

Hali ya usalama katika jiji la Bakhmut nchini Ukraine kwenye mstari wa mbele wa mashariki, inazidi kuwa ngumu zaidi na zaidi Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesema.
Imeelwa vikosi vya Urusi vimekuwa vikijaribu kuuteka mji huo kwa zaidi ya miezi sita. “Adui anaharibu kila kitu ambacho kinaweza kutumika kulinda nyadhifa zetu”. Zelensky alisema.
Matamshi ya kiongozi huyo wa Ukraine yametolewa wakati Waziri wa Fedha wa Marekani, Janet Yellen akiionya China dhidi ya kuipatia Urusi silaha wakati wa ziara yake mjini Kyiv Jumatatu.
Mapigano makali zaidi tangu Urusi kuivamia Ukraine mwaka mmoja uliopita yametokea katika eneo la Bakhmut, katika eneo la Donetsk nchini Ukraine, ambalo sehemu yake iko chini ya udhibiti wa Urusi na majeshi yake.