Simulizi

SIMULIZI|MZOA TAKATAKA SEHEMU YA – 01

Sehemu Ya Kwanza (1)

“Hallo halloo utajijuu tena mimi ndio Mwajei ukisikia mwengine basi ujuwe photo copy bibi ehee… utaisoma number mwaka huu unajisifu unambio msifu na

anae kukimbiza bibi wewe!” ni maneno yaliyo toka kinywani kwa binti mmoja hivi kashombe shombe bila shaka kanywa pombe. Mwembamba, kama ujuavyo

Wanawake wembamba kwa kuongea hawajambo tatizo nguvu ndio hawana. “Oyaa Mwajuma kuna nini hapa mbona unapayuka bila mpango?” Nikawa kama

nimechokoza nyuki vile

“ehee na wewe kifaurongo nilikuwa nakungojea kwa hamu tu nikupe vipande vyako!”

Nikamuuliza

“vipande gani tena dada yangu?”

“tabia ya kukaa kule kijiweni kwenu na kuanza kujisifia unatoka na mimi kimapenzi ukome tena wewe,”

“kwani Mwajei nani amekwambia mimi najitangazia hivyo?”

“Eti natoka na Mwajei pumbavu zako hivi ushaona hii shepu ya kutoka na wazoa taka kama wewe wakati kidudu chenyewe kibamia nikipiga chafya tu

kinachomoka!”

dahaa ni bonge la dharau kinyama yani nikabaki kumtolea macho tu jinsi anavyo nichamba huku akitingisha vikalio vyake kama pasi ya mkaa yani akienda kama

anarudi mdomo umemkaukaa kama kanywa maji ya betri vile sura ngumuu kapaka wanja mpaka nyuma ya sikio yani wee acha tu arafu anajisifu bonge la demu

mmh! nikaona isiwe shida nikasukumiza mkokoteni wangu huyoo mpaka ninapo upaki kwakuwa kazi ya kusomba taka tayari nilikuwa nishamaliza. Na kupata

pesa kidogo, nikarudi zangu getto kufika tu vicheko vya kishambenga vikaanza “hahaha,,..”,hahahaha mama Khadija umemuona?” “kumuona nani tena

mwenzangu?” “ahaaa wee hujui kwani?”

“ahaaa kumbe yule mnuka uvundo”

“kumbe umemuona eheee yani nnzi wote wanamfata yeye!”

“lakini sio vizuri kumcheka kaka wawatu wakati ile ndio kazi yake”

“ohooo wee nae hayakuhusu fata yako hapa naongea na shoga zangu umesikia nenda kapike huko ni maneno ya Mama mwenye nyumba sio siri ananiponda

vibaya sana mpaka nikatamani kuhama kwenye nyumba yake tatizo kwake chumba ndio bei rahisi yani kodi kwa mwezi ni tsh.20000 tu japo hakina umeme ndio

kwaanza nimetoka kijijini kwetu njombe mkoani iringa kuja kusaka maisha town nikafikia kwa jamaa yangu flani hivi kusema kwer nilipofika tu alinipokea

vizuri kwa mikono miwili baada kukaa nae miezi kazaa akaanza visa vya kiboya kwa kuja na mademu na kulala nao ndani mimi nalala nnje mpaka hasubuhi

Nikawa nalala nnje bila kujifunika chochote kile baridi langu mmbu wangu lakini ndio maisha nitafanyaje na nimekuja town kusaka life basi nakumbuka siku

moja nikiwa naosha vyombo akaja na kuinyanyua sufuria ambayo nimeweka miukoko akanimiminia kichwani kisha akanibamiza nayo kichwani huku

akinitukana “malaya wewe mtoto wa mmbwa kudadeki zako naomba pesa yangu uliyo ichukuwa mule ndani huku damu zikinivuja nikamuuliza “pesa ipi kaka

Sele?” unajifanya hujui sio ehee pesa yangu niliiweka chini ya kapeti pale K***mako nipe lasivyo ntakuuwa ohooo nikaona uboya huu pesa sijachukua

kunipasua na sufuria kanipasua afu tena ananitukania mama yangu nikainuka kwa kasi ya ajabu nikamtwanga kichwa nazani hakutegemea mimi kufanya vile

akaenda chini puhu akanyanyuka huku akiwa kafura kwa hasira tatizo uwezo wake mdogo tokea tukiwa wadogo kijijini nilikuwa namdunda tu watu wakajazana

kuja kutuamulia kuna mshkaji anaitwa madebe akasema “oyaa wee Sele yani kumuhifadhi jamaa yako ndio unamnyanyasa hivi ndugu huo uboya kwanza hiyo

pesa unayo sema kachukua si ulimpa demu wako kule unazani hatujakuona ukamwambia akaushe au?” kama umemchoka mwambie ukwer sio kumletea visa vya

kishamba oya boy kama vipi huyu mshamba asikutishe wala nini yeye mwenyewe wa kuja tu!! kaja hapa town michongo yote tumempa sisi leo kinajifanya

kidume embu chukua nguo zako boy tukakae maghetoni wanaume Siku zote twapeana compani leo kwake kesho kwako au sio masera,?” ndio kaka hapo

umechonga nikazama ghetto na kuchukuwa nguo zangu kwa kuziweka kwenye kimfuko cha Rambo nikatoka na washkaji huku nikimuacha Sele analia takribani

miezi mitatu Salumu mie nikawa mzoa takataka ninae julikana tandika temeke mtongani yote walinifahamu kwa utendaji wa kazi yangu kidogo nikipatacho

nakigawa na kukituma kwa wazazi kijijini wakazidi kuniombea baraka niweze kufanikiwa katika maisha sasa leo nyumba niliyo panga nachekwa na wapangaji

hadi mama mwenye nyumba mtetezi wangu ni mmoja tu mtoto wa mama mwenye nyumba anaekwenda kwa jina la Mwanaidi binafsi alitokea kunikubar sana na

kuweza kuniletea chakula pasipo mama yake kutambua

basi baada kutoka kuoga nikiwa napita ndipo nikamsikia mpangaji mmoja wapo anaekwenda kwa jina Hidaya akisema humo chooni kuna nukaje itabidi

umwambie akapige deki, mmh mwambie wewe mi naogopa asije akaninasa mabao hapa,” wee hivi unanisikia au unaniangaria kwa oga anipige aone ndipo

atakapo mtambua baba Mudy siku hiyo

nikiwa nazama gheto kwangu nikagongana na mwanaidi akiwa kajifunga kanga moko tu bira shaka nae anaenda kuoga kanga ikamdondoka na kubaki na chupi tu

jamani!!!

Kitendo cha mwanaidi kanga kumdondoka nikaweza kushuhudia dodo zake zilizo chongoka kifuani kwake ndipo akaiyokota kanga faster na kujifunga kwani

tuliweza kumsikia mama yake akinyanyuka huku akisema “ngojea nikakuletee hiyo pesa yako na leo ndio namaliza deni, nikazama chumbani kwangu huku

mwanaidi akitoka nnje na ndoo yake ya maji akaitwa na mmoja wawapangaji “wee mwanaidi,’ abee dada, huko chooni kuna nuka uvundo ndugu yangu, “kwanini

kunanuka uvundo?” si kaingia yule mzoa takataka,’ kitendo kile mwanaidi hakikupenda hata chembe akatoka chooni na kuanza kumtukana yule Dada “sikia wee

malaya usiekuwa na haya mshenzi wewe lione sura mbayaa kama tako la sokwe uso umekupauka kama mnywa gongo tabia ya kumsema sema kaka wawatu sijui

mnuka uvundo au mnuka kikwapa ukome tena kama ulivyo likoma ziwa la mama yako si akataka kumvaa ikabidi mama yake amzuie na kumwambia “mwanaidi

mwanangu acha basi yaishe ndipo akaenda kuoga “hivi mama mwanaidi mwanao kapewa nini na huyu mkaka mbona anamtetea hivi?” hata sijui mwenzangu, sasa

ipo siku nitamfumua mwanao hapa nimemkaushia kutokana na heshima yako tu vinginevyo ningemdunda vibaya sana,’ mmh hivi wewe unamjuwa mwanaidi au

unamsikia ukitaka habari zake mtafute Mwajuma akwambie kitaa hiki chote wanamsoma usimuone mpore vile mashetani yake yakipanda hadi mama yake

anatoka nduki kama yule kaka ndio anatetewa na mwanaidi mimi simo kabsaa

baada kupita siku tatu nikiwa nimekaa kijiweni njaa nayo inaniuma dahaa yani siku hiyo sikuweza kuambulia chochote taka taka zote zilibebwa na gari ya

manispaa ya temeke nikawa napiga miyaoo tu “aaam dahaa ndipo nikaweza kumshuhudia binti mrembo wa haja mfano wa Jacklin wolper akipita mbele yangu

viatu vya mchuchumio kapiga jeanse aina ya moder imemuwamba na kuweza kuonyesha hipsi zake za maana kapiga top iliyoweza kuacha kitovu chake kiasi

shingoni ana cheni na mikufu ya dhahabu na silver kichwani ananywele zilizo mfika hadi mgongoni sijui zake au wigi mi sijui kwa bahati mbaya akadondosha

kipochi ambacho kilitoka kwenye kimkoba alicho kibeba

nikaenda faster kukiokota na kukisunda ndipo nikakumbuka kauli ya mama akiniambia siku moja “mwanangu kipenzi Salumu usije ukathubutu kumuibia mtu

kitu chake, au kuzurumu cha mtu kama ukaokota kitu na ukamjuwa mwenyewe ni nani basi mpelekee ukifanya hivyo itakuwa vizuri zaidi huenda MWENYEZI

MUNGU akafungua milango ya riziki”

Baada kauli ile kuikumbuka nikajikuta namkimbilia yule Dada na kumkuta ndio anafunguliwa geti aingie ndani nikamwita “sister samahani, akanitizama juu

hadi chini kisha kwa dharau akatema mate chini

Yule aliyemfungulia Geti ni mtoto wa kiume akamwambia “Dada achana nae huyu mzoa takataka tu” akiwa anageuka kuingia ndani yani kanishit! ndipo

nikakitoa kile kipochi na kumwambia “Dada mzigo wako huu umedondosha pale” Akageuka kucheki dahaa hakuamini ikabidi apekuwe kwenye kibegi chake

hakukiona akaja mbio kukipokea kisha akakifungua kukagua hakuamini na kujikuta ananikumbatia.

Kitendo cha yule binti kuja kunikumbatia kilinifanya nipigwe na kitu kama short hivi dahaa kama haitoshi akanikiss kabisa huku akisema “shukrani sana baby

ahaa kaka kwa kuweza kuniletea mzigo wangu kwani kuna vitu vingi sana vya thamani kuna kama dollar 2000 ya kimarecan cheni zangu za dhahabu passport

yangu ya kusafiria n.k sijui nikushukuru vipi embu twende ndani akanishika mkono na kunivutia kwenye mjumba wao wa kifahari dahaa Tanzania nchi masikini

ukiniambia nakataa kuna watu wana pesa wee acha tu basi nikaandaliwa msosi ambao sijawai kula tokea nizaliwe eti dagaa mboga ya masikini akila tajiri

anajenga hafya dahaa lakini nikaweza kugundua kitu kimoja ya kwamba yule kijana akawa amechukia mbaya mi kufanyiwa vile na Dada yake ila sikumjar baada

kula na kushiba ndipo akakaa tupige story mbili tatu akaniuliza “dahaa kumbe ulikuwa na njaa sana ehee?”

wee acha tu ukicheki leo mishe zimekaba mbaya kila kijiwe nikipita manispahaa wamesafisha jiji,’ pole sana hivi unaitwa nani?” kwa jina naitwa Salumu salim

ndio jina nililopewa na wazazi wangu,’ oky unajina zuri sana yani doubre S mimi kwa jina naitwa Joyce Joseph,’ khaa kumbe nawe doubre J kweli noma baada

kuzungumza na kupiga story sana tu ndipo akanipa bahasha rangi ya kaki nikawa nasita kuipokea ila akaniambia “pokea usijari bana hizi pesa kiasi cha shilling

laki 5 zitakusaidia siku mbili tatu tu ndipo nikazipokea akanipa bossiness card yake nikaaga na kuondoka zangu njia nzima nikawa nafurahi kwa kupata zali

nikawa napiga mahesabu ya kwenda kunnua godoro na kitanda na kufungua biashara hata ya genge na kulipa kodi ya chumba mwaka mzima nikiwa sina hili wala

lile nakatiza kichochoro flani hivi nikastukia napigwa roba ya mbao nikajitahidi kujitoa nipambane kiume nikafanikiwa kuitoa na kumtwanga ngumi yule jamaa

kucheki mbele kuna vidume vya shoka vinakuja kucheki huku napo wanakuja nikawa nipo kati kati si unajuwa kichochoro dahaa nikajisemea “hapa kufa na

kupona tu wakanifikia nikajitahidi kupambana lakini wakanizidi nguvu vidume v5 kwa mmoja nikapigwa bapa za mgongo nikawa nisharegea damu tu zinanivuja

kati ya vidume vile mmoja tu kavaa mask usoni wakaichukua ile bahasha na bussnes card wakasepa dahaa

sikuwa na nguvu hata ya kusimama macho yakafumba Giza totoro

sikuweza juwa kilichoendelea nikaja kustuka baada kumwagiwa kitu cha baridii nikaweza kufumbua macho yangu na kuhisi maumivu kila maeneo nikicheki

pembeni nikaweza kumuona Mwanaidi akiwa ameshika bakuri na kitambaa kumbe nilikuwa nipo chumbani kwangu nimelala chini ya mkeka baada Mwanaidi

kuniona nimefumbua macho ndipo akatabasamu huku akijifuta machozi akapaza sauti kwa kuita “Madebe kaka,’ mlango ukasukumwa ndipo akaingia Rafiki

yangu kipenzi Madebe ndio ambaye alinichukuwa kule kwa Sele nikaenda kuishi geto kwake mpaka siku niliyo amua kujitegemea kwa kuondoka kwake japo

hakupenda kwa kuniambia “kaka bado hujapata mchongo wa maana mi naomba ukae tu hapa mpaka unnue godoro kitanda na vinginevyo ndipo uame,’

nikamwambia usijari kaka hata chini nitalala tokea niondoke kwake tukawa tukikutana kijiweni na kupiga story za hapa na pale sasa leo hii washkaji

wanashuhudia niko hoi sio kitandani bali kwenye mkeka Madebe akanisogelea na kuniuliza

“Salumu kaka ni nani amekutendea hivi?”

nikawa sina jibu zaidi ya mchozi kunichuruzika tu kwani sauti haikutoka japo nilijitahidi kuzungumza nikashindwa Madebe kwa hasira alizokuwa nazo akaishia

kupiga ngumi ukutani kwa kusema “shit! kudadeki mshkaji hawezi kuzungumza kitu kubabeki tungewafahamu hao waliomtendea hivi jamaa yetu. Wallahi

kingenuka leo hii

Nikiwa nimelala chini ya mkeka siwezi kunyanyuka wala kupapasa popote kwani mikono ilikuwa mizito sana mpaka nikajishangaa wale vibaka wamenipigaje

mpaka nimekuwa hivi yani nisiweze hata kunyanyua mdomo. Kuzungumza na mtu marafiki zangu kina madebe wakishilikiana na Mwanaidi waliendelea

kunitizama na kunipa huduma za hapa na pale kila siku niliweza kumsikia Madebe akisema “one day jamaa atapona tu na siku atayo nyanyua mdomo na kuwataja

walio mtendea hivi nitakufa na mtu siku hiyo hiyo

siku zikakatika yapata mwezi sasa nikiwa kitandani kwani madebe hakupenda nilale chini ya mkeka akaniletea kitanda cha 5×4 ndio nikawa nalala hapo siku hiyo

Asubuhi nikaweza kusikia mabishano nnje kati ya Mwanaidi na mama yake huku mama yake akisema

“utake usitake utaenda kama mimi ni mama yako niliekuweka tumboni miezi 9 utaenda tu nyau wee!!!

“hata kama umeniweka tumboni mgongoni au wapi siwezi kuolewa na Mwanamme nisiempenda na tena ukiendelea kunilazimisha huyo mwanaume ataipata pata

naweza nikamkata kata hiyo anayo jivunia kuitwa mwanaume”

“thubutu uwezo huo huna huyo nikidume shababi sio huyu mzoga wako ulio lala kitandani!”

dahaa mchozi ulinitoka kwa kusikia naitwa mzoga jamani binaadamu ndivyo walivyo,

“sikia wee mzee nikwambie kama mzoga ni mumeo na wazazi wako,’ “haa yani Mwanaidi umefikia hatua ya kumwita baba ako na bibi na babu yako mizigo sio

wee mtoto ntakuachia radhi Ohio”,,,,, nikasikia vishindo vya kukimbizana kikili kakala huku Mama Mwanaidi akipiga kelele “jamaniiii majilaniii nakufaa njoeni

mnisaidieee!!!

nikatamani kutoka kwenda kusaidia nikashindwa ndipo sauti zikasikika za majilani

“wee Mama Mwanaidi vipi embu fungua mlango kwanza, “sifungui Mwanaidi anataka kuniuwaa kusikia eti Mwanaidi anataka kumuua mama yake

nikajikakamua kusimama mpaka nikaweza cha ajabu nikasimama kabisa nikapiga hatua mbili tatu na kupaza sauti kwa kuita “Mwanaidiiiiiii

iii…huku nikitoka kufika mlangoni tukagongana vichwa puhuu kumbe yeye baada kuisikia sauti yangu akawa anakuja mbio tukabaki kutizamana kila mmoja

akihema si tukaanza kucheka,

Ha!ha!ha!ha! Akaniuliza

“baby ni wewe au?”

“ndio mimi dear tukakumbatiana kwa furaha huku machozi yakitutoka binafsi hakuna aliye tegemea mi kupona ghafla vile wakati

Madebe anahangaika kutafuta pesa nipelekwe hospital kwani pesa haikuwepo nikaenda kuoga nikaandaliwa chakula nikala

Mwanaidi akaniita Salumu my dear” nikaitikia,

“naamu Mwanaidi niambie”

akawa anajing’ata ng’ata kucha huku akilembua macho yake kisha akanitamkia

“nakupeenda naitaji uwe baba wa watoto wangu Salumu!”

kwanza nikashituka si akaja kunikumbatia na kukutanisha midomo yetu dahaa toto midomo lainiiii kama naramba sufi vile ghafla mlango ukasukumwa wote

tukageuza shingo zetu kuangalia mlangoni.

Majanga hakuwa mwengine

zaidi ya Madebe

akataka kurudi nnje maana alicho kiona hakuamini

macho yake.

Yani mgonjwa

aliye muacha kitandani hawezi kusimama wala kuongea

leo hii kama miujiza anamkuta yupo kifuani kwa Mwanamke anazinyonya chuchu,

nikainuka kutoka

pale kitandani na kwenda kukumbatiana nae maana alikuwa anafikicha fikicha macho

“eee Mungu baba kila jinsi ya sifa njema ni zako tunakushukuru kwa kuweza kujibu maombi yetu japo hatuingi Msikitini kufanya ibada yeyote ile ila

umeyapokea maombi yetu”,,,,,

ni maneno

ya Madebe

huku machozi

yakimtoka

nikamfuta machozi na kumwambia

“hakika Mungu ni mwema sana!”

Tukakaa chini na kuanza kuwapa full story kwa kile kilicho nitokea,

“dahaa pole sana kamanda wetu ila kisasi lazima kifanyike. Usiku huu huu tunamteka yule boya kisha tunamzamisha kwenye Mjumba ataeleza tu cha kwanza

ataje pesa ziko wapi kingine awataje wenzie wote kuanzia sasa tunakinukisha kitaa au sio?”

Nikaitikia,

“ndio kaka” basi kila mmoja akagonga tano na kusepa zao. Ndani ya chumba nikabaki mimi na Mwanaidi tukabaki kuangaliana kama vile, majogoo yanayo

tamaniana kupigana”

nikamtekenya kwenye mbavu mtoto wa kike akashituka huku sauti ya kuguna ahaaaaa,,,mi stakiii

nikamshika kiunoni na kumtekenya zaidi siwezi kukwambia nili enjoi vipi tunda la binti yule kigori usiku kucha ali

lala kwangu,

maana mama yake hakuwepo siku hiyo nikawa mimi ni kama baba mwenye nyumba

wapangaji walio

tuona nikienda bafuni

kuoga na

Mwanaidi wakabaki kusonya tu huku wakipindisha midomo yao kama kishuzi.

Siku hiyo nikiwa kitaa cha temeke mikoroshini

nazoa takataka kusema kweli sikuwa na vitendea kazi

kama Groups au choteo

la kuzolea taka zaidi ya kunyanyua migunia viroba na matenga nikiwa nishajaza rumbesa la taka huku njaa ikiniuma vibaya sana maana mpaka saa saba mchana

sikuweza kutia chochote kitu

tumboni kwangu.

Nikiwa najikakamua kusukumiza mkokoteni. Ghafla nikasikia sauti nyuma yangu

“za saa hizi mjukuu wangu?”

nikasimamisha mkokoteni na kumuangalia huyo anaye nisalimia ni nani?…..

kabla ya kumuitikia alikuwa ni Bibi kikongwe sana maana hata kusimama vyema hakuweza zaidi

ya kuupindisha mgongo wake sijui kiuno kinamuuma au. Mkononi ame beba mkongoja pamoja na kimkoba flani hivi, nikamuitikia

“sijambo Bibi yangu shikamoo!!!

akaitikia “marahabaa Baba nilikuwa naomba msaada wako baba hapa unionapo tokea jana usiku sijatia chochote kitu tumboni kwangu

nahisi utumbo

una nikata kata!”

nikabaki kumkodolea

macho tu na kuwaza hapa nilipo mi mwenyewe mfukoni nina shilling mia tano tu kingine

sijala tokea Asubuhi

sasa huyu bibi nitamsaidia vipi”……

nikamtizama

vizuri na kuona

maeneo ya tumboni kwake

kafunga jiwe kwa ajili ya kuzuia njaa

nafsi ikanisuta kwa kuniambia

Salumu embu mpe msaada huyo bibi

ndio wewe una njaa ila hukufunga jiwe kuzuia njaa tena unasukumiza mkokoteni wenye mizigo mizito

huyo bibi kashindwa

kustahamili mpaka kafunga jiwe,

nikajikuta namwambia “bibi nifate japo alitembea kwa shida sana akanifata mpaka kwa mama Somoe na kumuonyesha sehemu ya kukaa baada Bibi kukaa huku

akipepesa macho na kujiramba ramba kwa kutamani msosi maana aliwakuta wateja wengine wakigonga menu

nikamshika mkono mama

Somoe na kwenda nae chemba kidogo

“ehee vipi tena baba wewe mbona tunavutania pembeni?”

“ahaa hamna kitu sema nini!!!

“ndio nakusikiliza boss wangu,

“sasa mimi hapa sina kitu mfukoni nina jero tu so kama vipi mpatie msosi yule bibi kisha jioni nitakucheki,

“hamna shida boss wangu,

basi akaenda kumuandalia chakula na kumtengea yule bibi

binafsi alikuwa na njaa sana akakifakamia chakula chote,

nikaondoka na mkokoteni wangu kwenda kumwaga takataka dampo

yapata saa kumi na moja jioni niko masikani na kina

Madebe huku tukipiga story za hapa na pale

“oyaa Salumu kaka ule mchongo wetu tumeupanga leo lazima ufanyike time ya kama saa nne usiku hivi tunavamia pale na kumchomoa yule dogo kitu

nitakacho mfanyia atajuta kwa nini kazaliwa mwanaume

pumbavu zake,

ni maneno aliyo kuwa akiyatoa

Madebe mpaka mwili ukanisisimka kwa vitisho vile,

nikatoka zangu maskani na kurudi zangu ghetto cha ajabu nikakuta chumba changu kufuri sio ile ya kwangu nikatoka mpaka uwani na kumkuta

Mwanaidi akiwa amelala mapajani

kwa Mwanaume huku akimchezea kidevu na yeye akichezewa nywere na kushikwa shikwa katika maungo yake

nilibaki kuduwaa tu

na hata alipo niona

Mwanaidi hakustuka wala kujali lolote

nikasikia sauti ya kicheko

cha kimbea kikitokea nyuma yangu

“aha!ha!ha!ha warereeee!!! utaishia kula kwa macho tu mnuka uvundo,

ni maneno ya mama

Mwanaida na kunipushi huku akisema “embu nipishege mie!!!

nikayumba kabla ya kuushikilia ukuta

Mwanaidi kwa kuniumiza roho zaidi akanyonyana denda na yule jamaa mbele ya macho yangu

aseee!!!

dahaa inauma sana hii kidume nikajikaza baada kuikumbuka

kauli ya mama akiniambia

“mwanangu

Salumu katika dunia hii usimuamini mtu yeyote yule zaidi ya mimi mama yako na tambua ya kwamba wanawake ni kama nyoka muda wowote ule anaweza

kukubadirika

kwahiyo kuwa makini sana mwanangu,

nikatoka nikiwa sijui naenda wapi maana binafsi nilikuwa nime changanyikiwa si kidogo

nikastushwa na mlio waoni maana nusu nusu nigongwe nikajikuta nadondokea kwenye mtaro wa maji machafu kwa presha dereva wa ile gari aina ya Benz

macho ya paka

akafunga break gafla

akijuwa tayali

kashauwa akashuka na kuja mbio kwenye mtaro nikawa ndio natoka macho yetu yaka

gongana na binti mrembo huwa na penda kuwaita

Jacklin wolper maana hapa kwetu sijaona dada mrembo kama huyu sijui wewe katika macho yako unamkubali nani ila wolper kauteka moyo wangu,’

binti huyu hakuwa mwingine bali ni

Joyce hata yeye alipo niona akabaki kushangaa “whao!!! si

Salumu wewe?” Nikamuitikia kwa kichwa huku nikijiandaa kutoka kwenye mtaro akanipa mkono kwa ishara ya kunivuta nikampatia ile ananivuta tu nikajikuta

namvuta yeye

na yeye akaja vupuu kwenye mtaro na kujikuta mimi juu yeye chini huku face zetu zikiwa karibu zaidi akaanza kujichekesha kwa aibu watu walio weza

kushuhudia mchezo ule wakahisi muvi zetu za kibongo

tu maana gari hata haijanigusa

nimechumpa mtaroni wakabaki wakicheka tu kidume nikatoka na kumpa mkono

Joyce akatoka huku akisema

“kweli nimeamini Mwanaume ni mwanaume tu mi baada kukuvuta wewe kumbe navutwa mimi,

tukabaki kucheka tu kabla ya kuniuliza

“vipi tena mwenzetu

una tembea macho juu juu una tatizo gani?”

sikuweza kumjibu kitu zaidi ya mchozi kunidondoka pasipo

kujitambua akanishika mkono na kuniomba niingie kwenye gari

aina ya Benzi.

Nikazunguka upande wa pili wa gari ili nipande nafsi yangu ikasita baada kuona kwa jinsi ile gari ilivyo kuwa safi wakati huo Joyce kashapanda akaniuliza “vipi

tena mbona hauwingii kwenye gari?”

nikamjibu “kusema kweli siwezi kupanda nitakuja kuchafua siti bule!!! akacheeka na kuniambia embu

Salumu acha ushamba bwana ingia twenzetu kama viti vikichafuka vitaoshwa tu wee usijali ingia tu,

basi nikapanda ndani ya ndika yenye kiyoyozi sijui mnaita kipupwe huku mziki laini kutoka kwa west life unao kwenda kwa jina la my love ukilindima na

kunifanya nijisikie burudani, kila mmoja akawa kimya sikuweza kufahamu

Joyce anawaza nini zaidi ya kuwa makini kuendeesha gari basi safari ikazidi kusonga nisijuwe wapi tunakwenda na kigiza nacho ndio kina jongea, tukafika

sehemu moja

sijui hotelini au vipi akabaki gari maana hiyo sehemu kulikuwa na magari mengi tu yakishua basi tukashuka na kuingia ndani ya hoteli hiyo

“whaoo

Joyce huyoo, ni sauti ya binti mmoja akija mbio kumkumbatia Joyce

hakuwa peke yake kulikuwa na kikundi wanaume kwa wanawake basi

Joyce akafanya kunitambulisha ya kwamba mimi ni rafiki yake basi kila mmoja akanipa mkono wa bashasha nikaweza kukaa na kuagiza kile ambacho kina nifaa

furaha ikaongezeaka zaidi na kunifanya niweze kusahau mawazo ya kuachwa na Mwanaidi

kuna muda Joyce akanyanyuka sijui kwenda chooni au vipi mi sijui zikapita dakika kama tatu hivi tokea Joyce ainuke pale nikajikuta naguswa begani kucheki ni

muhudumu wa hoteli ile nikamuuliza “nikusaidie nini Dada yangu?”

akanijibu ya kwamba “unaitwa kule nnje na mwenyeji wako,”

nikajuwa bila shaka Joyce anaitaji tuondoke basi nikajinyanyuwa na kuwaaga wale nilio kaa nao meza moja nikatoka nnje nikakuta hali ya ukimya flani hivi

nikaisogerea gari kitendo cha kuifikia tu gafla nikapigwa na kitu kizito kichwani kikitokea nyuma yangu nikayumba yumba huku nikiona dunia inazunguka

mwishoe nikaenda chini

nisijuwe kinacho endelea,

ni sauti ya watu wakiulizana na maji kunimwagikia ndio ikanifanya nifumbuwe macho yangu japo kwa shida sana maana maumivu ya kichwa yalikuwa bado

hayajapoa nikajaribu kujinyanyua hamadi Mungu wangu nina bokxa tu mwilini mwangu sina nguo nyingine yeyote ina maana baada kupigwa nilivuliwa nguo au

wali nitupa vibaka ndio wakanisaura sikuweza kupata jibu zaidi ya mchozi kunitoka tu nikajiinua huku nimeshikilia sehemu zangu za sili huku nikitetemeka

kuna baazi ya watu wakasema mchawi kila mmoja akasema lake mwisho wakajadiliana nipelekwe kituo cha police,

nikanyanyuliwa msobe msobe huku nikipigwa mikofi ya maana na vijana wenzangu wasio kuwa na utu hata chembe “kijana mdogo unakuwa mchawi oyaa huyu

sio wa kumpeleka police dawa yake ni moto tu nikawashwa ngumi mitama na makofi nilipigwa kwa kugombewa kama vile mpira wa kona bahati nzuri police

wali shapewa taarifa kwa kukamatwa mchawi maeneo yale wakaja kunitoa mikononi mwa wananchi wenye hasira kali nikapigwa pingu damu chapa chapa ziki

nivuja nikapelekwa kituo cha police pale manzese na kusweka ndani hata huduma ya kutibu majeraha yangu sikupewa nikabaki kuugulia maumivu tu huku

nikijiuliza maswali mengi pasipo kupata majibu,

why me?” kwa nini mimi?

eee Mwenyezi Mungu ni kipi nimekosea katika dunia hii ni dhambi gani kubwa niliyo ifanya mpaka nateseka hivyo

furaha yangu ya muda mateso yangu yasio fika kikomo why?”

nilijiuliza maswali tu,

Salumu nililia maumivu yakazidi kunizidia Joyce nimekukosea nini mimi je nilifanya makosa kukuokotea kipochi chako na kukuletea

hii ni mara ya pili sasa napigwa Joyce nijibu basi unaitaji nife?”

nilijiuliza mwishoe mchozi unanimwagika dahaa yapata saa kumi alasiri nikasikia afande akilitaja jina langu kwa kuniita nika jinyanyua kiuvivu uvivu na

kwenda karibu na nondo za sero sikuweza kuamini macho yangu baada kuwaona washikaji zangu wakiongozwa na

Madebe wamefika pale kituoni hata wao wakastuka baada kuniona nikiwa katika hali ile,

Madebe midomo ikawa inamtetemeka kwa hasira huku akitamani kupiga hata afande basi nikatolewa

nikiwa ndani ya boksa tu iliyo lowana damu alicho kifanya

Madebe ni kuivua jeanse yake akabaki na bukta aina ya jenzi akanipatia ile suruwali niivae nikaivaa kisha

Sheby akavua T-shirt yake na kubaki na vest akanipa T-shirt nivae baada maandikishiano wakaondoka na mimi ndani ya daladala nikawapa mkasa mzima huku

nikimtupia kila laana Joyce na kumuuliza

Madebe wamejuwaji kama mimi nimekamatwa na tena nipo kituo cha police manzese?”

Madebe akajibu unajuwa jana usiku tulikuwa tushajiandaa kwenda kumteka yule boya sasa tukiwa tushakusanyika pale maskani tukawa tunakungojea wewe tu

muda ukazidi kwenda pasipo wewe kutokea tukaona kama vipi tukutimbie maguu mpaka maghetoni baada kufika pale tukakukosa tukachekecha akili pasipo

kupata jibu,

na tusingeweza kufanya uvamizi pasipo kuwapo wewe tukarudi maskani yapata saa tano hiyo baazi ya washkaji wakasepa kwenda kulala huku wakisema ishu

imebuma

baada kukaa kitambo kidogo tukaona kuna gari ikija kwa kasi pale maskani tukajuwa labda maafande kila mmoja akasepa kimtindo wake ila mimi na

Shaibu tukanyuti chemba kidogo ile gari aina ya benzi macho ya paka ikafunga break kwa kasi sana tukaweza kumuona msichana mmoja hivi akishuka huku

akipiga kelele “jamani!!! salumu nisaidieni!!! salumu jamani anakufaa!!!!

baada kusikia akitaja jina lako

ITAENDELEA

Said Abdullah

^ SENIOR C E O & PUBLISHER ^ Software engineering ^ Fan of programming ^ Technology Enthusiast.. ^ System developed|C,C++&java 👇Get more news and updates

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button