
SERIKALI imeahidi kutoa Sh Milioni 500, endapo timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ itafuzu fainaliza AFCON 2023.
Ahadi hiyo imetolewa leo na Waziri wa Utamaduni , Sanaa na Michezo, Dk Pindi Chana, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na mchango wa serikali katika kuongeza hamasa, ili Tanzania ishiriki fainali hizo kwa mara ya tatu.
“Kwa kutambua umuhimu wa mashindano hayo, serikali inaahidi kutoa Sh milioni 500 kama Taifa Stars itafuzu fainali hizo za Afcon 2023, naamini linawezekana,” amesema Waziri Chana na kuongeza kuwa muhimu ni Watanzania kuiunga mkono timu hiyo.
Kikosi cha Taifa Stars kwa sasa kipo nchini Misri kwa ajili ya maandalizi ya mchezo dhidi ya Uganda ‘TheCranes’ utakaopigwa Machi 24 katika mji wa Alexandria nchini Misri na baada ya hapo timu hizo zitarudiana tena Machi 28 Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salam