Habari

Watatu mbaroni mauaji ya Daktari Tarime

JESHI  la Polisi Tanzania limesema limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa watatu wanaodaiwa kumuua Dkt. Isack Daniel Athumani Sima aliyekuwa Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Nyamongo katika Halmashauri ya Wilaya ya Tarime mkoani Mara.

Watuhumiwa hao walitekeleza uhalifu huo Mei 3, 2023 na kukimbilia Mwanza na baadaye Dar es salaam.

Msemaji wa Jeshi Polisi Tanzania, David Misime akizungumza amesema Dk Isack aliuliwa akiwa ametoka kazini majira ya usiku.

“May 03,2023 Dk. Isack aliuawa akiwa anatokea kazini, Watuhumiwa watatu waliofanya mauaji hayo pamoja na kukimbilia Mwanza na baadaye Dar es salaam wamekamatwa na Askari wetu waliobobea katika uchunguzi wa matukio ya mauaji, uchunguzi unakamilishwa ili wafikishwe Mahakamani.”Amesema

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button