Biashara

Wafanyabiashara kampuni 100 China waja

WAFANYABIASHARA kutoka kampuni 100 nchini    China wanatarajiwa kuja Tanzania kwa lengo la kufanya mazungumzo na kampuni zilizopo nchini.

Wafanyabiashara hao wanaotarajiwa kufika nchini Septemba 20, 2023 watazungumza juu ya masuala ya uwekezaji na biashara.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Balozi wa Tanzania nchini China, Mbelwa Kairuki, ujumbe huo wa wafanyabiashara utakuwa nchini kwa muda wa wiki moja.

“Makampuni hayo yatakutana na makampuni ya Tanzania kwa ajili ya kuzungumzia fursa za ushirikiano katika biashara na uwekezaji,” amesema Balozi Kairuki.

Kwa upande mwingine Balozi huyo aliutaarifu umma kuwa wafanyabiashara wa Tanzania wamepata fursa ya kuonesha na kuuza bidhaa zao katika maonesho ya China-Africa Trade and Commodity Expo siku kuanzia Novemba 13-15 mwaka huu.

Balozi Mbelwa alisema maonesho hayo ambayo hayatakuwa na malipo yatafanyika jijini Jinhua katika Jimbo la Zhajiang.

“Wafanyabiashara hao watapewa nafasi za kuonesha bidhaa na huduma ya malazi bila malipo,” alisema.

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button