Habari

Sita kuwania mchezaji bora EPL

ERLING Haaland ni mmoja wa wachezaji watatu wa Manchester City walioteuliwa kuwania tuzo ya mchezaji bora wa mwaka wa chama cha soka FA.

Mshambuliaji huyo raia wa Norway mwenye umri wa miaka 23 alifanya makubwa katika msimu wake wa kwanza England.

Alifunga mabao 52 katika michuano yote huku vijana wa Pep Guardiola wakishinda Ligi Kuu, Ligi ya Mabingwa na Kombe la FA.

Katika orodha hiyo ya wachezaji sita wamejumuishwa ne Kevin De Bruyne na John Stones.

Wachezaji wawili wa Arsenal Bukayo Saka na Martin Odegaard pamoja na mshambuliaji wa zamani wa Spurs Harry Kane, ambaye sasa yuko na Bayern Munich, wanakamilisha orodha hiyo.

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button