Simulizi

SIMULIZI|MAUMIVU YA NDOA SEHEMU YA – 41 HADI 44

ngumu kuweza kuamini kama kweli Abdul alikuwa na uwezo wa kumpa talaka. Irina aliangua kilio utafikiri kama Mtoto mdogo.

Irina alilia kiasi ambacho alisikia kichwa kinamuuma, alijua fika kuwa Abdul atakuwa ametangaza kwa Watu wake kuwa yeye amebeba mimba ya Maganga

“Sikubali kushindwa hii vita hata kidogo, nitapambana mpaka tone langu la mwisho. Kama Abdul anataka kuniacha Mimi basi Mimi na Shaymaa ni bora wote tukose”

Irina aliongea na kuchana ile talaka ambayo ilikuwa imeandikwa na Abdul “Haachiki Mtu hapa” Irina aliongea na kuiona ile barua ambayo Abdul aliiacha kama wosia wake ambao aliandika muda mhache kabla ya kunywa sumu kisha akauchana na kuchoma karatasi zote moto

“Kwa gharama yoyote ile ni lazima Mimi na Shaymaa tumkose Abdul, sitakubali kumuachia Mwanaume hata kidogo na itakuwa fedhea kwa Mimi Mtoto wa mjini

Irina aliongea na baada ya kutafakari kidogo alikumbuka jinsi alivyokuwa kwa Mganga na kujikuta akikosa nguvu.

Aliingiliwa kimwili na Mganga pasipo ridhaa yake la hakuwa na insi kwani aliambiwa hiyo ndio dawa kuu ambayo itamsaidia kumfanya Abdul aduwae na kuwa chini yake

“Najua ni jinsi gani ulivyochukia Mimi kufanya kitendo hiki lakini nikwambie tu, hakuna njia nyingine mbadala ya kukusaidia zaidi ya kufanya hivi”

Mganga aliongea baada ya kumaliza haja zake huku akiwa amesimama, alivuta kaniki iliyokuwa juu ya kamba na kujifunga kiunoni kabla ya kuvuta kaniki nyingine na kumtupia Irina aliyekuwa amekaa katika kitanda kidogo kilichokuwa katika kitanda iccho huku akiwa analia.

Ingia bafuni kuna dawa maalumu nimekuandalia, unapaswa kuoga dawa hiyo na ukitoka hapa akikisha unakutana na Mumeo katika chakula cha usiku pasipo kuoga.

Irina aliinuka kwa shida na kufanya alichokuwa ameambiwa afanye na Mganga lakini alimtazama jicho kali Mganga na kuonesha dhairi alichukizwa kwa kile alichokuwa amefanyiwa.

Baada ya kufanya kila kitu ambacho alipaswa kufanyiwa, ilivunjwa nazi kwenye jiwe maalum na Mganga alifurahi na kumwambia “Kwisha kazi yake. Hapa ueshamuweza na hatoweza kufanya chochote”

“Inamaana yule mpuuzi alinidanganya” Irina aliongea mwenyewe na kuonekana amechukizwa kwa kile kilichokuwa kimejitokeza nyumbani kwa Mganga.

Irina alitoka na kuingia kwenye gari yake na kuelekea alipokuwa anapajua yeye mwenyewe

Katika wodi maalum aliyokuwa amelazwa Abdul, Shaymaa alikuwa amemshika kiganja chake cha mkono na kumuombea kwa Mungu walau ampe tena pumzi kipenzi chake.

Baada ya masaa kadhaa Abdul aliweza kuchezesha macho na Shaymaa alijikuta akitabasam baada ya kumuona Mwanaume ampendae anaweza kupepesa macho na kumpa tumaini kuwa alikuwa ni mzima wa afya.

Abdul aliweza kufumbua macho na alishangaa kumuona Shaymaa yupo pembeni yake akiwa anatabasam. Shaymaa alisogea mpaka kwenye paji la uso wa Abdul na kumbusu.

Alitamani kumuuliza maswali mengi Shaymaa ilikuaje mpaka akawa hapo lakini aliona ni kama yupo kwenye njozi au tayari ameshakufa na yupo katika ulimwengu mwengine na Mungu ameweza kumpa Maisha ya upendo ambayo alipaswa kuishi yeye na Mke wake.

Ilimchukua sekunde kadhaa kutafakari mpaka akagundua kuwa yalikuwa ni mawazo yake na aliweza kutambua kuwa alikuwa yupo hospital.

“Nimefikaje hapa?” Ili ndio lilikuwa ni swali la kwanza la kutoka kwenye kinywa cha Abdul akimuuliza Shaymaa

Irina aliendesha gari yake na kurejea kule kwa Mganga ili akamuulize maswali kadhaa ambayo alitaka kumuuliza baada ya kuona alikuwa amemchezea mchezo na kumpa tiba ya uongo na kumtumia kimwili huku akiwa ametoa pesa zake milioni mbili kama sehemu ya tiba hiyo

“Kama kweli alikuwa ni Mganga, kwanini alishindwa kujua kama Mume wangu amekunywa sumu? Kwanini nimkute Shaymaa na Abdul na sehemu ya tiba yake alisema Shaymaa atakuwa anamchukia Abdul?”

Irina alikuwa anaongea mwenyewe huku akiwa anaendesha gari kuelekea kule kwa Mganga.

Irina alifika na kuegesha gari yake kisha aliteremka na kuingia ndani kwa Mganga huku akionekana dhairi kuwa ni mwenye kisirani.

Irina alifungua mlango na kuingia ndani lakini alistuka na kuonekana kushangazwa kidogo.

“Samahani tukusaidie nini tafadhali?” Kijana mmoja alimuuliza baada ya kumuona Irina akiwa ameshangazwa

“Kuna watu nilikuwa nimewaacha humu, yani namaanisha Mganga na Mdada mmoja ambae alinisindikiza Mimi na yeye nikamuacha akiwa anaendelea na tiba”

Irina aliongea na yule kijna na Mwenzake walionekana kushangazwa tena. “Mganga? Mganga gani ambae unamzungumzia?” Yule kijana alijibu na kumfanya Irina apatwe na ghadhabu zaidi

“Hivi mnajua nyinyi mnanichanganya? Mimi nimetoka hapa masaa kadhaa yaliyopita na nilitoka kutibiwa hapa sasa inakuaje mnaanza kuniuliza maswali ya ajabu?”

Yule kijana ilimbidi amwambie Irina kuwa yeye ni Mganga ambae ndie mwenye ofisi na hapo kuna Mtu na Mpenzi wake ambao walikuja kukodi na kusema kuwa walikuwa na filam ambayo walikuwa wamekusudia kuifanya na walitaka kutumia ofisi kutwa nzima na wao waliwaachia kila kitu na kuondoka zao mpaka pale walipopigiwa simu na kuambiwa wanaweza kuendelea na ratiba yao kwani Boss wao amekuja na kughairisha shooting na watafanya siku nyingine kwa malipo mengine.

Irina alichanganyikiwa na kukosa nguvu baada ya kugundua kuwa alikuwa ametapeliwa “Boss wao mwenyewe walisema ndie huyu kwa maana mimi nilifika hapa na kukuta gari ya huyu Mdada ikitoka”

Yule kijana wa pili aliongea na kumfanya Irina achanganyikiwe zaidi baada ya kugundua kuwa alikuwa ametapeliwa

“Naombeni namba zao” Hiyo ndio kauli ambayo iliweza kutoka katika kinywa cha Irina na alipewa namba zote mbili ambazo walizitumia wale watu kwa nyakati tofauti na walipojaribu kupiga namba zilikuwa hazipatikani.

Irina alikumbuka kuwa alikuwa na namba ya Chausiku ambayo alimpa tena kwa mara ya pili baada ya kumfuata pale kwa kina Jack

Alipiga hiyo namba ya Chausiku lakini kwa bahati mbaya nayo ilikuwa haipatikani na kumfanya Irina apagawe zaidi.

Hakutaka kuongea zaidi, badala yake alitka huku akiwa amechanganyikiwa na kurudi nyumbani kwa kina Jack labda anaweza kupata taharifa sahihi kuhusu Chausiku.

Alifika kwa kina Jack na kwa bahati nzuri aliweza kumkuta yule Mbaba aliyekuwa anafua wakati alivyokuja kumfuata Chausiku

“Samahani kaka Mkeo amenitapeli sijui amekimbilia wapi kama una namba zake tafadhali naomba umpigie”

Irina aliongea huku akiwa amechanganyikiwa na kumfanya yule Baba astuke na kumshangaa “Wewe Dada umechanganyikiwa?” Yule Baba alimuuliza huku akionekana kumshangaa

“Ni kweli nimechanganyikiwa, Mkeo amenitapeli million mbili yeye na Mganga wake feki” “Mimi Mke wangu amekufa huu mwezi wa tatu sasa sijui umekutana na Mke wangu gani aliyekutapeli wewe? Au umetoka kuzimu na amekutapeli huko? Nenda kamtafute kuzimu huku ni Duniani”

Baba alichukia na kuongea kwa hasira hali iliyomfanya Irina ashindwe kuvumilia na kumfuata yule Baba na kumkunja shati huku akipiga kelele akitaka alipwe pesa zake.

Wakati Irina na yule Mzee wakiwa wamekunjana huku wakiwa wamekosa maelewano. Gari maalum za kukodisha kutoka kwenye moja ya kampuni iliyokuwa ikifanya biashara hiyo iliweza kuegeshwa mbele ya nyumba ya kina Jack na alishuka Jack akiwa sambamba na Hakeem na kukuta vulumahi ile.

“Baba Samweli kuna nini?” Jack alisogea na kumuuliza Mpangaji wao ambae alimueleza jinsi ilivyokuwa na kumfanya Jack astuke baada ya kusikia Irina anasema ametapeliwa na Mke wa Baba samweli.

“Hivi Shoga ndio unachanganyikiwa au nini? Mama samweli tokea amekufa nafikiri atakuwa anatimiza miezi mitatu sasa na kumuachia Mumewe Mtoto mdogo. Sasa wewe umekutana na Mkewe yupi?”

Jack aliongea na kumfanya Irina apate ubaridi na kupigwa butwaa baada ya maelezo hayo.

Walimuuliza aseme huyo Mwanamke anaitwa nani na ana muonekano hupi na Irina alielezea na kutaja jina la Chausiku na Jack alishangaa kwani kwao hapakuwa na Mpangaji anaeitwa Chausiku

“Yule Binti alikuja hapa na kuongea na Mimi mambo ya madini na Mimi siamuelewa hata kidogo, kisha akaniuliza kuhusu rafki yake anaekuja na gari kama ulikuwa umekuja na nikamjibu sijui. Baadae nilimuona amekaa hapo anachat na ulipokuja wewe nikaona mnaongea mambo yenu na mimi sikuwafuatilia zaidi ya kuendelea kufua”

Baba Samweli alielezea na Watu waliojaa pale aligundua kuwa Irina ametapeliwa huku kila mmoja akiwa anasema lake

Chausiku kama alivyoweza kujitambulisha, alikuwa ni tapeli mkubwa aliyekuwa anashirikiana na rafiki yake anaitwa Emmanuel kabija ambae aliigiza kama Mganga. Waliweza kumfuatilia Irina na kugundua mambo yake bila mwenyewe kujua na wakatumia fursa hiyo kuweza kumtapeli na kumfanyia udhalilishaji
*

“Abdul najua nini ulichokuwa umekikosa Mpenzi wangu. Wala hupaswi kukata tamaa!! Najua sasa utakuwa umejifunza na utaniheshimu kama Mke wako tafadhali naomba usijaribu kunywa sumu tena kwani Shaymaa wako nipo tayari kurudiana na wewe”

Shaymaa aliongea na Abdul alisisimkwa na nywele na kujikuta akipata nguvu nakuinuka na kujikuta akimkumbatia Shaymaa

MWABEJA SANA ………… USIKOSE EPISODE IJAYO

MAUMIVU YA NDOA
S2: EP 42
MTUNZI: Abdulkarim Dee

Kuna wakati unaweza kujikuta ulitaka kuchukua maamuzi fulani lakini unajikuta ukijilaumu wewe mwenyewe kwa maamuzi ambayo ulitaka kuyachukua, kwani unaona dhairi yalikuwa yanaenda kukukosesha jambo fulani

Ilikuwa ni siku ya pili kufurahi ukiondoa siku ile ambayo alifunga ndoa na Shaymaa. Inawezekana siku aliyofunga nda na Irina alifurahi pia lakini asikwambie Mtu, hakuna siku ambayo Abdul alifurahi zaidi kama siku ambayo alifunga pingu za maisha na Shaymaa.

Unajua kwanini Abdul alifurahi zaidi siku hiyo? Kwanza ndio ilikuwa kwa mara ya kwanza Abdul anaingia katika ndoa, lakini ilikuwa ni jambo la furaha kwake kufunga ndoa na Mwanamke ambae alitokea kumpenda kutoka moyoni.

Siku ya pili kwa Abdul kufurahi ilikuwa ni siku hiyo ambayo Shaymaa aliamua kumfungulia moyo kwa mara ya pili na kukubali kurejea katika ndoa yake

“Lakini nakumbuka kuwa uliniambia umeshachumbiwa na Mwanaume mwengine” Abdul alimuuliza Shaymaa ambae alipokea swali lake kwa tabasam la hali ya juu

“Mimi ni wako Abdul, niliaha Dunia ikuadae kwanza na ukishatambua thamani yangu basi nilipanga nilijee tena kwako” Shaymaa aliongea kwa upole huku Abdul akiwa anamtazama kwa unagalifu na kujikuta mwenye furaha zaidi

“Sasa kwanini ulinidanganya hivyo lakini?” “Nilikudanganya ili nikupime kama bado una upendo na mimi au lah”
Kwenye upendo wa kweli kila jambo linaenda sawa, Abdul wala hakujihisi kama Mtu ambae ametoka kunywa sumu.

Muda wote alikuwa anapata faraja kutoka kwa Shaymaa na kumsaidia kwa kila jambo “Shaymaa wewe ni Mwanamke wa mfano sana kwangu, sitakubali hata kidogo nikuache uumie tena” Abdul aliongea na Shaymaa alifurahi kusikia hivyo na kumtaka apumzike
*
Baada ya kugundua kuwa ametapeliwa, Irina alikuwa amechanganyikiwa sana na hakujua nini afanye kwa wakati huo zaidi ya kuangua kilio.

“Jack naomba msaada wako kama hautojali, Abdul akipona ataniacha Mimi” Irina aliongea na Jack hakutaka hata kidogo kushirikiana na Irina huku akimtaka kuwa busy na ndoa yake na yeye yupo busy na Mpenzi wake ambae alikuwa ni mgonjwa akimuuguza.

“Inamaana Jack anaenda kuolewa na Hakeem alafu Mimi nakaa bila ya kuwa na Mwanaume?”

Irina aliongea mwenyewe akiwa anaendesha gari yake na hasijue nini afanye kwa wakati huo.

Wakati anaendesha gari yake kurejea nyumbani kwake alijikuta akipata wazo na kumfanya atabasam kwani aliona ameshaweza kupata njia sahihi ya kutatua tatizo lake. {Je ni wazo gani hio ambalo alikuwa amelipata Irina?”

Endelea kufuatilia simulizi hii tamu na ya kusisimua yenye mafunzo ndani yake.

Irina aligeuza gari na kuelekea sehemu nyingine tofauti na ile aliyokuwa anaenda mwanzo na safari hii ilionekana ameshakubali kila kitu ambacho kitaenda kutokea “Ni kweli Mimi nina ujauzito wa Maganga wala sihitaji kuficha jambo hilo”
Irina aliongea mwenyewe na kucheka peke yake utafikiri Mtu aliyekuwa amechanganyikiwa.

Katika nyumba ile ya Mganga wa kienyeji aliyokuwa ametapiliwa na kuwakuta Waganga wengine ndipo alipokuwa amerudi.

Alifika na kuegesha gari yake vyema kabla ya kuvuta pumzi na kuziachia mfululizo, kisha akaongea tena mwenyewe kama ilivyo kawaida yake “Ni bora tukose wote kuliko kukubali kuwa mjinga hatua za mwishoni”

Irina aliongea na kuteremka katika gari yake na kuingia ndani kwa Mganga huku akiwa anajiamini

“Bado hauamini kama sisi sio hao uliokuwa umekubaliana nao?” Yule kijana wa pale awali almpokea kwa swali huku akimtazama kwa ufasaha

“Naitwa Irina, safari hii nimekuja kama Mteja ambae nimekuja kupata tiba tena, tuachane na wale wapuuzi kwani tiba yangu ni bora kuliko jambo lolote lile”

Irina aliongea na kumfanya yule kijana atabasam kiasi na kumkaribisha katika chumba maalum ambacho angeweza kusikilizwa shida yake
*
Mzee Mustapha aliweza kutuma vijana wake kila kona wamtafute Shaymaa ili wajue kuna nini kilichokuwa kimemkuta Binti yake kipenzi

Mwanzoni alichukulia kawaida akihisi labda Shaymaa anamfanyia mzaha au hataki kwenda kuwa Mmoja wa Wakurugenzi wa kampuni ya Baba yake

Lakini kadri muda ulivyokuwa ukisonga mbele ndivyo hofu na Mashaka dhidi ya Binti yake yalivyokuwa yanazidi kupanda “Inamaana Watu wa Madame bado wanafanya upuuzi wao hata kama Boss wao ameshikiriwa na polisi? Au wanafanya hivyo ili kushinikiza Mimi nimtoe Madame?”

Mzee Mustapha alikuwa akitafakari mwenyewe lakini kabla hajatafakari zaidi, alitaharuki kumuona Shaymaa akirejea nyumbani baada ya kushinda kutwa nzima akiwa na Abdul akimuuguza kule hospital

Hakuwahi kumuona Baba yake akiwa na hasira kiasi hicho kama hivyo ambavyo alimkuta siku hiyo.

“Umeniangusha sana Mwanangu” Mzee Mustapha alimsema sana Shaymaa kwa kitendo chake cha kutooudhulia Tafrija aliyokuwa amemuandalia pasipo kumwambia chochote.

“Nilipigiwa simu kuwa Abdul amekunywa sumu na nilishindwa kukupa taharifa kwani nilipatwa na mstuko sana. Samahani sana Baba ni kweli nimekuangusha” Shaymaa aliongea na Mzee Mustapha alistuka baada

Shaymaa aliongea na Mzee Mustapha alistuka baada ya kusikia taharifa hiyo na kujikuta akimuonea huruma Abdul huku akitaka kujua hali ya Abdul.

Shaymaa alimtoa hofu na kumwambia kuwa alikuwa anaendelea vyema, kisha Shaymaa alitumia fursa hiyo kumuomba Baba yake aruhusu arudi kwenye ndoa yake

“Hapana siwezi kukubali hata kidogo” Mzee Mustapha aliongea na Shaymaa alistuka na kumpigia magoti Baba yake akubali ombi lake

Mganga alimpa fursa Irina kuongea shida yake iliyokuwa imempeleka hapo

“Kuna Mtu nagombea nae Mume nilikuwa nataka kumkomesha Mwanamke mwenzangu sote tukose. Nataka nimuue huyu Mwanaume au nimtie uchizi na sote tukose”

Irina aliongea huku akiwa anatetemeka ……………… NINI KITAENDELEA? USIKOSE EPISODE IJAYO

MAUMIVU YA NDOA
S2: EP 43
MTUNZI: Abdulkarim Dee

Kuna tofauti kubwa sana kati ya Mnyama na Binaadamu. Mara nyingi Mnyama huwa hafikiri kabla ya kutenda na hajali hata baada ya kutenda ndio maana Binaadamu yoyote ambae ufanya matendo yanayoshabiiana na Mnyama, Watu umuita Mnyama.

Irina alikuwa amedhamilia kufanya ubaya dhidi ya Shaymaa au kwa Abdul ili tu yeye na Shaymaa wote kwa pamoja wakose ndoa. Na hakuwa tayari kumuona Shaymaa anarudiana na Abdul huku yeye akipewa talaka

“Unaweza kuuwa kweli wewe?” Mganga alimuuliza Irina huku akiwa anamtazama kwa umakini.

Ilikuwa ngumu kwa Irina kujibu ndio kwani alikuwa akisukumwa zaidi na moyo wa tamaa kuliko akili yake binafsi katika kuamua hilo “Ndio naweza kuuwa” Irina alijibu na kumfanya Mganga aangue kicheko kabla ya kunyamaza na kumtazama kwa jicho fulani kali ambalo liliambatana na sonyo kali.

“Sikiliza wewe Mwanadamu, usifikiri kuuwa Binaadamu mwenzako ni sawa na kumchinja Kuku sawa?” Mganga aliongea kwa lafudhi tofauti na aliyokuwa akiongea hapo kabla na alionesha alikuwa amepandisha majini yaliyokuwa yakiongea kupitia yeye

Ilikuwa ni kwa mara ya kwanza Irina anaenda kwa Mganga hivyo hakuwa mzoefu na mambo hayo, na hali hiyo ya Mganga kupandisha Majini ilimuogopesha sana na kumfanya atetemeke muda wote aliokuwa akiulizwa maswali na Mganga

“Sikia wewe mwanadamu, Mimi naweza saidia wewe kuaribu mwenzako ila siyo kuuwa, mana wewe huna moyo huo” Yule jinni alimwambia na Msaidizi wa yule Mganga alimsaidia kumtafsiria kwa kumwambia kuwa “Jini anasema anaweza kukusaidia kumtia uchizi huyo Mwanamke mwenzio ila kwa swala la kuuwa kwa wewe huna moyo huo hivyo unaweza kufa wewe”

Msaidizi wa Mganga aliongea na Irina alifurahi kusikia Shaymaa anaweza kupewa uchizi na hii aliona itakuwa njia bora ya yeye kummilikia Abdul wake “Bora tu hawe kichaa, mana sina jinsi” Irina aliongea mwenyewe huku akiwa anatabasam

“Hii ni dawa ambayo unapaswa kuoga kwa siku 21 na baada ya hapo ndio zoezi la kumtia uchizi mwenzako litafuatia”

Mganga aliongea na Irina alipokea kwa moyo mmoja na kutamani kuuliza kitu lakini alionekana kuogopa kiasi fulani. Mganga alimtazama na kuweza kugundua kitu kupitia yeye “Unaonekana una jambo unataka kuongea” Mganga aliongea na Irina aliitikia kwa kichwa kuashiria kweli alikuwa anataka kuuliza kitu. “Wala usijali wewe kuwa huru tu” Mganga aliongea na safari hii alionekana kuongea kwa lafudhi yake na kuashiria kuwa hakuwa na jinni kichwani mwake

“Heeh!! Nilitaka kuuliza kuhusu Mume wangu? Alishanipa talaka na niakaichana je nawezaje kumfanya asiwe na kauli kwangu” Irina aliongea huku akiwa amepoteza uwezo wa kujiamini kiasi.

“Tunapaswa kufanya jambo moja kisha tutamaliza jambo lingine” Mganga aliongea kisha akachukua kibuyu kimoja kati ya vibuyu vyake vilivyokuwa vimemzunguka na kumimina dawa fulani iliyokuwa humo na kuifunga kama ilizi na kumtaka akafukie mlango wa mbele wa nyumbani kwake na anuie kile ambacho alichokuwa anakitaka kutoka kwa Mume wake “Akikisha unafukia sehemu ambayo Mumeo anaweza kuitambuka”

Mganga aliongea na Irina alipokea na kulipa pesa ambayo aliambiwa anapaswa kulipa na kuondoka zake huku akiwa na matumaini ya kutatua matatizo yake

Shaymaa alimtoa hofu na kumwambia kuwa alikuwa anaendelea vyema, kisha Shaymaa alitumia fursa hiyo kumuomba Baba yake aruhusu arudi kwenye ndoa yake

“Hapana siwezi kukubali hata kidogo” Mzee Mustapha aliongea na Shaymaa alistuka na kumpigia magoti Baba yake akubali ombi lake

“Tafadhali Baba nilikuwa naomba ulidhie ombi langu, Abdul ni Mwanaume sahihi kwangu na tayari ameshatambua makosa yake”

Shaymaa aliongea na kushangaa baada ya kumuona Baba yake akiachia tabasam mwanana

“Natambua kama Abdul ni Mwanaume wa ndoto zako, wala siwezi kufanya hivyo Binti yangu. Hilo ni jambo la kheri kwako lazima nikupe fursa yako muhimu katika maisha yako”

Mzee Mustapha aliongea na kumfanya Shaymaa akumbatie Baba yake kwa nguvu huku akifurahi

Ilikuwa ni furaha isiyo kifani baada ya kuona Baba yake ameridhia ombi lake la kurudi kwa Abdul

Irina aliweza kurejea nyumbani kwake na jambo la furaha kwake ilikuwa Abdul bado hajatoka hospital hivyo aliona hiyo ndio nafasi ya kuweza kufanya ushirikina wake kama ambavyo alivyokuwa amepewa maelekezo na Mganga wake ili Abdul akipewa ruksa kutoka hospital basi akute kila kitu kimeenda sawa

“Naomba unifuate nahitaji nikuagize” Irina alimwambia oliver na bila kupinga Oliver alimfuata Irina mpaka sebuleni na kusikiliza kitu ambacho alikuwa ameagizwa na Boss wake

Alimtuma mbali makusudi na lengo lake lilikuwa ni kufanya ushirikina ambao alikuwa ameambiwa afanye ili kumtuliza Abdul. Alifanya hivyo kusudi ili Oliver hasijue nini ambacho anataka kukifanya

Baada ya Oliver kutoka na kwenda alipoagizwa na Boss wake, Irina aliweza kuitumia fursa hiyo na kuchimba mbele ya mlango na kufukia dawa aliyokuwa amepewa na kunuia yale yote aliyokuwa anayataka kutoka kwa Abdul. Baada ya kufanya kila kitu, alifukia na kupaweka vyema na kutabasam kwani aliona kila kitu chake kimeenda kama vile alivyokuwa anataka
*
Kwa mara ya kwanza kesi ya Madame na Watu wake iliweza kusikilizwa katika mahakama kuu kama ambavyo ilikuwa imepangiwa baaada ya Madame kukata rufaa katika mahakama ya mwanzo

Ilikuwa ni kesi iliyoweza kuwavutia Watu wengi, huku Shaymaa, Hakeem, Mzee Mustapha na wengineo walikuwa ni sehemu ya Watu walikuwa wameudhuria mahakamani kusikiliza kesi hiyo iliyokuwa inamkabili Madame na Watu wake.

Feisal aliweza kusimama ipasavyo kumtetea Mama yake na kweli Madame aliweza kukanusha mashtaka yote yaliyokuwa yanamkabili, huku mwanasheria wake ambae ni Feisal akiithibitishia Mahakama kuwa hapakuwa na ushahidi uliojitosheleza kumtia hatiani Mteja wake na washirika wake

Ilikuwa tofauti na Watu wengi walivyokuwa wanafikiri, kila Mmoja alikuwa akifikiri kuwa itakuwa kesi ngumu kwa Mdame na Watu wake lakini mbele ya usimamizi wa Feisal ilikuwa ni kesi nyepesi sana kwa upande wa Madame na kuubana ipasavyo upande wa jamuhuri na kuoenaka kama hakukuwa na ushaidi uliokuwa unajitosheleza kwani hata sauti ambayo ilikuwa imerekodiwa, Madame aliikana si yake huku akisema kuwa Watu walikuwa wametengeneza ili kumchafua.

Kesi ilihairishwa na kupangiwa tarehe mpya na Madame aliweza kurejeshwa rumande lakini safari hii alikuwa ni Mtu mwenye tabasamu tele tofauti hata na vile alivyoletwa mahakamani

“Ni ngumu sana Nyoka kuzaa Mjusi japo mara kadhaa inaweza kutokea”

Madame aliongea mwenyewe moyoni akiwa anapanda kalandinga, tayari kurudi lumande kwenda kusubiri tarehe mpya ya kurudi mahakamani aliyokuwa amepangiwa
*
Baada ya matibabu ya siku kadhaa, Abdul aliweza kupewa ruksa na kurejea nyumbani kwake.

Amina ndie alikuwa Mtu aliyekuja kumchukua na kumrejesha nyumbani “Wakati mwengine unapaswa kukubaliana na baadhi ya mambo ili kujiweka sawa kisaikoloji na kukwepa baadhi ya maamuzi ambayo unayachukua na yanayoweza kukughalimu” Amina alimwambia Abdul aliyekuwa siti ya pembeni huku Amina akiwa anaendesha gari kurejea nyumbani kwa Abdul

Abdul alicheka kiasi na kumshukuru Amina kwa kipindi chote alichokuwa anajitoa kwake.

“Najua nini unamaanisha Amina, lakini kwasasa Mimi natambua kuwa siwezi kuikwepa fedhea ya Irina kwa kutembea na Maganga mpaka kushika ujauzito wake. Ila jambo kubwa ambalo nafurahi ni Shaymaa kukubali nimrejee”

Ilikuwa ni taharifa mpya kwa Amina, kusikia Shaymaa na Abdul walikuwa wamekubaliana kurudiana. Lilikuwa ni jambo ambalo alikuwa analiomba siku zote

“Sasa kama unarudiana na Shaymaa, vipi kuhusu Irina itakuaje?” Amina alimuuliza Abdul huku akiwa mwenye furaha

“Nilishafanya maamuzi ya kumpa talaka hata kabla sijanywa sumu” Abdul aliongea na kumfuraisha zaidi Amina, akiona maombi yake yalikuwa yamepokelewa

Walifika nyumbani kwa Abdul na walishuka na kuingia ndani lakini kwa bahati mbaya, Abdul aliweza kuvuka ile dawa aliyokuwa ametegewa na Irina na kujikuta akisisimka mwili mzima kama Mtu aliyekuwa amepigwa shot ya umeme na kujikuta akipiga kelele na kuganda na kubaki ameduwaa huku macho yakiwa yamemtoka akimtazama Amina na kuhema mfululizo
*
“Hatuwezi kumtegemea Feisal tu ni lazima tufanye jambo ili kuweza kujinasua kwenye hii kesi” Madame alimwambia Hakeem aliyekuwa ameenda kumtembelea Mama yake

“Kosa kubwa ambalo ulikuwa ukilifanya, ni kutonishirikisha katika Mambo yako, wewe unafikiri nawezaje kumaliza hii kesi wakati hata sijui wapi kwa kuanzia?” Hakeem alimuuliza mama yake huku akiwa makini hasisikike

Madame aligeuza shingo kuangaza ulinzi na alipojiridhisha kuwa hakuna Mtu aliyekuwa anawafuatilia aliweza kutoa kikaratasi kilichokuwa na ujumbe uliosomeka “Chini ya kabati langu kuna sabuni ya kufua nguo. Hiyo ndio unaweza kutumia kufua nguo hii”

Madame aliongea na Hakeem aliweza kumuelewa Mama yake. Haraka aliondoka na kuelekea nyumbani kwa Mzee Mustapha kwenda kutazama sabuni ya kufulia nguo aliyokuwa ameongelea Mama yake

“Abdul hupo sawa kweli?” Amina alimsogelea Abdul na kumuuliza lakini cha ajabu Abdul alimsukuma Amina kwa nguvu na kuanguka chini na wakati huo Irina alitoka ndani na kushuudia tukio hilo.

Abdul baada ya kumuona Irina alianguka chini na kupiga goti na kumuomba msamaha Irina “Samahani sana Mke wangu najua Mimi ni Mkosefu kwako”

Abdul aliongea na kumstua Amina ambae hakutegemea kama Abdul angefanya tukio lile huku Irina akimtazama Amina kwa dharau akiona jambo lake limefanikiwa.

“Kweli yule ni Mganga, huyu Mpeezi nimemuweza bado yule nguruwe wake” Irina aliongea Mwenyewe moyoni huku akiwatazama kwa zamu

NINI KITAENDELEA? USIKOSE EPISODE YA 44

MAUMIVU YA NDOA
S2: EP 44
MTUNZI: Abdulkarim Dee
FINAL EPISODE

ILIPOISHIA………

Abdul baada ya kurudi nyumbani aliweza kutambuka eneo ambalo lilikuwa limefukiwa dawa na kujikuta akipatwa na mstuko kama Mtu aliyekuwa amepigwa shot ya umeme.

Amina alimsogelea Boss wake na kumuuliza kama yupo sawa? Lakini Abdul alimsukuma kwa nguvu Amina kiasi ambacho alianguka kama mzigo

Irina alisikia yowe la maumivu ambalo alilipiga Mumewe na kutoka je kuja kutazama nini kilikuwa kimetokea. Katika hali ya kushangaza, Abdul alipiga goti na kumuomb msamaha Irina kitu kilichomshangaza mpaka Amina……………
ENDELEA …………………

“Kweli yule ni Mganga, huyu Mpeezi nimemuweza bado yule nguruwe wake” Irina aliongea Mwenyewe moyoni huku akiwatazama kwa zamu

“Kama kweli unaomba msamaha kutoka moyoni naomba umtimue huyu mpuuzi wako?’ Irina aliongea huku akimuoneshea Mkono Amina

“Mke wangu amesema hakutaki tafadhali naomba uondoke” AAbdul aliongea kwa hasira huku Irina akiwa anatabasam baada ya kuona Amina anatimuliwa kama kibaka.

“Umashangaa nini utafikiri umefumaniwa ugoni? Kuanzia leo sitaki kukuona unakaa karibu na Mume wangu”
Irina aliongea na kumsogelea Amina aliyekuwa ametulia tuli akimtazama kwa hasira. Irina alisogea na kumshika mkono Amina ili amtimue lakini alistukizwa na kibao kimoja ha haja kutoka kwa Binti huyu “Mchawi mkubwa wewe” Amina alimwambia Amina baada ya kumchapa kibao

“Baby unamuona huyu mpuuzi?” Irina alimwambia Abdul huku akiwa ameshika shavu lake kuashiria alikuwa anaumia

“Hivi kati ya Amina na wewe unadhani ni nani anaefaa kuitwa mpuuzi?” Abdul aliongea kwa msisitizo na kumshangaza Irina “Abdul!! Umechanganyikiwa?”

Irina alijikuta akiuliza huku akiwa na hofu kiasi na hakuweza kugundua kulikuwa na nini kinaendelea baina ya Mumewe na Amina “Wala sijachanganyikiwa, nina akili zangu timamu. Nataka uniambie hivi ni nani aliyekushauri uende ukaniloge? Unafikiri Mimi unaweza kuniloga kirahisi namna hiyo?”

Abdul aliongea na safari hii alikuwa akiongea huku anamsogelea Mkewe aliyekuwa anatetemeka na kupoteza uwezo wa kujiamini “Aaaah Abdul Mu mee wangu mbona sikueee……”

Kabla hajamaliza kauli yake alizibuliwa kibao kingine na Abdul kilihomfanya apepesuke na kuona nyota kabla hajakaa sawa na kuangua kilio kama Mtoto Mdogo.

Abdul alimsogelea na Kumziba Mdomo ili asipige kelele “Upaswi kulia Irina, unapaswa kusherekea yale yote uliyokuwa ukinifanyia, yani unisaliti kwa kutembea na Mlinzi wangu, unisingizie mimba nab ado unataka kuniloga?” Abdul aliongea kwa hasira huku akiwa amemziba mdomo

“Kama unitaki ni bora uniache tu kuliko unisingizie mambo ya kipuuzi” Irina aliongea baada ya kupewa nafasi na Abdul

“Ooh Nimekusingizia au siyo? Basi sawa” Abdul aliongea na kumuita Oliver aliyekuwa katika chumba chake maalum akitimiza majukumu yake ya ulinzi. Oliver aliitika na kusogea pale huku wakitazamana na Irina, huku Irina akiwa anamtazama kwa jicho kali

SIKU KADHAA ZILIZOPITA

Baada ya Irina kutoka kwa Mganga, alirudi nyumbani ili kutekeleza majukumu yaliyobaki kama ambavyo aliyokuwa ameelekezwa na Mganga. Alifika na kumkuta Oliver, alijua fika kama Oliver akiona alichokuwa anataka kufanya anaweza kuvujisha siri zake.

Irina alimtuma Oliver mbali ili apate nafasi ya kufanya mambo yake ya kishirikina bila hata ya Oliver kuona.

Oliver nae alijiuliza maswali kadhaa baada ya kutumwa na Irina kwani walikuwa wanakata siku nyingi pasipo kuongea chochote. “Itakuwa kuna Mwanaume anataka kumuingiza”

Oliver aliongea mwenyewe na aliona busra kama atajificha ilia pate kushuudia kila kitu. Alizunguka kwenye fens ya nyumba ya Abdul na kujibanza seheme akihungulia pasipo hata Irina kumuona.

Alifanikiwa kumuona Boss wake akitoka ndani na kufanya ushirikina wake na hapo aliweza kugundua maana ya Irina kumtuma mbali ili kufanya alichokuwa anataka kukifanya. Oliver alijua kivyovyote Irina atakuwa amemloga Abdul hivyo hakutaka kulifumbia macho swala hilo na alimpigia Amina na kumueleza kila kitu.

Usiku wa siku hiyo Amina alikuja nyumbani kwa Abdul, na kwa kushirikiana na Oliver waliweza kufukua pale alipokuwa amefukia Irizi na walifanikiwa kuitoa.

Baada ya pale Amina alipoenda kumtembelea Abdul hospital, hakutaka kumficha kitu. Alimueleza kila kitu Abdul na hapo waliamua kumchezea mchezo Irina ili watambue ile Irizi Irina alikuwa amefukia ili kumtega nani?
*
Abdul alimaliza kmsimulia kila kitu Irina na kumwambia ana ushahidi wote kwa yale yote aliyokuwa ameyafanya “Kwa kushirikiana na Watu wangu, Maganga yupo katika mikono salama na nimemkamata ili nipate uthibitisho wa vipimo. Kama unasema Mtoto ni wangu basi nitasubiri utakapojifungua ili tupime D.N.A na ikigundulika Mtoto ni wangu basi nitakulipa fidia utakayotaka, lakini ikigundulika Mtoto ni wa Maganga basi utanilipa fidia nitakayokudai”

Abdul alingea na Irina hakuwa na ujasir wa kuendelea kusimama na badala yake alianguka na kupiga magoti huku akilia kilio cha Maumivu “samahani sana Abdul, nikweli nimekukosea sana Mimi” Irina aliangua kilio na kuongea ukweli wake kuwa Mimba ilikuwa ni yay aganga.

Hakufiha kitu na alimwambia ukweli kuwa talaka aliyokuwa amemuandikia alikuwa ameichana hivyo alikuwa anaomba msamaha waishi pamoja na ikiwezekana Shaymaa aolewe Mke wa pili.

Ilikuwa ni ngumu kwa Abdul kukubali ombi lake kwani hakuweza kurudi nyuma na alihoweza kufanya ni kumpa talaka tatu ili arejee nyumbani kwao akajifunze ni jinsi gani anaweza kuitunza ndoa yake endapo atabahatika kupata nafasi ya kuolewa tena.

Hakeem aliweza kufika nyumbani kwa Mzee Mustapha na Mzee aliweza kumpokea vyema Mwanae huku akimtaka hawe mwema tofauti na alivykuwa anataka kufuata upande wa Mama yake

“Wewe ni Mtoto wangu tu, na nimekuandika kama mmoja wa warithi wangu pindi itakapotokea nimefikwa na umauti”

Mzee Mustapha alimwambia Hakeem ambae aliinamisha kihwa chini na kumuomba Msamaha Baba yake, pia alitumia fursa hiyo kumuombea msamaha Mama yake kwa yote aliyokuwa amemtendea Mzee Mustapha.

Hakeem hakurudi nyumbani kwa wema kama ambavyo Mzee Mustapha alivyokuwa akifikiri. Lengo lake lilikuwa ni kupata sabuni ya kufulia nguo kama ambavyo Mama yake alivyokuwa amemuagiza.

Alifanikiwa kuhongesha funguo ya chumba cha Mzee Mustapha na baada ya kupata funguo, aliweza kuvizia Mzee Mustapha hayupo, aliweza kuingia chumbani na kufanikiwa kuiba begi la pesa ambalo Mama yake alikuwa amelifiha kwa niaba ya kufungua nguo {Kutoa rushwa ili Mama yake atoke}
*
Kesi ya Madame ilikuwa ikiendelea huku Feisal akijatahidi kupangua shitaka moja baada ya linguine na Madame aliweza kufutiwa baadhi ya makosa na kuonekana alikuwa na nafasi kubwa sana ya kuweza kushinda.

“Habari yako Msaliti” Shaymaa alishindwa kukaa kimya na siku hiyo alikuwa amefunga safari kuelekea ofisini kwa Feisal kwenda kumkabiri Kaka yake

“Shaymaa unanitusi?” Feisal alimuuliza Dada yake huku akiwa ameshangazwa na jinsi alivyomuita.

Shaymaa alitumia nafasi hiyo kumkumbusha Feisal maovu yote aliyokuwa ameyafanya Madame na kumtaka angalau avae viatu vya ndugu wa Watu wote waliouliwa na Madame

“Msihana mdogo kama Liyuna aliweza kuuwawa na Madame tena akiwa na Mtoto tumboni, Madame hakujali hilo na alichoweza kujali ni maslahi yake”

Shaymaa aliongea mengi kiasi machozi yalikuwa yakimtoka na Feisal alikaa kimya kumsikiliza “Mungu angempa anagalau pumzi Mjomba ili arejee tena Duniani walau kwa sekunde kadhaa basi kitu kimoja angeweza kukifanya ni kukuhapa kibao Mtoto wake ili uzinduke”

Baada ya kuongea maneno mengi yaliyokuwa yakimchoma Feisal, Shaymaa alimwambia kuwa kama anaona Mama yake ana thamani kubwa hapa Duniani kuliko Watu wanaopoteza maisha bila hatia, basi achague moja Mama yake au yeye.

Shaymaa aliongea na kutaka kuondoka lakini Feisal alimuita na Shaymaa alisimama kumsikiliza “Smahani sana Shaymaa kwa kunielewa vibaya, ila sikuwahi kutamani kumsaidia Madame hata siku moja. Nilikuwa natafuta ni jinsi gani naweza kulipa kisasi change kwake. Tokea siku ya kwanza nilimuhoji maswali na nilimrecord ili kupata ushahidi. Lengo langu ni kumuangusha wakati ambao hata yeye hawezi kutegemea. Mimi simtetei ila nataka nimuoneshe kuwa nilikuwa na uwezo wa kumtetea lakini nitamfanya akatumikie kifungo ili ajutie dhambi zake”

Feisal aliongea na Shaymaa alishindwa kuvumilia na kujikuta akimkimbilia Feisal na kumkumbatia kwa nguvu huku akimuomba radhi kwa maneno aliyokuwa akimwambia.

Hakeem akishirikiana na Mpenzi wake Jack waliweza kuwasiliana na Hakimu aliyekuwa anaendesha kesi ya Madame na Watu wake na waliongea nae ili wampe rushwa na ampendelee Madame kiwezekana apindishe sheria na Madame aweze kushinda kesi.

Bila kujua Hakimu aliweza kuwawekea mtego na walifanikiwa kunaswa na taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa wakitaka kutoa rushwa.

Akiwa mwenye furaha akijua siku ya ushindi imefika, Madame aliweza kupanda mahakamani katika siku yake ya mwisho ya kutolewa hukumu.

Katika hali ya kushangaza, Feisal aliweza kutoa ushahidi ulioweza kumtia hatiani Madame na Madame alihukumiwa kifungo cha maisha jela.

Ilikuwa ni kama alikuwa kwenye njozi, hakuweza kuamini kama Feisal angeweza kumgeuka lakini ndio hivyo Mtoto wake wa kumzaa alitumia fursa hiyo kuweza kumuhumu Mama yake.

Hakeem na Jack nao walipatikana na hatia na kila Mmoja alihukumiwa kwenda kutumikia kifungo cha miaka 10 jela

Baada ya Madame kuhukumiwa jela, Shaymaa na Abdul waliamua kurudiana kwa kuandaa sherehe kubwa utafikiri walikuwa wanafunga ndoa upya.

Irina hakukubali hata kidogo kumuona Shaymaa na Abdul wanarudiana na kuishi pamoja. Aliamua kwenda kwa Mganga ili kuvunja ndoa hiyo.

Alipewa masharti makubwa na magumu ili kuvunja ndoa hiyo, alipaswa kwenda kuvunja nazi katikati ya jiji huku akiwa uchi wa Mnyama.

Halikuwa jambo gumu kwake kwani nia yake ilikuwa ni kuona Shaymaa na Abdul hawaishi pamoja. Irina aliingia kwenye gari mpaka katikati ya jiji akiwa na Mtu wake aliyekuwa ameongozana nae. Waliegesha gari sehemu na Irina alishuka akiwa uchi na kuvunja nazi kama alivyoelekezwa.

Baada ya kufanya alihokuwa amekusudia huku Watu wakimzomea. Alikimbia mbio ili kurudi kwenye bahati gari yake lakini kwa bahati mbaya Irina aligongwa vibaya na gari na kupoteza maisha papo hapo.

Japokuwa Irina alikuwa amefanikiwa kufanya alichokuwa amekusudia kabla ya kufikwa na umauti, lakini Shaymaa na Abdul hawakutengana wala hawakupata mtikisiko wa aina yoyote.

Kila kwenye jambo jema, Mungu yupo karibu kulisimamia.

Ilikuwa ni ndoa iliyokuwa na furaha na ndani ya Miaka miwili walifanikiwa kupata Mtoto wao wa kwanza wa kike waliyempa jina Rayuu.
MWISHO

Simulizi hii ni ya kubuni wala haina mahusiani na kisa au maisha ya Mtu yoyote. Majina yametumika ili kuleta uhalisia.

JE UMEJIFUNZA NINI KUPITIA SIMULIZI HIi

Said Abdullah

^ SENIOR C E O & PUBLISHER ^ Software engineering ^ Fan of programming ^ Technology Enthusiast.. ^ System developed|C,C++&java 👇Get more news and updates

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button