Simulizi

SIMULIZI|MZOA TAKATAKA SEHEMU YA – 05

IMEANDIKWA NA : HAFIDHI J IKRAM

Sehemu Ya Tano (5)

Ikabidi niulize

“Jackson ndugu yangu nini tatizo mpaka mnazozana hivyo?”

Akanijibu,

“muulize huyu mpangaji wako anaakili za kiboya yani mambo yangu Mimi yeye anaenda kuyatangaza kule kijiweni sijui yana muhusu nini”

Ikabidi nitumie busara kuweza kuwapatanisha kwanza nikamuonya

Bulongo kwa kumwambia

“haipendezi mtu kuwa muongo au mmbea kwa kuhadithia kila analo

lisikia au kuliona je unapenda kula nyama ya ndugu yako?”

Kwa upole akanijibu

“hapana kaka Salumu siwezi hata iweje!”

“Sasa kama huwezi basi kitendo cha kukaa sehemu na kuanza kuongea maneno ya kumteta mtu iwe kwa mazuri au kwa mabaya huko ni kusengenya kwahiyo ni

sawa na kula nyama ya ndugu yako!”

Kingine kila penye ugomvi basi Shetani huchochea kuni na kujitahidi kupuliza moto ili mpigane muumizane

Iwe furaha kwake yeye,

Binafsi naomba sameheaneni muwe kitu kimoja,

Basi wakapeana mikono na kuombana msamaha,

Hivi ndivyo inavyotakiwa ajabu utakuta watu wengine waliokosa akili hata za kufikiri tu,

Wanakuta watu wanagombana jitu zima kujifanya punguwani anachota mchanga na kusema puta mambo hayo ya watoto wadogo sio wewe

Unaenyonyesha au una mindevu na mvi kibao,

Baada kuona tayari wamepatana nikaingia chumbani kwangu, na kufanya baazi ya mambo kama kuosha vyombo na kupika chakula cha usiku

Nikiwa bado jikoni

Rahma akaweza kufika na kuniuliza

“baby leo ulikuwa wapi maana nimekuja hapa kama mara tatu sijakukuta kibaya zaidi napiga simu yako inaita tu ndani, kutizama Mkokoteni wako upo ehee

niambie ulienda kwa Malaya gani?”

Nikamtizama my baby usoni kisha nikamkonyeza kijicho,

“bwana mi staki unajuwa mwenzako mapigo ya Moyo yananienda kasi niambie ulikuwa wapi?”

“baby bwana punguza presha basi mwenzako leo hii nilienda kwa yule Bibi muokota makopo kwenda kuchukuwa dawa. Si unajuwa ndugu zake marehemu

Madebe wanataka kunitoa kafara kisa hiki kibanda?”…..

“Ahaa kumbe nilijuwa umeenda kwa kimada embu pisha nipike huko!”

Kwa sauti ya kudeka Rahma akaniambia hivyo nikanyanyuka na kumtekenya kisha nikakimbia,

“ahahaha,,,assess,,,mi staki bwana ujuwe nitaunguza chakula”

Nikatoka zangu mpaka masikani na kuwakuta washikaji wakipiga story za hapa na pale,

“ehee afadhali Salumu umefika jembe letu maana jembe kubwa ndio limetutoka”

Nikawapa tano washikaji kisha nikakaa kwenye benchi,

huku nikisema

“leteni habari mpya kitaa vipi wana mnasemaje?”

Azizi akadakia kwa kujibu

“Hatuna cha kusema kaka labda Zuberi hapo maana alikuwa anakuulizia muda tu”

Nikamtizama Zuberi na kutabasamu

Ndipo

Zuber akaanza kusema

“habari mpya zipo nyingi tu, kikubwa hapa tulikuwa tukijadili swala zima la mali za marehemu Madebe,

Kwanza kabisa Madebe tokea tukiwa watoto hakuwai kusema kama ana ndugu wowote tuliangaika pamoja kuuza biskuti pipi

Na mzagazaga kibao tu kwenye magari.

Tukabonda kokoto na kubeba zege,

Mara kibao tulikamatwa na Mapolisi kwa kuonekana sisi wezi,

Kama ujuavyo Mungu siku zote hamtupi mja wake tukaweza kupata maisha mazuri na kujenga nyumba zetu. Leo hii ajabu

Madebe kafariki ndio ndugu zake wanajitokeza kutaka Urithi, siku zote walikuwa wapi?…….

Zuberi alizungumza maneno yale kwa uchungu sana mpaka machozi yakamtoka.

Ikabidi nimbembeleze, huku nikimwambia

Asijali sana kwani kila kitu kitakwisha tu”

Kwa sauti ya kwikwi yenye kuambatana na kilio Zuberi akasema

“Salumu kaka hakika kuna mambo muda mwingine yanaumiza moyo.

Binafsi marehemu Madebe kuna siku alisema kama atakuja kufa kwanza yeye, basi tuakikishe kila kitu chake kinabaki mikononi mwako.

Wewe ndie ndugu pekee uliyebakia kwenye maisha yake!”

Washikaji wote wakasema hakika watapambana kiume kuakikisha ya kwamba hao mafisadi waliojitokeza hawapati hata shilling kumi.

Tuliongea mambo mengi sana huku tukipanga mikakati ya hapa na pale,

Nikarudi zangu nyumbani njia nzima nikawa najiuliza, kama Madebe hakuwa na ndugu je katokea wapi…..”ina maana hana Wazazi na kwanini kaitaji mali zake

nibaki nazo Mimi wakati sio ndugu yake

Wema gani nimemtendea mpaka kaamua kunilipa kitu kikubwa kama hiki”……je mambo haya yapo katika jamii mtu kumrithisha mali Rafiki yake

Nikafika nyumbani na kumkuta Rahma ananisubiri kwa hamu baada kuniona akaja kunikumbatia kisha nikapelekwa bafuni kuogeshwa baada hapo nikala na

kulishiba ahaa sio kushiba ni kulizika maana Mwanaume ashibi anaeshiba ni Mwanamke tu,

Baada ya kula Rahma akaondoa vyombo na kwenda kuviweka jikoni.

Ukafika muda wakulala tukapanda kitandani kila mmoja akiwa na mhemuko wa kumuhitaji mwenzie. Kwa macho maregevu yenye kutawaliwa na kama

kausingizi fulani hivi

Rahma akaniangalia, na kuuleta mdomo wangu kwangu,

sikutaka kujiuliza mtoto anataka kuning’ata au vipi”,,,,,,,,nikampokea na kuanza kumung’unya dodo

hakika Rahma alikuwa mtundu kila kona nikipeleka kitu nae anaenda uzuri hakuwa gogo kama baazi ya Wanawake wengine

Mtoto anarembua macho utasema

amekula sijui Kungu manga,,,

Assess,,,,ohooo,,,mmmm,,,,ndio miguno aliyokuwa akiitoa pindi alipoumeza muhogo wangu wa jang’ombe.

Mpaka tunafika mshindo kila mmoja alikuwa hoi tukajitupia pembeni kulala

Salumu sikutaka kusahau kile ambacho alinipa Bibi, nikafanya kuichukuwa ile dawa na kuipaka usoni kama mafuta vile kisha nikalala

Usingizi haukuchelewa kunipitia.

Sikumbuki ilikuwa saa ngapi”,,,,,,

ila usiku uleule nikaja kushituka

kwa kufumbua macho

yangu kwanza nikawa naona

maluweluwe sijui nyota nyota.

Nikabaki kustaajabu sana

Baada kuweza kuona ndani ya chumba changu,

Kuna kikundi cha watu kama watano hivi sura zao ni zenye kutisha sijui wamejipaka masinzi au matope siwezi kufahamu,

Nikahisi labda ndoto,

naota tu muda si mrefu nitazinduka.

Ajabu haikuwa hivyo, nikakumbuka dawa aliyoweza kunipa bibi.

Vile viumbe baada kusimama kama dakika tano hivi huku wakiongea maneno fulani kwa kunong’onezana kisha mmoja wao ambaye alikuwa ni Mwanadada

akaanza kukizunguka kitanda chetu,

akazunguka kwa muda huku akiimba wenzake wakipiga makofi

Akapanda kitandani na kuja kumkalia Rahma tumboni na kumsotea kitendo kile kikanifanya niwe na hasira na kutamani kuinuka, nikabaki

kuhofia naweza kuuwawa maana kawaida ya mchawi akitambua ya kwamba umemjuwa

atafanya kila namna aweze kukuondoa hapa duniani.

Baada kumsotea Rahma na kumtambuka wenzake wakaja na kumbeba kisha wakamshusha chini,

Nikabaki kujikausha tu sijui wakamfanyia nini pale chini mwishoe wakampandisha kitandani

ikawa zamu yangu kukaliwa akaja na kuanza kunisotea

jamani huyu binti alikuwa na kitu cha maana utasema Chura wa Snura,,,,kule kunisotea nikajikuta mnara wangu unasimama pasipo kutalajia hakika nikatamani

kukishika japo kiuno chake kwa style ya kuvizia nikashika

Kalio lake nikamfinya ghafla akashituka na kuruka kutoka kitandani na

kwenda kwa wenzie akiwa haamini

Wenzake kwa ishara wakamuuliza vipi”……akatoa maelezo kisha wote kwa pamoja wakaja kitandani kuja kuangalia vizuri wakamkagua kwanza Rahma kisha

Mimi kidume utasema nacheza movie vile nilikuwa kimyaa mmoja wao akasema tena kwa sauti niliyoweza kuifahamu vyema,

“Wewe Zaituni mbona unakuwa muoga namna hiyo hawa wote wapo katika nusu kuzimu, kuamka sio muda huu embu endelea na kazi!”

yule binti sijui ndio Zaituni aliyetajwa akasema

“Binafsi mizuka yangu yote ishakata ninachoona hapa tuondoke tu tupange tuje siku nyingine,

Baada kusema vile wakapotea kupitia pembe ya Chumba, baada kupita dakika kadhaa nikaanza kucheka

yani nilicheka mpaka Rahma nae akashituka kutoka usingizini,

Wakati huo nikiwa nimesimama akaniangalia huku akifikicha macho na kuniuliza

“Baby nini tena mbona Vicheko usiku wote huu unacheka kitu gani?”

Sikuweza kumjibu kitu zaidi ya kuendelea kucheka,

“Baby umzima kweli au Maralia imekupanda kichwani nini”,,,,,baby..

Rahma nae akanynyuka kutoka kitandani na kuja kunishika huku akinipapasa Usoni

Akanishika mkono na kunirudisha kitandani niweze kukaa….

Maswali yake yakakosa majibu kwa mfano kama wewe ungemjibu nini”,,,,,,,,

“baby unatatizo gani mbona unijibu

(Why?”)

Nikamshika kiuno na kumwambia tulale nitampa maelezo pakikucha,

Kesho yake Asubuhi nilijikuta nachelewa kuamka nikapapasa pembeni yangu Rahma hakuwepo

basi nikajizoazoa kutoka kitandani, nikatoka mpaka ukumbini huku nikijinyoosha na kuangalia pande zote

Nikatoka hadi nnje na kukutana na wapangaji tu nikapeana nao Salamu

Kuna mdada mmoja alikuwa anafuwa,

Akaniambia

“naona siku hizi sio Mzoa takataka tena umekuwa boss!”

Nikamtizama na kumuuliza

“Kwanini unasema hivyo Salima?”

Akanijibu kwa kusema

“unajuwa wewe Salumu haukuwa mtu wa kulala mpaka saa nne Asubuhi wewe ulikuwa saa kumi na moja Alfajir ushaamka unachukuwa mkokoteni wako

huyoo unaenda kuwajibika

Nashangaa tokea Afariki kaka yako

Madebe uendi tena kuzoa Taka”

“Aisee ni kweli ukisemacho Salma yani kwa kipindi hiki nimekuwa mvivu kwa sababu kuna Mambo mengi sana yamenizunguka kwahiyo naitaji kuweka kila

kitu sawa. Kisha nianze kuingiza Benzi langu kitaa,

“Sawa fanya hivyo kaka yangu maana uko mtaani kila kona ukipita Mitakataka kibao imerundikana,

Sijui manispaa ya wilaya hii wamekususia wewe!”

“unajuwa Mimi hii manispaa yetu siwaelewi kabisa yani Mimi nikiingia na mkokoteni wangu, na wao hao

Sasa ajabu mie niko busy

Sijui wao wanafanya nini”,,,,,,,,

Salma hakuwa na neno la kuongeza ndipo nikakumbuka Ahadi niliyompa bibi jana usiku

Nikaona dahaa nitakuwa nimechelewa balaa nikafanya haraka kwenda huko.

Nikasikia naitwa baada kukatiza mtaa mmoja hivi,

“wee mkaka”

Nikageuka kwanza kabla ya kuitikia na kumuona Mwanamama akiwa pamoja na sijui mumewe au,,,,akaniita kwa ishara ya mkono, nikaenda kumsikiliza

Kwanza nikawaamkia,

“Shikamooni wazee wangu sijui niwasaidie nini?”

“Marhabaa kijana, shida yetu kubwa ilikuwa ni wewe”

wewe si ndio Mzoa takataka?”

Nikaitikia kwa kutikisa kichwa kuashilia ndio ni mimi.

yule Mwanamama akaniuliza

“sasa kijana mbona siku hizi hauji kuzoa takataka nini tatizo mwanangu”

Kabla ya kujibu nikafikilia kidogo kisha nikajibu,

“Sijui niseme nini Mama yangu kiukweli kabisa mkokoteni wangu matairi yamepata pancha kingine umeshakuwa mbovu na pesa ya kuupeleka kwa fundi sina,

Yule Baba akaniuliza huku akisema

“kwanza pole sana kijana wangu naomba kujuwa ni kiasi gani kinaitajika huko kwa fundi”……maana kwa sasa tunakosa raha kabisa takataka zimerundika ndani

nnje mpaka zinanuka Aisee imekuwa kero kubwa sana kwetu!”

Nikamjibu kwa kusema

“kwasasa bado sijaupeleka kwa fundi bado kama upo tayari kunisaidia hiko kiasi cha pesa

Wacha leo niende kuongea na fundi kisha nitakuja kukuona mzee Wangu!”

“sawa kijana fanya hivyo maana tutashukuru sana kuonyesha msisitizo kamata kiasi hiki kwanza,

Sikuweza kuamini ananipatia kiasi cha pesa

Shilling elfu ishillini, duhuu nikaona kama ndoto

Nikaagana nao na kuendelea na safari ya kwenda kwa bibi

Wakati nakalibia kufika

Kwanza nikashangaa baada kuona kwenye kile kibanda cha bibi watu wamejazana. Nikabaki kujiuliza kuna nini pale,.

Nikapiga hatua za haraka na

kukuta watu wakijadili ili na lile

Kwakuwa nilikuwa kila mmoja namfahamu

Nikamfata kijana mmoja na kumuuliza.

“Mambo vipi kaka kuna nini hapa?”

Akanijibu jibu ambalo likanifanya nishituke zaidi,

“Kaka wee acha tu huyu Bibi muokota makopo amevuta aisee yani amekufa hapa tulipo tulikuwa tuanajadili jinsi ya kuwapata ndugu zake kiukweli hakuna

anaefahamu walipo Muafaka umefikiwa atazikwa na Manispaa!”

Sikuweza kuamini nikajikuta natoka mbio kuingia kwenye ndani ya kibanda kile.

Juu ya kitanda cha kamba ndipo mwili ulikuwa umelala wakati huo

umefunikwa na shuka jeupe nikaufunua.

Ni kweli Bibi alikuwa hapumui nikaanza kuita na kuongea huku nikilia

“Bibi”……amka…..tafadhali,,,nishakuja kukuletea pesa ya vitafunwa na chai,,,,bibi Amka tukaokote makopo kule kwa mpemba nimeyakuta mengi tu.

Bibi tukio gani ulilifanya mpaka ukasema utanisimulia leo….bibi amka basi,,,,,,,nili

lia kama mtoto mdogo

Hata kwenye msiba wa rafiki yangu

Madebe sikulia kama hivyo,

Nikaja kushikwa na kutolewa nnje,

Gari ya Manispaa ikafika kwa ajili ya kuuchukuwa mwili wa Bibi

Nikapaza sauti kwa kusema

“hapana,,,,,hapana mwili wa bibi yangu hauwezi kuzikwa kama kama Kunguru au mzoga wa Kuku,

Kama mmeshindwa kujitolea kunisaidia kumzika bibi yangu nitamzika Mimi mwenyewe.

Kila mmoja akabaki kushangaa wakati huo kina Zuber na Washikaji wengine ndio wanafika wakaja kunituliza maana ni wao ndio wanaojuwa ukaribu wangu

Mimi na marehemu yule

Zuberi akasema

“Kama mlivyoweza kusikia

Bibi hawezi kuzikwa na manispaa wakati sisi wajukuu zake kama watoto wake tu kuanzia sasa tutasimama pamoja kumzika bibi yetu

Tunaomba kila mmoja apotee eneo hili

Yani kumzika mtu mpaka awe ndugu yako au wajilani kama hana ndugu

Muite manispaa sio!”.

Nikiwa bado nalia ndipo nikamkumbuka bwana Tariq

Mmoja kati ya matajili hapa nchini na ndio mtoto mkubwa wa bibi nikaongea na Zuberi kuhusu jambo lile akasema huku akishangaa

“khaa! Salumu kaka unataka kusema kweli au”,,,,,yani unataka kusema huyu bwana Tariq yule tajili ndio mtoto wa huyu bibi?”

“ndio jana tu kanipa full story

Ndugu”

Kuna kitu Zuberi akafikilia kisha akasema.

“ok! kama ni kweli binafsi Mimi napafahamu kazini kwake hadi nyumbani kwake anaishi huko Mbuyuni kule maeneo ya Namanga”

Namie nikashangaa na kuuliza

“unasema kweli Zuberi au utani?”

Akanijibu

“ni kweli ndugu kama vipi twende kwanza kazini kwake pale Posta ya zamani tukimkosa twende nyumbani kwake au vipi hapo?”

Nikamuitikia sawa ikabidi tuwape taarifa kina Azizi na wengineo nao wakakubaliana nasi.

Tukatoka kwenda huko Posta

baada kufika tukavuka barabara na kuingia mitaa kadhaa hatimae nnje ya jengo kubwa gorofa yenye vioo ndio tukasimama kwanza ikabidi tumuulize

Fundi viatu

Tuliyemkuta kwenye ubize wa kushona kiatu,

“Habari za saa hizi kaka yangu?”

Nilianza kusalimia hivyo

Nae akaitikia

“Nzuri tu Kaka sijui nyie!”

“Sie wazima tunamshukuru Allah

Sema Kaka kuna mtu tunamuulizia anaitwa bwana Tariq Wahidi sijui kama unamfahamu?”

Akacheka kidogo na kutabasamu

“Unajuwa ndugu yangu swali lako ni kama kichekesho kwangu kwanza huyo mtu kwajinsi alivyo maarufu ni sawa na kuulizia Ndevu kwa Osama bin laden

huyo Tanzania nzima tuseme dunia

Wanamfahamu.

Nikamwambia huku namie nikilazimisha tabasamu

“Ndio inawezekekana kila mtu anamfahamu kwa jina lake sio kwa sura hata Bakharesa ni watu wachache ndio wanamfahamu kwa sura wengi wanamfahamu

kwa jina tu”

“Sawa ndugu hapo nimekupata kwa kifupi Bwana Tariq wahidi namfahamu kwa sura kila siku akija ndani ya ofisi yake lazima aje hapa kunisalimia na kunipa

chochote kitu

Kama mnashida nae sifikilii kama itakuwa ni jambo rahisi nyie kuonana nae

Kwanza analindwa kingine kabla ya kumuona yeye

Kuna watu kama sita hivi mnatakiwa mpitie kwao.

Kingine ana sura nyingi huwezi kutambua yeye ni yupi,

kwakuwa Mimi ni swahiba wangu

Muda wowote ule nikiitaji kuonana nae hakuna haja ya kupitia kwa hao watu”

Mpaka hapo tukachoka hoi

ikabidi tumpatie pesa kama Elfu kumi na tano hivi ndipo akatupa Ramani nzima ya kumuona Tariq kiurahisi zaidi

Basi tukaingia ndani ya

Jengo hilo na kupandisha lift kwenda juu

Zuberi akanitizama na kusema

“Ndugu isiwe tunaenda kufa huku maana vibopa kama hawa hawataki mchezo tukawashwa chuma cha moto

Nikavuta pumzi

Na kuzishusha nikasema

“opsiii….usiogope hata kama tukifa tutakufa kishujaa yani kuileta taarifa ya msiba wa bibi ni ushujaa tosha,

Baada kumwambia vile Zuberi akabaki kutabasamu tu. Kisha akanishika

begani na kusema

“hakika wewe ni mtu wa

ajabu sana yani unajitolea maisha yako kwa ajili ya Bibi ambaye hana undugu na Wewe!”

Lift ikaweza kusimama kila mmoja akamtizama mwenzie, tukashuka na kuelekea mapokezi,

Hakika duniani kuna mabinti warembo sana huyu aliyoko mbele yangu ni mmoja wao

Binafsi binti alikuwa na uso wenye kupendeza pua utasema kapewa robo,

Midomo yenye kukufanya ushikwe na Ashki fulani hivi nikabaki kumsaminisha pasipo kumwambia chochote kile

Sauti yake tamu na nyororo ndio ikanistua kutoka kwenye dimbwi zito la kumuwaza yeye,

“Samahani Kaka yangu sijui nikusaidie kitu gani?”

Kwa sauti kidogo ya kubabaika

nikamjibu huku nikijiweka sawa mzoa takataka mie nilitokea kumpenda ghafla yule Binti

“zaa,,,saaahizi”

“nzuri tu mbona kama una wasiwasi fulani hivi nini shida”,,,,,

Nikamcheki Zuberi yeye alikuwa amekaa kwenye kiti kwa mbali kidogo na pale,

“hapana Dada yangu unajuwa tena vijana kama sisi tukiona Warembo kama nyie tunapagawa ghafla”

Nilijikuta naongea hivyo mpaka mwenyewe nikajishangaa.

Yule binti akatabasamu na kuzidi kunipa uchizi

“oky nashukuru na mie kuwemo kwenye orodha ya Warembo ehee nikusaidie nini?”

“nilikuwa namuulizia bwana Tariq wahidi kama nimemkuta au laa?

“ndio yupo je wewe ni nani yake”,,,,,,,,

“mimi ni mmoja kati ya watu wake muhimu sana kuna ujumbe nimekuja kumpatia”

“Unajuwa sio jambo rahisi kuweza kumuamini mtu hivihivi kwa sababu

Huyo mtu analindwa na mitambo maalumu kabla hujafika kwake unatakiwa upitie pale kwanza”

Yule binti aliongea maneno hayo na kunyanyua mkonga wa simu akabofya number

Kadhaa na kusikilizia

kuna maneno akaongea kwa Kizungu mie washule za Kayumba sikuelewa neno hata moja kisha akaniambia unaweza kusubiri pale maana yupo na Mgeni ndani”

Sikutaka kuuliza swali nikaenda

Kukaa pamoja na Zuberi kila mmoja kiroho kikimdunda,

Ghafla mbele yetu tukasimamiwa

na njemba kama nne hivi wametinga suti na kuamliwa tusimame

hatukuleta ubishi tukasimama na kuanza kusachiwa

Baada kuonekana hatuna siraha yeyote ile nikapewa Ruhusa ya

Kwenda kuonana na bwana Tariq kijasho chembamba kikaanza kunivuja.

Ndani ya Ofisi kubwa

Mbele kulikuwa na baba mtu mzima hivi amekaa

Baada kuniona akaweka miwani yake

Sawa, nikamuamkia

“Shikamoo Kaka”,,,,,,,,

“marhabaa kijana unaweza kukaa tu hapo kisha uniambie nini shida yako”

Nikakaa kwenye kiti huzuni ikaanza kunishika na kujikuta nadondosha mchozi,

“kijana nini shida mbona unalia tu huwongei chochote una njaa au?”

Nikamtizama usoni kisha nikafumbua mdomo wangu na kuanza kumpa full story.

Hakika alishituka sana baada

kuzisikia taarifa zile akainuka kwenye kiti na kuuliza

“yuko wapi Mama yangu,,,,,,”

Nikamjibu tayari ameshakufa”

Hakuweza kuamini akajishika kichwa na kuanza kulia akaigonga gonga meza kwa ngumi hakika

ilishangaza sana, (Why)

Akaniomba nimpeleke aweze kwenda kuuwona mwili wa Mama yake tukatoka Ofisini nikamwita Zuberi

Huku nikimtizama yule binti kwa jicho la husda mpaka mwenyewe akatambua

Baada kushuka hadi chini tukaingia kwenye gari

Safari ya kwenda Temeke ikawa imewadia,

Ndani ya gari kila mmoja alikuwa kimya huku mimi nikitoa maelezo kwa dereva

jinsi ya kufika.

Bwana Tariq machozi yalikuwa yana mrenga renga tu na kujifuta mafua yaliyomshika ghafla. Hatimae tukaweza kufika gari ikasimama tukashuka

hakika watu walikuwa wengi sana sijui hata wametokea wapi,

Rahma nae alikuwepo baada kuniona akaja mbio kunikumbatia huku analia

Bwana Tariq akaingia ndani kwenda kuuwona mwili wa bibi

Apate uwakika je ni Mama yake.

Kitendo cha kuifunua shuka tu akastuka na kurudi nyuma hakuweza kuamini kabisa

Akaangua kilio kama mtoto mdogo

“hiiiiiiiiiiihaaaaa!!!,,,,,ndio nini sasa Mama umefanya,,,,kwanini uliishi kwa kujificha mama yangu, hapana sio wewe!!!,,,,,

Kilio chake kiliambatana na maneno mengi sana embu tumsikie sisi wenyewe

“mama uliishi kwa kuiyogopa Serikali

Hukutaka kukutana na mtu yeyote yule maisha gani haya tena. Mama kwanini hukuja kwangu nilikuwa na uwezo wa kufuta kila kitu,,,,,,mama iko wapi thamani

ya utajili wangu

umeishi maisha ya magumu kiasi hiki umelala kwenye kibanda ambacho hata kuku hakustahili kuishi humu.

Mama (why)

Bwana Tariq akawa akimtikisa Mama yake kwanini amefanya yote hayo,

Nikaenda kumshika na kumsihi

Auwache mwili wa marehemu upumzike kwa Amani

huku machozi yakimtoka

Tariq akaniangalia na kusema

“nashukuru sana ndugu yangu kwahiki ulichonifanyia hakika ni jambo kubwa sana sitokaa nikasahau

Kwa wema huu. Hakika nimeweza kumuona mama yangu kwa mara ya mwisho

Japokuwa nilikuwa nikimtafuta miaka zaidi ya Kumi na tano sasa

Akanikumbatia, basi msiba ilibidi uwe nyumbani kwa Madebe nilipewa heshima hiyo nikiwa kama mtu

Wa karibu na marehemu Bibi,

Tukiwa katikati ya msiba vishankupe yani ndugu zake marehemu Madebe wakafika

yule Dada akaanza kubwata huku akitukana matusi makubwa na mazito kwa hakika siwezi kuyaandika…..

“washenzi wakubwa nyie wapumbavu msiokuwa na haya hivi mmeona hii nyumba imekuwa sehemu ya kufanyia misiba sio”,,,,,yani mnaokota mizoga huko

Na kuja kufanyia nyoko nyoko zenu

Watoto wa malaya nyie akazidi kuongea pasipo kujali kuna watu kutoka Serikalini tena matajili wakubwa wakubwa bwana Tariq kwa mwendo wa kinyonge

akanisogelea na kuniuliza

“vipi kaka huyu nani yako mbona anatutusi hadi anamwita Mama yangu mzoga!”

Nikampa maelezo japo kwa ufupi tu.

Akanielewa na kunyanyuka nikamuona anafungua mlango wa gari,

Na kutoka na Bastora

kitendo pasipo kuchelewa akafyatua risasi ikaenda kutua moja kwa moja mguuni kwa yule Dada akarushwa hewani kimo cha mbuzi na kwenda chini puhuu

wenzake aliokuja nao wakatimua mbio na Baazi ya watu wengine.

Mie nikabaki kucheka tu,

si unajuwa mkaidi hafaidi mpaka sikukuu ya iddy akataka kumtwanga nyingine sijui ya kichwa Bodyguard wake akaenda kumzuia na kumpora ile bastora.

Tariq akang’aka kwa hasira

“shenzi embu nipe hiyo kitu nimwage ubongo wa huyu kenge

yani wewe unamtusi mama yangu Mimi”,,,,,,,akamkanyaga sehemu yenye jeraha

Binti akapiga kelele za uchungu maana hayo maumivu aliyokuwa akiyapata

Usimpimie,

police wakafika na kuondoka na yule Dada bwana Tariq akaachwa pale pale

Akaja kuniambia hivi

“Salumu kaka tulia kuanzia sasa naomba ukae kando hii kesi na hawa kenge sijui kugombea Urithi usiowahusu niachie mimi.

Nikaitikia sawa Kaka”

Binafsi ulikuwa msiba uliojaza watu wengi sana tukianzia Wanamuziki hadi wabunge na mawaziri walifika

Kwa mara ya kwanza niliweza kumuona live Mwanadada mrembo

Jacklin wolper

kuna kipindi nilikuwa namuota sana ndotoni Asubuhi ikifika nimejichafua vibaya mno.

Sikuwai kuwaza wala kufikilia kama ipo siku nitaweza kumuona live dahaa,

Nikabaki kumkodolea macho tu mpaka akafika sehemu ambayo tulikuwa tumekaa Mimi na bwana

Tariq akatoa salamu kwa kushikana mikono na Tariq mapigo ya moyo yakaanza kunienda mbio

Nikitamani anishike na Mimi

Kama nilivyo tamani ndivyo ilivyokuwa akanipa kiganja chake. Jamanii”,,,,,,moyo wangu ulikuwa unadunda utasema Speaker za za studio ya Master J kwa

macho yake malegevu

akaniambia

“pole sana Kaka yangu Mungu ametoa na Ametwaa jina la bwana lihimidiwe”

Nikaitikia Ameeni”

Ndipo akaondoka kwenda kwa wengine

Walikuja wengi kutupa pole

Sijui Wema sepetu Shamsa Lulu

Wengi tu

Hatimae kesho yake tukaenda kumzika bibi kwenye makaburi ya Tandika

sikuweza kujuwa kama familia ya upande wa Baba yake wako vipi”

Kesi ya Mirathi ikaanza kuunguruma katika mahakama ya kisutu

Ni kesi ambayo inaweza kuchukuwa miaka hata mitano au zaidi

Bwana Tariq akaniambia pale nihame

Akanipa nyumba kubwa tu ya gorofa mbili kabla kesi ya mirathi haijaisha pale akavunja na kujengwa kituo cha police,

Maana katika eneo letu kituo cha police kilikuwa kipo mbali mno.

Nikaweza kufunga ndoa na Rahma sikuacha kwenda maskani kwa Washikaji zangu kule temeke kupiga nao story,

Nilikuwa natoka zangu Ilala bungoni ninapoishi na kwenda kuwatembelea washikaji nikipita ile sehemu ambayo alikuwa akiishi bibi mchozi unanitoka mwisho

natabasamu

Maana kile kibanda chake hakipo tena

Bwana Tariq kaangusha zinga la Msikiti

“Salumu kaka”

Zuberi aliniita, nikamuitikia

“naam ndugu”

“Azizi alikuwa anaomba ule Mkokoteni wako”

“Mkokoteni tena wa nini”,,,,,

“nae anataka kuwa Mzoa takataka siku moja apate zali kama lako”

Nilicheka si mchezo nikamuuliza

Azizi eti kweli akisemacho Zuberi”

Akajibu

“ahaaa wapi Zuberi jau tu mi nina mishemishe kibao kwanza bahati ya mwenzio usiilalie mlango wazi au sio kaka Salumu?”

Nikaitikia

“ndioo”

Maisha yakazidi kusonga hatimae mahakama ikatoa maamuzi haya

“kutokana na kupata udhibitisho kutoka kwa Bwana Salumu udhibitisho ambao unaonyesha moja kwa moja kama yeye ndio mrithi halali wa mali za zote za

ndugu marehemu Madebe Abdallah

Kwahiyo basi mahakama inafunga kesi hii na kumkabizi kila kitu

Ndugu Salumu!”

Nilicheka mpaka nikalia hakika sikuweza kuamini kwa yote yanayo tokea katika maisha yangu. Yani ulikuwa kama muujiza tu, japokuwa kiwanja tulikuwa tayari

tushakitoa sadaka

Allah akaweza kujaalia tukapata watoto mapacha mimi na mke wangu mpendwa

Bibiye Rahma. Kwa upande wa Mama yangu aliweza kuja kuishi kwenye ile nyumba yangu kubwa na ndugu zangu wengine familia ya Bwana Tariq ikawa kama

familia yangu na familia yangu ikawa ya bwana Tariq maisha ya upendo na furaha yakatawala

Nikawa na tabia kila movie ya kibongo ikitoka tu nikiona Jacklin wolper yupo nainunua napenda kumtizama akitabasamu akilia

Naumia pindi nionapo

Muigizaji wa kiume akimkiss sema ndio basi tena nina familia yangu

Nitafanyaje”,,,,,,,,,,

Sikuweza kuwaona tena wale wachawi.

Baada ya ziki faraja mtegemee

Mwenyezi Mungu kwa kila jambo”…….

ENDELEA KUBAKI NAMI MSINIACHE

MWISHO

Said Abdullah

^ SENIOR C E O & PUBLISHER ^ Software engineering ^ Fan of programming ^ Technology Enthusiast.. ^ System developed|C,C++&java 👇Get more news and updates

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button