Teknolojia

Tope la kimiminika sasa linapatikana Tz

BIDHAA inayotumika kuchimbia visima vya mafuta, gesi na maji  ijulikanayo kama tope la kimiminika sasa inapatikana hapa nchini badala ya kufuatwa nje ya nchi.

Mhadhiri Msaidizi  kutoka Idara ya Kemia, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ( UDSM), Naswibu Kassimu amesema hayo katika mahojiano yake na HabariLEO.

Kassimu amesema changamoto kwa wachimba visima nchini wamekuwa  wakiagiza vitu vinavyochanganywa kutengeneza tope hilo nchi mbalimbali ikiwemo China, India na nyinginezo, hivyo kuchelewa kufika.

” Wachimbaji hao huingia gharama kubwa kwenye uagizaji pia wanachukua muda mwingi kushughulikia hiyo bidhaa kutoka nje, kwani huchukua takribani mwezi mmoja hadi miwili mpaka meli ifike bandarini,” amesema.

Amesema kupitia ubunifu wao wa kutumia udongo wa mfinyanzi na mabaki ya vyakula yanayotokana na mimea, wanatatua changamoto hiyo ya kuagiza bidhaa nje ya nchi.

” Hii itarahisisha uchimbaji wa visima kwa mfano visima vya maji itasaidia upatikanaji wa visima vingi pamoja na upatikanaji wa maji.

” Katika sekta ya nishati itarahisisha uchimbaji wa visima vya kitafiti katika maeneo ya gesi pamoja na uchimbaji wa visima vya kuzalisha gesi,” amesema.

Kwa maelezo yake bidhaa hiyo ni nzuri, kwani wameifanyia vipimo vya kimaabara, ina ubora zaidi ya ile inayotengenezwa na viunganishi toka nje ya nchi.

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button