Biashara

Vijana 200 kunufaika kilimo biashara Tanga

HALMSHAURI ya Jiji la Tanga, imetenga eneo lenye ukubwa wa hekari 200, ambalo wanatarajia kuligawa kwa vijana wapatao 200, ili waweze have kujishughulisha na kilimo biashara  kwa lengo la kuwasaidia kujikwamua kiuchumi.

Akitoa taarifa hiyo Mkurugenzi wa Jiji la Tanga, Dk Sipora Liana, amesema kuwa kwa kushirikiana na shirika la Botner Foundation, wanatarajia kuwawezesha vijana kuingia kwenye uchumi wa kilimo kama ilivyo azma ya serikali.

Amesema kutokana na jiograhia ya Tanga, aridhi yake ambayo inastawi mazao mbalimbali, itasaidia sana kuufungua mkoa huo kupitia sekta ya kilimo, huku ikienda kuakisi kwa vitendo kauli mbiu ya sasa inayosema: ‘Tanga lango kuu la uchumi Afrika Mashariki’.

“Tumeweza kupate eneo la hekari 200 tutalisafisha tukishirikiana na shirika la Botner Foundation, tuweze kuwagawia waweze kulima mbogamboga na kisha kuwaunganisha na masoko ya mazao yaliyoko kwenye nchi jirani kama Comoro na Kenya,” amesema.

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button