Habari

Yaliyompaisha Samia 2022

RAIS Samia Suluhu Hassan ametekeleza kwa vitendo falsafa yake ya Kazi Iendelee katika kipindi cha mwaka huu kwa kuhakikisha miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ya kimkakati haikwami kwa sababu yoyote ile.

Baada ya kuapishwa kuwa Rais Machi mwaka jana, baadaye, Rais Samia alikuja na falsafa yake ya ‘Kazi Iendelee’ inayolenga kuendeleza falsafa ya mtangulizi wake, hayati John Magufuli ya ‘Hapa Kazi Tu’.

Wakati mwaka huu unaendea ukingoni, Watanzania wameshuhudia namna Rais Samia alivyoisimamia na kuitekeleza falsafa yake ya Kazi Iendelee kwa vitendo kwa kuhakikisha miradi yote ya kimkakati inaendelezwa na kukamilishwa na miradi mipya ikianzishwa.

Miongoni mwa miradi hiyo ya kimkakati ni ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) kutoka Dar es Salaam hadi Mwanza na kutoka Dar es Salaam hadi Kigoma ambapo wakati anaapishwa kuwa rais mwaka jana, ujenzi wa kipande cha Dar es Salaam hadi Morogoro kilikuwa chini ya asilimia 90.

Wakati utiaji saini wa ujenzi wa kipande cha SGR Tabora-Kigoma hivi karibuni, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Masanja Kadogosa alisema ujenzi wa SGR katika vipande vyote unaendelea vizuri.

Kadogosa alibainisha kuwa Serikali ya Rais Samia imefanikiwa kuendeleza ujenzi huo ambao mpaka sasa ujenzi kutoka Dar es Slaam hadi Morogoro umefikia asilimia 97.67, Morogoro-Makutupora (asilima 91.32), Makutupora-Tabora (asilima 3.26), Tabora-Isaka (asilima 0.49) na Isaka-Mwanza (asilimia 19.70).

Mradi mwingine wa kimkakati ni ujenzi wa Bwawa la Julius Nyerere (JNHPP) la kuzalisha umeme wa maji Mto Rufiji. Wakati anazindua ujazaji maji wa bwawa hilo Desemba 22 mwaka huu, Rais Samia alisema alikuta ujenzi wa mradi huo ukiwa asilimia 37 wakati anaingia madarakani lakini mpaka alipozindua ujazaji maji ujenzi wake ulikuwa umefikia asilimia 78.68.

“Namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunipa uwezo wa kuuendeleza mradi mhuu,” alisema Rais Samia. Waziri wa Nishati, January Makamba, katika kuonesha mradi huo unakwenda vyema, alisema kuwa maneno yanayozushwa kuwa mradi huo unacheleweshwa au umekwama au unazorota siyo ya kweli baada ya Rais Samia kuzin dua ujazaji maji.

Pia falsafa ya kazi iendelee imemwezesha Rais Samia kuen deleza ujenzi wa Daraja la John Magufuli la Kigongo-Busisi mkoani Mwanza lenye urefu wa kilometa 3.2 kwa gharama ya zaidi ya Sh bilioni 700.

Wakati alipotembelea ujenzi wa daraja hilo Juni mwaka jana, ujenzi wake ulikuwa umefikia asilimia 27 lakini mpaka sasa kwa mujibu wa Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) Mkoa wa Mwanza, Pascal Ambrose, ujenzi wa daraja hilo umefikia asilimia 63.

Kuhusu utekelezaji wa ujenzi wa barabara ya njia nane kutoka Kimara hadi Kibaha yenye urefu wa kilometa 19.2, katika kipindi cha mwaka huu, Serikali ya Rais Samia imefanikiwa kuuendeleza mradi huo.

Mradi mwingine mkubwa ambao Rais Samia na serikali yake ameanza kuutekeleza ni mradi wa Kuchakata na Kusindika Gesi Asilia (LNG) ambao Juni mwaka huu ali shuhudia Ikulu Dodoma utiaji saini makubaliano ya awali ya mkataba wa nchi hodhi (HGA) kwa ajili ya kuchakata na kusindika gesi hiyo.

Siku hiyo, Rais Samia alisema mradi huo utagharimu Sh trilioni 70 na kwa mujibu wa tafiti asilimia 10 sawa na Sh trilioni saba zitatumika hapa nchini katika kipindi cha ujenzi wa mradi utakaochukua miaka minne hadi mitano na kutoa ajira 10,000 hadi kukamilika.

Miradi ya maji

Katika kuhakikisha Watanza nia wanapata maji safi na salama, katika kipindi cha mwaka huu, Rais Samia amezindua miradi ya maji katika maeneo mbalimbali uki wemo mradi wa maji Kigamboni. Novemba 11 mwaka huu, alizindua mradi wa maji Kigamboni ambao unatoa lita milioni 70 za maji kwa siku kwa ajili ya wakazi wa maeneo mbalimbali ya Dar es Salaam.

Pia ameanza utekelezaji wa mra di mkubwa wa Bwawa la Kidunda wenye thamani ya Sh bilioni 329 utakuwa na uwezo wa kuhifadhi maji kwa miaka mitatu ili kupun guza changamoto ya upatikanaji wa maji kwa Mkoa wa Dar es Salaam.

Agosti mwaka huu, Rais Samia alizindua mradi wa maji wa Mbalizi (Shongo-Igale) uliogharimu Sh bilioni 3.345.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Anthony Sanga, alimweleza Rais Samia kuwa mradi huo pia umehusisha ujenzi wa tangi la lita milioni 1.5 la kuhifadhia maji na utakuwa na uwezo wa kuzalisha lita kati ya milioni nane hadi 12 na kuhudumia wakazi 80,000 wa Mbalizi.

Hii ni baadhi tu ya miradi ya maji aliyoizundua mwaka huu, lakini kuna miradi mingi ya maji inayotekelezwa katika maeneo mbalimbali nchini.

Vyeti feki
Jambo jingine kubwa ambalo Rais Samia amelifanya katika kipindi cha mwaka huu ni uamuzi wake wa kuridhia watumishi wa umma walioondolewa kazini kwa sababu ya vyeti feki kulipwa michango yao waliyochangia kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii.

Kutokana na hatua hiyo ya rais, utekelezaji wa jambo hilo ulianza rasmi Novemba kama alivyobainisha Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Profesa Joyce Ndalichako.

Uwekezaji
Miongoni mwa mambo makub wa aliyoyafanya Rais Samia katika kipindi cha mwaka huu ni kuvutia wawekezaji hapa nchini kutoka nchi mbalimbali.

Ili kufanikisha hilo, alitembelea nchi mbalimbali duniani ikiwemo Falme za Kiarabu (UAE) ambako aliwataka wafanyabiashara na wawekezaji kutoka UAE na kote duniani kuja kuwekeza Tanzania.

Wakati akifungua siku ya kitaifa ya Tanzania katika maonesho ya Dubai 2020 Februari mwaka huu, Rais Samia aliwaambia wafanyabi ashara na wawekezaji kutoka nchi zaidi ya 190 walioshiriki maonesho hayo kuwa Tanzania inafungua mlango kwa yeyote anayetaka kutembelea, kuwekeza na kufanya biashara hapa nchini.

Kutokana na jitihada hizo, Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kupitia Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wake, John Mnali, kilisema kuwa kimesajili jumla ya miradi 132 yenye thamani ya Dola za Marekani bilioni 3.16 sawa na Sh trilioni 7.376 katika kipindi cha miezi mitano kuanzia Julai hadi Novemba mwaka huu.

Elimu Katika kuhakikisha sekta ya elimu inaboreka, mwaka huu ametoa Sh bilioni 160 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa 8,000 ili wanafunzi wanaomaliza darasa la saba na kufaulu wote waingie sekondari, ujenzi ambao umeshakamilika. Pia ametoa ufadhili kwa watoto 640 waliofanya vizuri kwenye masomoya sayansi ili wasome bure elimu ya juu.

Royal Tour
Kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa Covid-19, sekta ya utalii kama ilivyo sekta nyingine iliathirika kwa kiasi kikubwa hali iliyomsukuma Rais Samia kurekodi Filamu ya Royal Tour ambayo aliizindua Mei mwaka huu Dar es Salaam baada ya kufanya hivyo nchini Marekani na jijini Arusha.

Hilo ni moja ya mambo makubwa aliyoyafanya mwaka huu. Wakati akizindua filamu hiyo alisema sekta ya utalii imeajiri asilimia 4.5 ya Watanzania na wakati Covid-19 utalii ulishuka kwa asil imia 27 na watu 412,000 walipoteza ajira, hivyo akaamua kuitangaza Tanzania ili kuirejesha sekta katika hali yake ya awali.

Moja ya matunda ya filamu hiyo ya Royal Tour ni ujio wa meli kubwa ya kitalii ya Zaandam mwanzoni mwezi uliopita ikiwa na jumla ya watalii 1,060 kutoka Marekani waliokuja kutembelea vivutio mbalimbali vya utalii nchini.

Ujio wa meli hiyo ulimfanya Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Amos Nnko kusema “Tunamshukuru Rais Sami akwa sababu ujio wa meli hii ni matokeo ya kazi nzuri inayofanywa na serikali chini ya uongozi wake, ni matunda ya filamu ya Royal Tour aliyoiasisi.”

Ajira

Katika kipindi cha mwaka huu, Rais Samia ameajiri watanzania wengi na miongoni mwake ni taarifa ya Juni mwaka huu inaeleza alitoa kibali cha ajira kwa kada za ualimu 9,800 na wataalamu

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button