Habari

Warusi wazidi kuwa matajiri zaidi

THAMANI ya pamoja ya watu tajiri zaidi Urusi imeongezeka kwa dola bilioni 10.4 tangu Januari mwaka huu licha ya vikwazo vya Magharibi vilivyowekwa kwa wafanyabiashara wa nchi hiyo, Bloomberg imeripoti.

Vladimir Potanin, mmiliki wa kampuni kubwa ya madini ya Norilsk Nickel, ameongoza kwa mara nyingine tena kuwa mfanyabiashara tajiri zaidi wa Urusi kwenye orodha hiyo, huku utajiri wake ukikadiriwa kuwa dola bilioni 28.5, ripoti hiyo ilionyesha.

Leonid Mikhelson, mmiliki mwenza na mtayarishaji wa pili wa gesi asilia wa Urusi Novatek, alichukua nafasi ya pili. Ameripotiwa kupata dola milioni 516, na kufikisha utajiri wake hadi dola bilioni 25.1.

Vladimir Lisin, mbia mkuu wa kampuni ya chuma ya NLMK ya Urusi, aliorodheshwa kama mfanyabiashara tajiri wa tatu wa Urusi. Amepata dola milioni 905 tangu mwanzo wa mwaka, na kuongeza utajiri wake hadi dola bilioni 20.8.

Lisin alifuatiwa na Alexey Mordashov, mwenyekiti wa kampuni kubwa ya chuma ya Severstal, ambaye alichukua nafasi ya nne kwenye faharisi, akiwa na jumla ya dola bilioni 20.2. Utajiri wake umeongezeka kwa dola bilioni $1.54.

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button