Habari

Watanzania kushindana gofu watoto Uganda

TIMU ya watoto ya mchezo wa gofu ya Tanzania inatarajia kushiriki shindano la All Africa Juniors jijini Kampala, Uganda kuanzia Aprili 17-21 mwaka huu.

Akizungumza jijini Dar es Salaam,  Mwekititi wa Chama cha Mchezo wa Gofu nchini (TGU),  Girman Kasiga amesema, timu hiyo inajumisha wachezaji nane, ambao wamefanya maandalizi ya kutosha.

“Watoto wamejiandaa vya kutosha wanasubiri siku husika waweze kwenda kushindana, ni matumaini yangu watafanya vizuri, ” amesema na kuongeza timu hiyo itaondoka nchini Aprili 15:

Kwa upande wake Rais wa Chama cha Mchezo wa Gofu Wanawake (TLGU), Queen Seraki amezishukuru klabu za gofu nchini zinazowakuza vijana wadogo katika mchezo huo na ameomba Watanzania waendelee kuunga mkono mchezo huo.

Naye mmoja wa wachezaji wataakoshiriki shindano hilo Shufaa Hassan kutoka Klabu ya Lugalo  amesema, wamejiandaa vizuri kimashindano na wanaamini watarudi na ushindi.

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button