume’ wake wala hakujali akaenda kukaa na wanawake wengine na kuanza kunywa chai, huyu ‘mwanamke’ wake alipotuona sisi akatufuata

“samahani naomba mnipunguzie chai!” alitunyooshea kikombe

“mssssyuuu wakati mnafanya mambo yenu hamkukumbuka kama kuna chai?” Anitha alimsonya, mimi nikamwangalia na kumuhurumia nikachukua kikombe changu na kuanza kummiminia chai lakini kabla sijafanya hivyo kikombe changu kilipigwa ngumi kikaruka juu juu chai ikimwagika yote, kutazama aliyekipiga alikuwa ni yule ‘mwanaume’ wake aliyekuwa akinitazama kwa hasira……

Inaendelea………

NILIPOFUNGWA KWENYE GEREZA LA WANAWAKE KIMAKOSA

SEHEMU YA 05

na @King Author
WhatsApp 0629980412
utapata story 3 kwa 2000 tu

Kikombe changu cha chai kilipigwa ngumi nzito kikaruka juu juu na kujigeuza geuza huku chai ikimwagika juu kwa juu karibia inimwagikie chai hiyo ya moto na kikombe kikarudi chini sakafuni kikidundadunda kama kitenesi

Nikabaki nikimtazama mwanamke huyo ‘jike dume’ ambae alibaki akiwa amenikazia macho kwa hasira, huku ‘mwanamke’ wake akiwa ametulia tuli akiogopa

“mlikuwa mnafanya nini?” aliuliza
“nilikuwa nampunguzia chai tu mbona unanimwagia chai yangu tatizo liko wapi?”
“unampunguzia chai demu wangu kwa ruhusa ya nani?” mwanaume huyo aliniuliza kwa amri kana kwamba yeye ni mwanaume kumbe ni mwanamke tu kama wengine sema akiwa na vijitabia na hulka za kiume

“sasa mbona unafika mbali kumpunguzia chai kuna tatizo wakati ni jambo la kawaida tu!”
“halafu wewe demu mgeni usiniletee dharau umesikia wewe utapaona jela pagumu!” mwanadada huyo mnene mnene kidogo mwenye kifua na mfupi kiasi alinijibu akinikunja na kunikwida nguo yangu akijua mimi ni mwanamke mwenzake, askari walikuwepo lakini wakitazama tu kinachoendelea bila kufanya lolote, wafungwa wengine wakaanza kushangilia kwa kupiga makofi na kutuchochea tupigane

“niachie tafadhali!” nilimwambia nikiutoa mkono wake,
“Censia muachie mwenzako kwani amekukosea nini?” Anitha rafiki yangu nae alijaribu kunitetea mbele ya mwanamke huyo ambae jina lake halisi kwa nilivyosikia ni Mwajuma lakini wakimbatiza jina la mwigizaji nguli wa kike ‘Cynthia’ na mpiganaji nguli, kutokana na tabia zake za ukorofi na kupenda kupigana pigana

Alimsukuma Anitha ambae kutokana na kukosa pa kujishikiza alainguka mpaka chini mzima mzima jambo ambalo sikulifurahia nikautoa mkono wa mwanadada huyo ‘Cynthia’ na kuutupa kwa nguvu, akakasirika na kurusha ngumi ambayo nilikosea kuiotea ikatua shavuni mwangu ikiniingia kisawa sawa, ingawa ilikuwa ya mtoto wa kike lakini mikono yake ilikuwa imekomaa akionekana ni mfanya mazoezi ya mwili

Censia alirusha ngumi nyingine ambayo alidhani ataniotea tena lakini niliiyona na kuudaka mkono wake kisha nikamrushia ngumi nzito ya uso ambayo niliizuia kwa kumuhurumia ikaishia usoni mwake ikimgusa tu puani, laiti ingemshukia nadhani asingesalimika, nilikumbuka kuwa ni mtoto wa kike tu atabaki kuwa hivyo, sina haja ya kupigana nae

“piga huyo Sherma mpigee!” Anitha alinihamasisha akiwa na kisasi baada ya kuangushwa pale chini

“siyo kila umwonae ndiye ndivyo ilivyo mwingine siye!” nilimwambia mwanadada huyo kwa fumbo ambalo hakulielewa, nikarudisha ngumi yangu ambayo haikumfikia na kumletea madhara yoyote na nikamwachia mkono wake

“kuna nini kinachoendelea hapo eeh!” afande Rukia akajifanya kusogea baada ya kuona pambano limehairishwa kila mfungwa aliyekuja kuona ugomvi huo akarudi kwenye meza yake, pamoja na mimi na Anitha na yule dada mwingine niliyetaka kumpunguzia chai, tukakaa kwenye meza moja huku ‘mwanaume’ wake bado akiwa anaendelea kututazama kwa hasira, hasa mimi, akiwa kwenye meza yake aliyokaa

“samahanini kwa yaliyotokea!” yule dada aliyeniomba chai ambae mtu wake ametuletea fujo alituambia mimi na Anitha

“mssssyuuu!” Anitha akasonya
“usijali chukua muhogo huu!” nilimjibu kwa sauti ya kike kama kawaida yangu nikimpa kipande cha muhogo ambacho alikipokea kwa mashaka huku akimtazama mtu wake yule Censia ambae aliendelea kumtisha tisha

Muda wa chai uliisha sasa ikawa ni kila mtu kwenye usafi, mwenye nguo akafue nguo zake, mwenye kusafisha chumba chake asafishe na kila aina ya usafi, mimi nikatumia muda huo ambao kila mtu alikuwa bize kwenda kuoga bafuni kimya kimya, tena nikaoga haraka haraka kabla sijakutwa kisha nikarejea chumbani nilipomkuta Anitha akifagia fagia huku yule mwanadada mwingine ambae anaitwa Queen akiwa amekaa kitandani kwake akinitazama tu, yule ambae nilimpunguzia chai, mchumba wa Censia

“ulikuwa wapi Sherma!” Anitha aliniuliza
“nilikuwa huko nje natengeneza tengeneza viatu vyangu!”
“nje wapi mbona una maji kichwani?” Anitha alinishtukia
“nimenawa tu kichwa!”
“umenawa au umeoga wewe wakati mwili wa baridi kabisa hebu toa ushungi wako huo!” aliniambia akitaka kunivua
“uache bwana!” nilimjibu nikimzuia

“mwache tu anapendeza sana akivaa hijabu yake!” Queen aliyekuwa kitanda cha pili aliongea
“kelele nawewe maongezi yetu yanakuhusu nini?” Anitha alimjibu kwa hasira huku akinifuta futa maji na wakati huohuo kumbe yule Censia alikuwa mlangoni amesimama akiona kinachoendelea, akamfuata mpenzi wake huyo kitandani

“umeanza kupenda penda mtu mwingine eeh mpaka unamsifia kuwa anapendeza bila hata aibu?”

“hapana nimesema tu hijabu yake imempendeza siyo kama ninampe.. ” kabla Queen hajamaliza sentensi yake hiyo alichapwa kofi la shavuni na Censia

“nyamazaaa mjinga mmoja wewe!” Censia alimkaripia mwanadada huyo akitaka kumtwanga ngumi lakini nikamuwahi na kumdaka mkono wake

“mwache!” nilimwambia,
“achilia mkono wangu!” alinijibu nikwamwachilia akatoka ndani ya chumba hicho kwa hasira, Anitha akawa amesimama kwa pembeni akionekana kuchukizwa na kitendo cha mimi kumtetea tetea Queen

Siku hiyo ya mapumziko iliisha na hatimae usiku uliingia baada ya kula jioni tukapanda vitandani saa tano za usiku kwa amri na askari wakitembea kwenye korido kuhakikisha kila mmoja amelala, mimi nikiwa nimelala na Anitha ambae hakuniongelesha chochote akionekana kukasirishwa na mimi hasa kitendo changu cha kumtetea tetea Queen kutokana na matendo anayotendewa na Censia

“Anitha umelala dia?” nilimwuliza nikimgusa begani akiwa amegeukia upande wa pili
“bwana usinisumbue Sherma!” alinijibu akiutoa mkono wangu nisimguse
“yamekuwa hayo jamani nisikilize basi” nilimjibu nikimshika kiunoni, Anitha akashtuka kidogo na kutulia kwa sekunde kadhaa mkono wangu ulipokuwa kiunoni mwake kisha akageuka na kunitazama, nikatoa mkono wangu lakini akaurudisha tena kiunoni mwake

“nikueleze au nikuonyeshe nini Sherma ujue kama nakupenda naumia unapoanza kumjali mtu mwingine!” Anitha aliniambia

“mh Anitha mimi si…..!” kabla sijazungumza Anitha akinisogezea midomo yake kinywani mwangu na kuanza kuninyonya mate taratibu…….

Inaendelea

Said Abdullah

^ SENIOR C E O & PUBLISHER ^ Software engineering ^ Fan of programming ^ Technology Enthusiast.. ^ System developed|C,C++&java 👇Get more news and updates

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button