Habari

Ujenzi chuji la maji Mtwara Mikindani wakamilika

UJENZI wa chujio la Maji Manispaa ya Mtwara Mikindani, mkoani Mtwara umekamilika kwa asilimia 100 na sasa wananchi wanakunywa maji safi na salama.

Mkurungezi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mhandisi Rejea Ng’ondya amesema utekelezaji wa mradi huo wenye thamani ya Sh bilioni 3.4 ulianza Octoba mwaka 2020 na sasa umekamilika.

“Hapa ninapoongea ni kwamba wananchi wanaendelea kunywa maji ambayo yameboreshwa, ni mafanikio makubwa. Lakini yote haya ni kwa sababu ya serikali ambayo inaongozwa na Mama Samia Suluhu Hassan, ” amesema.

Baadhi ya wananchi ambao wanatumia maji hayo wamesema kwa sasa wanapata maji safi tofauti na siku za nyuma, ambapo walikuwa wanatumia maji ambayo sio safi.

“Kama kuna ushuhuda wowote ambao sisi wananchi tunao hapa mtaani ni kuhusu maji ambayo kwa sasa tunatumia, ni masafi sana, yemeboreshwa kwa kiwango kikubwa na cha kuridhisha sana,” amesema Amina Omary mkazi wa Mangamba , Manispaa ya Mtwara.

Serikali kupitia wizara ya Maji ilianzisha mradi wa chujio hilo kutokana na maji yanayotumika kuwa na changamoto ya madini ya chuma na kufanya maji hayo kutokuwa salama ajili ya matumizi ya binadamu.

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button