Habari

Wawili wapandikizwa uume

WANAUME wawili waliokuwa na matatizo ya  nguvu za kiume kutokana na matatizo mbali mbali ya kiafya, wamefanyiwa upasuaji na kupandikizwa uume katika Hospitali ya Benjamini Mkapa (BMH) kwa kushirikiana na Chama cha Madaktari Bingwa wa upasuaji wa mfumo wa mkoji nchini (TAUS) pamoja na Daktari bingwa kutoka nchini Ufaransa.

Upasuaji huo wa kupandikiza uume umefanyika katika hospitali hiyo iliyopo mkoani Dodoma kwa mara ya kwanza.

Akizungumza Daktari Bingwa wa magonjwa ya mfumo wa mkojo kutoka Hospitali ya Benjamini Mkapa Remigius Rugakingira amesema upandikizaji huo wa uume umefanyika kwa mara ya kwanza nchini.

“Hii ni mara ya kwanza kwa Tanzania kufanya upasuaji wa aina hii kilichofanyika hapa ni kuweka vipandikizi maalumu vitakavyowezesha uume kurudi katika hali yake ya kufanya kazi.”Amesema

Dkt. Rugakingira amesema Hospitali ya Benjamin Mkapa inajali afya ya Wanaume na upasuaji kama huu unaweza kufanyika Tanzania na kuwataka wanaume wenye matatizo ya nguvu za kiume kufika hospitali ya BMH kufanya upasuaji wa kuweka vipandikizi kwenye uume kwani ndio hospitali pekee kwa sasa inayotoa huduma hiyo hapa nchini.

 

 

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button