HABARI

UN yaomba Taliban kuruhusu tena masomo ya wasichana

Wiki chache baada ya kuchukua hatamu za uongozi Agosti mwaka jana, utawala wa Taliban ulifungua tena masomo ya shule za upili kwa wavulana Septemba 18, lakini ukapiga marufuku masomo hayo kwa wasichana. Kwa mujibu wa shirika la habari la AFP, miezi michache baadaye, hapo Machi 23, wizara ya elimu iliruhusu wasichana kurudi shuleni, lakini saa chache baadaye, uongozi wa Taliban ulibatilisha hatua hiyo.

Tangu wakati huo, zaidi ya wasichana milioni 1 wamenyimwa haki ya elimu kote nchini, kulingana na ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa Afghanistan UNAMA. Mkuu wa UNAMA Markus Portzel kupitia taarifa amesema kwamba marufuku hiyo ni aibu na ingezuilika. Ameongeza kusema kwamba ni hatua inayoathiri kizazi kizima cha wasichana nchini Afghanistan.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button