HABARI

Upinzani Ghana wapinga matokeo ya urais

Upinzani nchini Ghana umeyapinga matokeo ambayo yamempa ushindi wa kuongoza awamu wa pili, Rais Nana Akufo-Ado na kusema watakata rufaa kupinga matokeo rasmi yaliyotangazwa na tume ya uchaguzi.

 Haruna Iddrisu, ambae ni mbunge wa chama cha upinzani cha National Democratic Congress NDC, amesema kuna ushahidi wa kutosha ambao unawafanya wao wasikubaliane na matokeo.

Hatua hiyo ni baada ya Tume ya Uchaguzi wa Ghana, kumtangaza Rais Addo wa chama cha New Patritiotic, NPP, kuwa ni mshindi wa asilimia 51.59 za kura na kumbwaga mpinzani wake kiongozi wa chama NDC, John Mahama.

Taifa hilo la Afrika Magharibi linajulikana kwa sifa ya demokrasia thabiti, lakini mivutano iliongezeka Jumanne baada ya Mahama kudai kushinda kwa wingi wa bunge na kumuonya hasimu wake Nana Akufo-Addo, dhidi ya wizi wa kura.

Publisher

Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button